Bila Lissu Bungeni tungeburuzwa sana

Bila Lissu Bungeni tungeburuzwa sana

Mlulajr

Member
Joined
Mar 21, 2015
Posts
80
Reaction score
49
Kwakweli huyu Mh. Lissu anajua nini kimempeleka bungeni, hakyanani Mungu aendelee kumlinda.

Dodoma. Hoja 22 za kupinga vifungu Muswada wa Sheria ya Makosa ya Mtandao wa mwaka 2015 zilizotolewa juzi na Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu jana zilisababisha kikao cha 14 cha Bunge kuvunja rekodi ya kutumia muda mrefu baada ya kumalizika saa 6.15 usiku.

Marekebisho yaliyowasilishwa na Lissu yaliungwa mkono na Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika ambaye pia alikuwa na marekebisho yake katika muswada huo, hivyo wote wawili kuichachafya Serikali bila mafanikio baada ya muswada huo kupitishwa kwa sauti kubwa ya "Ndiyooo" ya wabunge wa CCM.

Kuanzia saa 12.30 jioni, Bunge lilikaa kama kamati kupitisha muswada huo baada ya kumaliza kuupitisha muswada wa Sheria ya Miamala ya Kielektroniki ambao haukuwa na mvutano mkali.

Mvutano wa kisheria kati ya Lissu dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), George Masaju, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa, naibu wake, January Makamba ulianza saa 12.30 jioni hadi saa 5.30 usiku na baadaye Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akatumia muda uliosalia kuahirisha Bunge.

Mpaka inafika saa 5.00 usiku wabunge wa upinzani waliokuwapo bungeni walikuwa 12 tu, akiwamo Lissu na Mnyika na hivyo kufanya idadi ya wabunge wote kuwa 86, wakiwamo wa CCM na mawaziri.

Kuna wakati Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM), Andrew Chenge alilazimika kusimama kutoa ufafanuzi wa kina, ikiwa ni pamoja na namna ya kuvitamka kwa ufasaha vifungu vya sheria ili kukubalika na pande mbili zilizokuwa zinavutana.

Mapendekezo yote yaliyotolewa na Chenge ambaye amewahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, yaliungwa mkono na Lissu pamoja na Masaju na Wizara ya Mawasiliano.

Wakati mnyukano huo ukiendelea, Pinda alikuwa kimya akisubiri kusoma hotuba yake ya kuahirisha Bunge.

Pinda alianza kusoma hotuba hiyo saa 5.30 usiku mpaka saa 6.00 usiku, ikiwa ni baada ya Bunge kuupitisha muswada huo. Baada ya dakika 15 za kutoa matangazo mbalimbali na kuwashukuru wabunge, Spika Makinda aliahirisha mkutano huo.

Kuna wakati Lissu aliwataka wabunge kutochoka kutokana na hoja anazozitoa kusababisha kikao hicho kuwa kirefu, huku Makinda naye akiwaeleza wabunge kuwa ‘zege halilali', akimaanisha kuwa Bunge haliwezi kuahirishwa mpaka muswada huo upitishwe na Pinda atoe hotuba ya kuahirisha Bunge.

Kati ya marekebisho 22 yaliyowasilishwa na Lissu, ni matano tu yaliyokubaliwa na Serikali huku Lissu akikubali vifungu viwili tu vilivyofanyiwa marekebisho na Serikali, akivisifia kuwa vimeandikwa kama sheria inavyotaka, lakini vingine akiviita vya ovyo na sheria inayotungwa ni mbaya yenye malengo ya kuwakomoa baadhi ya watu.

Ilivyokuwa
Hoja kubwa iliyozua mabishano ya kisheria ni muswada huo kutokuwa na tafsiri ya baadhi ya maneno yakiwamo, ‘matumizi ya mfumo wa kompyuta kinyume cha sheria', ponografia ambayo yanatengeneza kosa kwa mujibu wa sheria hiyo.

