Bila Katiba Mpya na Tume huru ya uchaguzi wapinzani hawatashinda hata jimbo moja 2020

Pamoja na kuwa sio mfuasi wa chama chochote lakini nimekuwa sifurahishwi na namna Uchaguzi unavyoendeshwa katika nchi hii Chini ya Katiba iliyopo na Tume ya Uchaguzi iliyopo.

Naamini Wapinzani wamejionea chaguzi za marudio zilivyofanyika hivi karibuni na kuwafanya Wagombea wa CCM kushinda Chaguzi zote kirahisi kabisa.

Wasimamizi wa Uchaguzi ambao ni Wakurugenzi wamefanya walivyotaka. Mbinu zilizotumika kuwafanya Wagombea wa CCM kushinda ndio hizo hizo zitatumika 2020 tena kwa nguvu zaidi kwani Katiba ni ile ile na Tume ya Uchaguzi ni ile ile.

Kama Vyama vya Upinzani vitashindwa Kudai Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi ni bora visishiriki Uchaguzi huo kwani kitakachofanyika ili ionekane CCM inakubalika hamtaamini Macho na Masikio yenu na Wanachama wafuasi na wapenda mabadiliko mtawakatisha tamaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Katba iliyopo ingekua haifai lissu asingekua anaiquote kama biblia kila siku na kulalama kizushi haifuatwi. Ukweli wananchi hawajakua tayari kukabidhi madaraka kwa upinzani hivyo wajitahidi kua wapinzani wenye tija kwa taifa kulingo kuombea njaa nchi kama mkakati wa kuindoa ccm madarakani.
 
Mustakabali wa nchi ni maendeleo ya watu haswa wanyonge.Hatujakosa maendeleo kwa sababu ya katiba mbovu bali kwa kushindwa kufanya kazi na kuendekeza ubadhirifu huku tukijilaza kwenye makucha ya wanyonyaji.
Waliotulaza kwenye makucha hayo ya wanyonyaji (mikataba mibovu) ni nani ?!.
Na huo ubadhirifu umefanywa na nani ?! FIKIRI NJE YA BOX

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu wanataka maendeleo sio katiba mpya.
Magufuli hakuahidi katiba mpya.

Unaweza kukumbuka ni bilioni ngapi zilitumika kuandaa mapendekezo ya katiba mpya ?Vipi kama fedha hizo zingesambaza maji vijijini?
Kwani hii nchi yake hadi afanye atakavyo?
 
FB_IMG_1545542555099.jpeg
 
Watu wanataka maendeleo sio katiba mpya.
Magufuli hakuahidi katiba mpya.

Unaweza kukumbuka ni bilioni ngapi zilitumika kuandaa mapendekezo ya katiba mpya ?Vipi kama fedha hizo zingesambaza maji vijijini?

Kada vipi ? Hayo Mabilioni unayoongelea pia yametumika kwenye chaguzi za marudio za wabunge na maidiwani walionunuliwa .

Vipi kama hayo Mabilioni unayoongelea yangetumika kwenye miradi mingine ya maendeleo.
 
Kipi usichokipata leo utakipata kwenye katiba mpya?Hata 77 Iliwekwa katiba mpya je imeleta nini kwa mwananchi wa kawaida?
Katiba ndiyo sheria kuu. Panapotokea mgongano wa sheria na katiba, katiba ina prevail.
Viongozi wetu wanachaguliwa kwa mujibu wa katiba.
Wana pewa madaraka kwa mujibu wa katiba
Wana achia madaraka kwa mujibu wa katiba.
Watu wengine ni raia na wengine ni raia kwa mujibu wa katiba

Mtu asiyeona umuhimu wa katiba ya nchi hasa katiba bora na bado anajiita mzalendo huyo ni mwendawazimu aliye na maslahi na kikundi cha watu wenye nia ya kulinyonya na kuliibia taifa rasilimali zake.

Na watu hao wanapoona upande wasioutaka umeshinda aidha;

1. Hutumia nguvu kubwa na hata wizi kujibakiza madarakani au
2. Kukimbilia kubadilisha katiba kuleta vifungu vinavyowaficha wanapoona dalili ya kushindwa

Yote haya yanafanywa ili katiba isiyofaa isije kuwatenda kama ilivyokuwa ikiwatenda wapinzani wao.

