Naomba tuache ushabiki,unafiki,na siasa zisikuwa na msingi...! siku zote penye ukweli uongo unajitenga pembeni, na siku zote mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni...!
Ni jambo lilokuwa wazi, mwenye macho mwenyewe anaona,...bila juhudi,uvumilivu na utashi wa Mh.Freeman Aikael Mbowe pamoja na kushirikiana vizuri na makamanda wengine! CHADEMA leo kingekuwa sawa na CUF,TLP,NCCR MAGEUZI na hata kisingekuwa na mbunge hata mmoja kama SAU,APPT,TADEA,MAKINI..kutokana na Nguvu kubwa ya chama tawala CCM..,Ambacho kimekuwa kikitumia kila iana ya silaha kushambuliwa upinzani kama kununua baadhi ya viongozi wakuu katika vyama vya upinzani,kutumia nguvu ya dola (polisi,makachero),kutumia sera za udini na ukabila kuvishambulia vyama vya upinzani..!
Napenda nikupongeze na kukutia moyo mh.Mbowe ingawa kuna baadhi wanaongea sana na kukukwaza lkn najua ushawafahamu na ni mbinu siku zote inayotumiwa na CCM kuvuruga upinzani ikiwamo kuunda makundi ama kununua baadhi yenu kuwadhoofisha ama kuwagombanisha na ni mara kwa mara baadhi ya wabunge wenu waliwahi kuwasiliti ama kununuliwa ama kushawishika..,lakini kwa umoja,ushirikiano wa chama..,naona uongozi wako bdao upo makini kudhibiti sumu zote za CCM..!
Wengi wanasema CHADEMA ni chama cha wachaga...,hivi mjiulize mwaka 2005 Kikwete kwenye kampeni za uraisi alifanya harambee moshi mjini na kukusanya zaidi ya Mil.200 kwaajili ya kurudisha jimbo la moshi mjini CCM,..hivi waliochangia hizo pesa walitoka wapi..? na wajikumbushe tena miaka ya 2000 na 2005 chama cha CUF kilikuwa na nguvu kubwa ya Upinzani zikaendeshwa propaganda kwamba CUF ni chama cha Kiislamu na hao hao CCM..,sasa hv CHADEMA kina nguvu wameanza kukiita chama cha kikristo..,hizo ni siasa majitaka..!
Mh.Freeman Mbowe ndio alikuwa mtu wa kwanza kuasisi uvaaji wa kombati,matumizi ya teknolojia katika kampeni kama ya helikopta,alikuwa akifinance chama kipindi chama kilikuwa kikipata ruzuku kiduchu kutokana na idadi ya wabunge kuwa ndogo, alimpiga tafu sana Dk.Slaa kipindi cha 2005 kwenye ubunge ambako alifanyiwa mizengwe ya ajabu...,na pia ndiye alikuwa ni mmoja ya washawishi wakubwa kumshauri dk.slaa agombee uraisi..,na pia aliwalea vizuri watu kama john mnyika,halima mdee,nasari na kuwapa fursa wataalamu kutoa ushari kama tundu lissu,prof.baregu,kitila mkumbo na n.k, nani halijui hilo..,na hata mh.zitto kabwe aliwahi kukiri mbowe ndio alikuwa akimsaidi kipindi akisoma chuo kikuu
Tatizo watz ni wavivu sana wa kusoma historia,...viatu vya uenyekiti vimemkaa vizuri sana mh.mbowe...,bila yy sidhani kama chadema kingepiga hatua kubwa kama sasa hv akisadiana vizuri na mzee mtei na mh.ndesamburo