PreGE2025 Bila Polisi CCM wepesi kama karatasi

PreGE2025 Bila Polisi CCM wepesi kama karatasi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
16,818
Reaction score
62,030
Anachotendewa mheshimiwa Lissu ni ushahidi wa wazi kuwa CCM uwezo wake mdogo sana kisiasa, na bila mabavu ya polisi hawewezi kudumu kisiasa hata kwa mwaka mmoja!.

Wamepigwa operesheni moja tu ya NO REFORMS NO ELECTION, wamekimbilia polisi. Hii ikuonyeshe kuwa hiki chama ni genge la watu wepesi sana kisiasa. Na genge hili linachokiweka hai ni kwa sababu limekaa mainroad ya ulaji, au upigaji. Kwa hiyo mafisadi wako tayari kutumia kila aina ya violence kunyamazisha sauti za haki na mageuzi nchini.

Lakini hii pia inatuonyesha dalili ya Genge linalokaribia kufika mwisho, na sababu kubwa ni kuwa hili genge halina cohesion ya kisiasa,halina unanimity ya kisera wala mipango mkakati ya kulivusha taifa kisiasa na kiuchumi. Kiufupi genge hili ni kama genge la wachawi, urafiki gizani halafu kila mmoja asubuhi na lwake.

Hakuna marefu yasiyo na ncha, Genge hili limeshindwa kutatua shida za wananchi, halina vision wala uwezo wa kuleta maendeleo. Akili yao ni kuwaza kukopa nje, kupewa misaada hata kama ni kujengewa matundu ya vyoo na kupiga blahblah wakati maisha ya wananchi yakizidi kudidimia. Kwa hivyo ni dhahiri genge hili linakaribia kufika mwisho. Inahitajika ujasiri kidogo tu wa wananchi kukataa ujinga ili kuleta reforms za msingi nchini.

Kumkamata Lissu kumewaacha weupe mbele ya umma na dunia kuwaona jinsi fragile walivyo.
Wameshindwa Siasa wanakimbilia polisi.
Poor them!
 
Back
Top Bottom