Vilevile, ulitokea ubishi katika hoja ya kuingilia mawasiliano kinyume cha sheria ambacho adhabu yake ni kifungo kisichopungua mwaka mmoja au faini isiyopungua Sh5 milioni, ikipendekezwa kuwa yaingizwe maneno ‘kwa nia mbaya au kwa makusudi', ili kuwalenga wenye nia ovu na kuwaacha wale watakaoingilia mawasiliano kwa bahati mbaya.

Mbunge huyo wa Singida Mashariki alikipinga kifungu cha 14 kinachozuia utazamaji wa filamu za ngono, akitaka kifutwe chote kwa maelezo kuwa kinawazuia watu wazima kutizama filamu hizo, isipokuwa kwa watoto.

"Filamu hizi zinaonyeshwa katika majumba ya sinema na hii ni biashara halali. Kifungu hiki kinasema ukionyesha hiyo filamu ukikutwa unatozwa faini Sh30 milioni au kifungo cha miaka 10," alisema Lissu na kufafanua kuwa sheria hiyo inalenga kuwageuza Watanzania kuwa watawa na mapadri na si kupiga marufuku makosa ya mtandao.

Hoja ya Lissu ilitolewa ufafanuzi na Profesa Mbarawa, Makamba na Masaju, huku Lissu akisisitiza kuwa neno ‘ponographia' halijatolewa ufafanuzi katika sheria, lakini ilipingwa na kifungu hicho kupitishwa.

Lissu pia alipinga kifungu cha 19 kinachozungumzia mauaji ya kimbari akitaka kifutwe kwa maelezo kuwa muswada huo haujaeleza mauaji ya kimbari ni kitu gani.

Chanzo: Mwananchi
 
Watu walewale,akili zilezile na mbinu zilezile



Ni miaka sasa hamsini,watanzania wakishuhudia chama kinachojinasibu kuwa makini kikiendelea kuvurunda,na kwa kuwa watoto( raia wa Tanzania), wamekulia humo, wamelelewa humo imefika sehemu wamejengewa utamaduni wa kuona shida za umaskini Mungu kawaumbia,kukisa maji,umeme na Elimu bora wanasema Mungu ndio katuumba hivyo.

Wakati wakiwaza hivyo Nchi kama Singappre ambayo wananchi wake huishi kwa kutegemea Utalii na bandari,wanafurahia maisha na kujiona Mungu kawapa nchi ya maziwa na Asali.

Barabara za Singapore ni za kisasa,telnolojia,Elimu,Uchumi umelisukuma Taifa hili mbele ambalo wakati tunapata uhuru 1961 nao walipata mwaka uleule kwa umaskini waliokuwa nao,lakini kwa sasa wako kwenye Tiger countries.


Wakuu,nimeona niwape Muda kuitafakari ccm na sera zake.

BARABARA

Tangu uhuru,ujenzi wa barabara ni wa hovyo,huwezi kushangaa zinajengwa ndogo hata ile akili ya baadae kujenga Flyover kama Singapore haiwezekani.

Mathalani barabara ya kutoka Ubungo hadi feri haikubuniwa kuacha nafasi ambapo tungejenga barabara hizo,ukiuliza utaambiwa tumethubutu tuneweza na tunasonga mbele!

SHERIA

Mwaka 1995, Dr Masha akigombea jimbo la Sengerema na Dr wiliam Shija,kama kawaida aligawa mipira,majezi na kununua Ng'ombe wa kula wananchi,uchaguzi ulipofika akashinda,lakini Dr.Masha( baba yake L.Masha aliyekuwa waziri wa Mambo ya ndani) akapeleka shitaka akashinda uchaguzi ukarudia, Dr.Shija akafanya vilevile mahakama ikatengua uchaguzi huo,

Baada ya shija kuona hivyo,haraka wakashauriana na Sumaye waziri Mkuu wakaleta mswada bungeni wa takrima maana walikuwa wanaelekea uchaguzi wa 2000 ambao kwa tabia zao ungewapa shida,mswada ulipita harakaharaka.

Mwaka 2004, ulipelekwa mswada wa fedha za uchaguzi,hofu ilikuwa kwamba,Chadema watapata wafadhili tuwabane,lakini mwisho wake ccm hiyohiyo hata haikuwahi kutangaza wafadhiri wao walikuwa akina nani uchaguzi ule na 2010 pia.

