Bila Ubinafsi Hamfiki Popote

Bila Ubinafsi Hamfiki Popote

Companero

Platinum Member
Joined
Jul 12, 2008
Posts
5,609
Reaction score
1,738
Ndivyo wanavyosema wachambuzi wanaolinganisha maendeleo ya taasisi za kiuchumi na kisiasa katika nchi mbali mbali. Wanasisitiza kuwa kuwa tatizo la jamii zetu ni kuwa zinaendekeza sana kusaidiana na kuaminiana wenyewe kwa wenyewe. Nchi zetu ni maskini na zitaendelea kuwa hivyo, wanaendelea kusema, kama tutaendelea kubebana.

Ili tuendelee, wanadai wataalamu hao, inabidi tuwe na taasisi ambazo msingi wake wa kuaminiana unakuwa umejikita katika mikataba/makubaliano rasmi hasa kati ya watu wasiojuana. Hili, wanaendelea kudai wachumi, wanahistoria wa uchumi na wachambuzi wa sayansi ya siasa, litasaidia kujenga ufanisi katika mahusiano ya kibiashara na kiuchumi.

Hakuna nchi yoyote ambayo imeendelea ilhali watu wake wamefungwa katika minyororo isiyo rasmi ya kidugu, chambuzi za wanazuoni hao zinadai. Wanasema hata tuzunguke vipi hatuwezi kukutana na jamii yoyote ambayo imepiga hatua kubwa huku watu wake wakiwa wanaishi maisha ya undugu wa kupanga kwa matofali. Hivyo, eti, tukitaka kusonga mbele lazima tuachane na mifumo isiyo rasmi.
 
Back
Top Bottom