Hawa si wazalendo, mwl alisema wazi katika hotuba zake kuhusu katiba hii.

Pia, ni yeye tu aliyetetea hoja ya upinzani kurudi nchini.
Hakika alikuwa mzalendo wa kweli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu wanataka maendeleo sio katiba mpya.
Magufuli hakuahidi katiba mpya.

Unaweza kukumbuka ni bilioni ngapi zilitumika kuandaa mapendekezo ya katiba mpya ?Vipi kama fedha hizo zingesambaza maji vijijini?

Kwani swala la katiba ni la mtu au ni matakwa ya wananchi?
 
Watu wanataka maendeleo sio katiba mpya.
Magufuli hakuahidi katiba mpya.

Unaweza kukumbuka ni bilioni ngapi zilitumika kuandaa mapendekezo ya katiba mpya ?Vipi kama fedha hizo zingesambaza maji vijijini?
Kutumia mabilioni ya fedha kununua wabunge na madiwani ni sahihi na haikuathiri maendeleo ya nchi ila hela kutumia kuandaa Katiba ya nchi kuna athiri maendeleo ya nchi.
1.ELIMU
2.ELIMU
3.ELIMU.
 
Vp zile million hamsini kila kijiji?
 
sio tuu katiba mpya, hata mtaani wapinzani hawasomeki. hivyo kwenye sanduku zitakuwa za kuokoteza
 
Kutumia mabilioni ya fedha kununua wabunge na madiwani ni sahihi na haikuathiri maendeleo ya nchi ila hela kutumia kuandaa Katiba ya nchi kuna athiri maendeleo ya nchi.
1.ELIMU
2.ELIMU
3.ELIMU.
Wazee wa ulipo tupo bado mnaota elimu, elimu, elimu
 
Watu wanataka maendeleo sio katiba mpya.
Magufuli hakuahidi katiba mpya.

Unaweza kukumbuka ni bilioni ngapi zilitumika kuandaa mapendekezo ya katiba mpya ?Vipi kama fedha hizo zingesambaza maji vijijini?
Bwana mkubwa kawaambia kama zinapatikana pesa basi zitaelekezwa kwenye ujenzi wa stiegler's gorge na reli.

Muafrika ni maskini kwa sababu anaamini kuwa kila kitu kinatatuliwa kwa kutegemea njia za mkato.
 
Mustakabali wa nchi ni maendeleo ya watu haswa wanyonge.Hatujakosa maendeleo kwa sababu ya katiba mbovu bali kwa kushindwa kufanya kazi na kuendekeza ubadhirifu huku tukijilaza kwenye makucha ya wanyonyaji.
Maendeleo gani umeyapata? Miaka 60 ya uhuru bado kuna shule za nyasi ndio maendeleo? unadhani FlyOver ndio maendeleo unazijenga leo Kenya walizijenga miaka ya 90 eti una maendeleo hakuna lolote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Mpima Mstaafu, kwanza asante kwa hoja hii, japo haya usemayo kuna mengine ni kweli na mengine sii kweli.

Tuanze na la kweli ni Uchaguzi wa 2020, CCM itashinda kwa kishindo na wapinzani watapigwa chini jumla, hivyo Tanzania kurudi kuwa nchi ya chama kimoja kwa Bunge la chama kimoja.

Tangu kuanza kwa uchaguzi wa vyama vingi nchini, tumeshudia wapinzani wakiingia Bungeni na madiwani kwa Katiba hii hii na Tume hii hii ya Uchaguzi, hivyo hizi hoja zako za NEC na Katiba weka pembeni.

Sababu za CCM kushinda kwa kishindo ni kazi nzuri ya rais Dr. John Pombe Magufuli ambaye ameufanya CCM ikubalike sana kama nilivyoeleza humu.

Swali la Ukweli Mchungu: Je, 2020 Magufuli ana mpinzani au mshindani, au Ni Magufuli tu?!. - JamiiForums

Kufuatia kazi hii nzuri sana ya rais Magufuli kutuletea maendekeo makubwa Kama Flyover, Ndege, SGR, na sasa anajenga Tanzania ya viwanda na tunakwenda kuwa nchi ya uchumi wa kati, hivyo nikauliza kama bado tunahitaji kufanya uchaguzi mwaka 2020 au tumuache tuu rais Magufuli aendelee na kwenye ubunge na udiwani tuiachie tuu CCM ipite bila kupingwa?.

Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020? - JamiiForums

CCM itashinda kwa kishindo kufuatia kukubalika sana na tunashuhudia jinsi wapinzani wanavyo vikimbia vyama vyao na kujiunga na CCM
Trend Reading: Wanaohamia CCM wasibezwe! Wanaona mbali, 2020 Majimbo yote kurejeshwa. Je tunarejea nchi ya Chama kimoja? - JamiiForums

P
Pascal sikubaliana na wewe kuwa ccm inashinda sababu ya kazi nzuri ya mh.Rais ingekuwa hivyo kusingekuwa na ubabaishaji unaofanywa na Wasimamizi wa chaguzi , Tume na Vyombo vya Dola wote ni mashahidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tuatshiriki chaguzi kwa kila nafasi inayopatikana huku tukipigania tume na katiba mpya.kwa sababu hujui vitapatikana lini.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hilo ndio neno. Mama akiipua chakula akasema; Njooni tule jamani. Wewe ukasema nitakula siku nyingine. Je, wenzio wagome ka wewe?? Kukataa kushiriki uchaguzi ati kwa kuwa unajua kuwa hutafanyiwa haki ni uzuzu wa kiwango cha lami au SGR
 
Naam hili ndilo kusudio la Nduli kwamba uchaguzi FAKE wa 2020 kuwe na wizi wa kutisha kwenye uchaguzi huo utakaosimamiwa na Tume FAKE ya uchaguzi na policcm ili kuhakikisha mjengoni hakuna hata mbunge mmoja wa upinzani.

Pamoja na kuwa sio mfuasi wa chama chochote lakini nimekuwa sifurahishwi na namna Uchaguzi unavyoendeshwa katika nchi hii Chini ya Katiba iliyopo na Tume ya Uchaguzi iliyopo.

Naamini Wapinzani wamejionea chaguzi za marudio zilivyofanyika hivi karibuni na kuwafanya Wagombea wa CCM kushinda Chaguzi zote kirahisi kabisa.

Wasimamizi wa Uchaguzi ambao ni Wakurugenzi wamefanya walivyotaka. Mbinu zilizotumika kuwafanya Wagombea wa CCM kushinda ndio hizo hizo zitatumika 2020 tena kwa nguvu zaidi kwani Katiba ni ile ile na Tume ya Uchaguzi ni ile ile.

Kama Vyama vya Upinzani vitashindwa Kudai Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi ni bora visishiriki Uchaguzi huo kwani kitakachofanyika ili ionekane CCM inakubalika hamtaamini Macho na Masikio yenu na Wanachama wafuasi na wapenda mabadiliko mtawakatisha tamaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu mimi huwa sio mvumilivu? nisaidie pungufu langu nilifanyie kazi!

Hapana, nilijiweka kwenye nafasi yako katika majibishano yenu.

Nikakuona ulikuwa mtu wa subira nyingi ulivyoonyesha uvumilivu katika kujibu maswali ya kipumbavu ya huyo uliyekuwa ukijibishana naye.
 
Kwenye swala la kudai katiba mpya wanasiasa wanachoangalia ni maslahi yao tu msukumo wao ni mazingira ya uchaguzi, madaraka ya raisi (ili ata mimi ninatatizo nalo) na maswala ya muungano.

Ivyo ndio vigezo vyao cha kudai katiba mpya; sasa hivi ni vitu vya kutaka katiba mpya au kutaka amendments?

Katiba ya Tanzania sisi tunaichukulia poa hila ukitoa porojo za wanasiasa ile ni katiba ya kijamaa katika kutoa haki au kupata huduma za serikari mtu akiamua leo hii anaweza ku challenge mfano huduma za muhimbili kuweka madaraja ya huduma kutokana na uwezo wa malipo.

Chini ya katiba ya Tanzania hilo swala aliruhusiwi kwa taasisi ya serikari utakiwi kutoa huduma yenye kigezo/criteria (mfano malipo tofauti) kitakachomfanya mwingine apate huduma hafifu ina maana serikari inatakiw i-subsidize huduma za walala hoi ili twende sawa huo ndio mwongozo wa katiba.

Hii katiba ya sasa ina mambo mengi ambayo siyo mzaha na mtu akiamua anaweza fanya sheria nyingi sana zifutwe kuwa kinyume na katiba.
 
Back
Top Bottom