Mwaka huu 2015, watanzania wameamuka,waandishi wa habari na vyombo vyao vimeamuka wanapashana na kuzifuatilia habari za uongo na za kweli kutoka ndani na nje ya nchi,
Wanafuatilia habari za kweli na za uongo ndani ya idara za serikali,taasisi,na chama cha Mapinduzi,si hapo tu hata vyama vya upinzani vya kweli na vile vya ccm.

Kuona kuwa ccm itakamatwa vizuri juu ya ukweli wa mambo, juu ya ahadi takribani 350 alizoahidi Rais Jk tangu 2005-2015 zimeota mbawa,Ccm inapeleka sheria kali ya vyombo vya habari na watumiaji wa mitandao,lengo kubwa ni kujilinda dhidi ya uchaguzi baada ya hapo utafanyiwa marekebisho.Unawezaje kupeleka hati ya dharura bungeni?

Watanzania tumevumilia sana,sasa tuseme uendeshaji wa nchi kwa staili hii basi,tumechoka udikteta ccm iondoke madarakani

Watanzania,tuliambiwa kuwa kila shule iwe na darasa la Awali,niwaulize hapa Dar es salaam wanasomaje?, hii ni baada ya Pr.Lipumba kusema atahakikisha shule zote zina shule za awali

Dr.Slaa aliposema atahakikisha anawatengenezea wananchi katiba bora,muliona ccm ilivyodandia gari kwa mbele!

Usafiri wa baharini
Ccm imenunua boti ya ajabu inayotumia masaa matatu kufika Bagamoyo , Badala hata ya kuwanunulia usafiri wananchi wa Kisiwa chetu cha Mafia ambao tangu 1961 wanasafiri kwa mashua.

Hivi sasa ccm inapita kila wilaya,kupitia TASAF kuwahimiza watendaji wa vijiji na Mitaa kupita nyumba kwa nyumba kubaini famili maskini ili watoto wao walipie Ada,wazazi wawape mikopo ili wajiendeshe.wameshindwa kwenye MkUKUTA&MKURABITA ,watoto wameishi tangu 2005-2015 wakiuza ndizi,maji,karanga na kashata leo unakuja na hati ya dharura ya TASAF?

Hiyo ndiyo,Ccm kadri uchaguzi ukikaribia utakuwa balaa!
 
Huyu jamaa ----- wa issues your blind because of his legal knowledge....hajui what are whistle blowers au ponographic practices...lisu leo kachemka
 
Huyu jamaa ----- wa issues your blind because of his legal knowledge....hajui what are whistle blowers au ponographic practices...lisu leo kachemka

Kivipi, nadhini umezidiwa na usingizi. Pata kahawa urudi tena jamvini utushawishi
 
Who are hackers..je hackers should be set free with their practices? Nchi gani duniani inakubali hackers? Were is snowden na mardon brandley and julian assange? Do thisman understand what is child porn? Can you view it online or were? To know the law is not to know IT!
 
Huyu jamaa ----- wa issues your blind because of his legal knowledge....hajui what are whistle blowers au ponographic practices...lisu leo kachemka

Tunaihitaji ufafanuzi na si maneno ya juu juu.
 
Who are hackers..je hackers should be set free with their practices? Nchi gani duniani inakubali hackers? Were is snowden na mardon brandley and julian assange? Do thisman understand what is child porn? Can you view it online or were? To know the law is not to know IT!

Haya peleka kwenye discussion za madarasa ya sheria...si lazima kila mtu awe mwanasheria ila hata kama Lisu anatupeleka chaka let him...kwanza yuko smart kumzidi A.G mara 1000!
 
Aiseee kaazi sana issue ni kuondoa mfumo huu mbovu ulowekwa na CCM kwakuhamasishana kujiandikisha,kupiga kura na kulinda kura
 
wanafiki watasema ndiyooooo mswada upte.bora ifke october tutoe hawa wanafiki
 
Tungekuwa na kina Lisu watano 2! Hi nchi ingekaa pazuri! Kazi nzuri Tundu! wasiharibu hilo tundu ,,tumia kisu
 
Back
Top Bottom