Bila Katiba Mpya na Tume huru ya uchaguzi wapinzani hawatashinda hata jimbo moja 2020

mpimamstaafu

JF-Expert Member
Jul 18, 2018
4,445
4,704
Pamoja na kuwa sio mfuasi wa chama chochote lakini nimekuwa sifurahishwi na namna Uchaguzi unavyoendeshwa katika nchi hii Chini ya Katiba iliyopo na Tume ya Uchaguzi iliyopo.

Naamini Wapinzani wamejionea chaguzi za marudio zilivyofanyika hivi karibuni na kuwafanya Wagombea wa CCM kushinda Chaguzi zote kirahisi kabisa.

Wasimamizi wa Uchaguzi ambao ni Wakurugenzi wamefanya walivyotaka. Mbinu zilizotumika kuwafanya Wagombea wa CCM kushinda ndio hizo hizo zitatumika 2020 tena kwa nguvu zaidi kwani Katiba ni ile ile na Tume ya Uchaguzi ni ile ile.

Kama Vyama vya Upinzani vitashindwa Kudai Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi ni bora visishiriki Uchaguzi huo kwani kitakachofanyika ili ionekane CCM inakubalika hamtaamini Macho na Masikio yenu na Wanachama wafuasi na wapenda mabadiliko mtawakatisha tamaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu wanataka maendeleo sio katiba mpya.
Magufuli hakuahidi katiba mpya.

Unaweza kukumbuka ni bilioni ngapi zilitumika kuandaa mapendekezo ya katiba mpya ?Vipi kama fedha hizo zingesambaza maji vijijini?
 
Tjidanganye kwani waliopo walipita na tume na katiba IPI,shida ni awareness ambapo ccm imechangia sana kujidhoofisha sababu ya matendo maovu iliyowafanyia watu
 
Nadharia ya kukariri watz ni waoga ni wajinga si ya kuwafanya walewe.
 
na wapinzani 2020 watapoteza sana majimbo kwakutoonewa na tume ya uchaguzi, kwanza wameshapoteza mvuto na wameonekana ni wababaishaji tu na matapeli tu.
 
hivi lissu awezi kuongea na mabebelu,yatufadhiri silaa hata mapanga tu tuwatie adabu sisiem myb tutaheshimiana.haiwezekani kila cku wanatuonea tu eboh.
Ni rahisi kusema kuliko kutenda. Ukipewa hata kisu ushike, utakimbia maili mia.
 
#kabla ya 2020
#tunahitaji katiba mpya
#Tunahitaji tume huru ya uchaguzi
#bila hizo conditions tutaingia field
 
Watu wanataka maendeleo sio katiba mpya.
Magufuli hakuahidi katiba mpya.

Unaweza kukumbuka ni bilioni ngapi zilitumika kuandaa mapendekezo ya katiba mpya ?Vipi kama fedha hizo zingesambaza maji vijijini?

Hapo ndio Lisu anaposema haichafui nchi bali serekali. Suala la katiba ni la nchi sio la serikali. Katiba iko juu ya utashi wa rais, yeye rais ana haki ya kukataa katiba mpya kwani sio mtu anayeitii katiba, hivyo anajua katiba mpya haitampa fursa ya kufanya kila atakacho ikiwemo kuwalinda watu wasiojulikana. Katiba mpya inazuiaje maji kupelekwa vijijini?
 
na wapinzani 2020 watapoteza sana majimbo kwakutoonewa na tume ya uchaguzi, kwanza wameshapoteza mvuto na wameonekana ni wababaishaji tu na matapeli tu.

Ni hivi, hiyo 2020 rais atatumia madaraka yake kuitisha tume ya uchaguzi na kuagiza vyombo vya dola kuhujumu wapinzani ili yeye na wagombea wa chama chake watangazwe washindi.
 
Watu wanataka maendeleo sio katiba mpya.
Magufuli hakuahidi katiba mpya.

Unaweza kukumbuka ni bilioni ngapi zilitumika kuandaa mapendekezo ya katiba mpya ?Vipi kama fedha hizo zingesambaza maji vijijini?
Mtu mpuuzi na mjinga kama huyu ana faida gani humu ?!.

Maghufuli si mwamba akaishi milele, katiba mpya muhimu na tume huru pia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu wanataka maendeleo sio katiba mpya.
Magufuli hakuahidi katiba mpya.

Unaweza kukumbuka ni bilioni ngapi zilitumika kuandaa mapendekezo ya katiba mpya ?Vipi kama fedha hizo zingesambaza maji vijijini?
Kama hakuahidi basi zirudi zile 2.4 trillion zitumike kwenye katiba mpya
 
Kama Vyama vya Upinzani vitashindwa Kudai Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi ni bora visishiriki Uchaguzi huo kwani kitakachofanyika ili ionekane CCM inakubalika hamtaamini Macho na Masikio yenu na Wanachama wafuasi na wapenda mabadiliko mtawakatisha tamaa.
Nadhani nia yako ni kuwaongezea muda tena hawa walioko. Katiba mpya sio kitu cha siku 1. Upinzani wasiposhiriki ni kuwapa ushindi mezani hao ccm. Acha waharibiwe uchaguzi wao kwa kuibiwa kura au kutangazwa ndivyo sivyo ila hata huyo atakayeingizwa kinyume na matakwa ya wananchi atajua HAPENDWI.
 
Hapo ndio Lisu anaposema haichafui nchi bali serekali. Suala la katiba ni la nchi sio la serikali. Katiba iko juu ya utashi wa rais, yeye rais ana haki ya kukataa katiba mpya kwani sio mtu anayeitii katiba, hivyo anajua katiba mpya haitampa fursa ya kufanya kila atakacho ikiwemo kuwalinda watu wasiojulikana. Katiba mpya inazuiaje maji kupelekwa vijijini?
Hilo ling'ombe akili zake ziko toboni kama jiwe anajiita jingalao
 
Hapo ndio Lisu anaposema haichafui nchi bali serekali. Suala la katiba ni la nchi sio la serikali. Katiba iko juu ya utashi wa rais, yeye rais ana haki ya kukataa katiba mpya kwani sio mtu anayeitii katiba, hivyo anajua katiba mpya haitampa fursa ya kufanya kila atakacho ikiwemo kuwalinda watu wasiojulikana. Katiba mpya inazuiaje maji kupelekwa vijijini?
Kipi usichokipata leo utakipata kwenye katiba mpya?Hata 77 Iliwekwa katiba mpya je imeleta nini kwa mwananchi wa kawaida?
 
Tjidanganye kwani waliopo walipita na tume na katiba IPI,shida ni awareness ambapo ccm imechangia sana kujidhoofisha sababu ya matendo maovu iliyowafanyia watu
Chini ya Magufuli Majimbo yote yatarudi CCM.. Alisha waagiza wakurugenzi kuwa kama wanatumia usafiri wa serikali, nyumba ya serikali.. Iliyo chini ya CCM.Huyo mkurugenzi atahatarisha kibarua chake.

Ha Trailer mmeliona kwenye chaguzi za marudio, hali halisi ilivo kuwa.

Jifunze kutofautisha CCM iliyo kuwa kipindi cha Kikwete na CCM iliyopo kipndi cha Magufuli.
Kikwete alikuwa fare angalau kwenye chaguzi za ubunge, mshindi halali alikuwa anatangazwa bila kuiba kura..
 
Back
Top Bottom