Mkwawa
JF-Expert Member
- Jun 8, 2011
- 1,334
- 1,464
Anatolewa mwizi anateuliwa mwizi.Kwanini wasiendelee kuiba wakati kwasasa sio rahisi waziri kumaliza hata miaka 5? Wote wanajua wakiiba adhabu kubwa na kujiuzulu na kuendelea ama na ubunge ama na kazi zao au biashara ambazo tayari wamevuna mtaji kutoka kodi za watanzania.
Wanaiba kwani wanajua fika hatutawafanya lolote, tutapiga kelele tutanyamaza, watakuja majimboni mwetu na vitita vya fedha, watapata kura, wataingia makanisani na misikitini na vitita vya fedha watasafishwa na maaskofu na masheikh wetu, siku itakuja siku itakwenda.
Adhabu ndio inaogopwa tu, sio kelele za kisiasa wala kelele za barabarani, hata tupige vipi kelele hawaogopi tena imekuwa ni kawaida. na wale wezi wadhoefu kama chenge huwa wala hawasumbuki hata kujieleza anajua ni upepo tu utapita kama Rada, Richmond, Iptl, sasa Escrow, Buzwag, Meremeta, Tangold, ndege ya Raisi, ndege za air Tanzania etc kala zote na sasa ndiye mwandishi wa katiba huku akipewa ruhusu ya kujadili jinsi ya kuhukumu wezi mjengoni, wakati huo huo tukiwa bungeni tunaunga mkono hoja zake-shame shame shame shame!
Tifa linapotea, unless watu watumie haki zao za kimsingi kuwajibisha watawala, na kurudisha utawala unaoogopa wananchi. Sio kitu cha kuombea ila inakuja pale nguvu ya wananchi itaingia mtaani na kuchukua vyote vilivyoibwa, wanasikia kila wanapotajwa na wanawaona kila wanapopita mitaani wakiwa na maisha mazuri ya fedha za wizi, huku wakijiita waheshimiwa.
Siku inakuja Askofu atakaposhushwa madhabahuni kwani hana sifa za kuhubiri neno la Mungu, hafai kuwa mfano kwa jamii ya watu wanaomfafuta mungu, siku inakuja hawa akina Kilaini watakimbizwa makanisani, Siku inakuaj masheikh wanaowakumbatia hawa wezi watatolewa misikini, siku inakuja wachungaji wanaoendesha makanisa kwa fedha za akina Lowassa watafungiwa nje na fedha zao.
Siku inakuja ikulu watajaa watanzania ndani na nje wakidai fedha zao. Siku inakuja watoto wote wa akina chenge, Jk, Werema, Maswai, Ngeleja, Tibaijuka, Lowassa, Muhingo, etc etc na marafiki zao watatamani kurudi kwenye matumbo ya wazazi.
Naomba wezi wa leo wajue historia ipo wazi, pale wananchi walipofika mwisho wa uvumilivu walipeleka hasira zao kwa yeyeyote aliyefaidika na fedha zao na kuwaletea mateso makali maisha yao yote.
Wananchi wanaona majengo ya thamani yanajengwa bila kazi wala biashara, magari ya thamani, maisha ya anasa kwa fedha zao.
Siku inakuja kila mwananchi atarusdisha jasho lake kwa nguvu. hiyo siku haiko mbali kama watawala hawa wa leo hawako tayari kuwahukumu kwa haki wote waliothibitishwa ni wezi.
Inashangaza sana chombo kikubwa bunge, Takukuru, CAG, waseme hawa wameiba mali ya umma, hawa wanaharufu ya rushwa, hawa hawakutimiza wajibu wao kuokoa fedha za walalahoi, halafu leo wanajipitisha huku wakisema eti Raisi wa nchi hana ubavu wa kuwatoa madarakani kwani wao ni wachapakazi?? Hii inaleta maswali ya kutosha kwamba ikulu ndio imehusika asilimia 100.
Chief Mkwawa
Alikufa kuwatetea watanzania. Je nani mwingine anafuatia??!!??