esther mashiker
JF-Expert Member
- May 29, 2018
- 616
- 555
Kiukweli huu utakuwa uamuzi sahihi sana.,ambao utachangia ongezeko la wageni kwa kiasi kikubwa kwani njia ilikuwa Kati ya changamoto mbaya iloligarimu taifa kwa muda mrefu.View attachment 1040871
MAMLAKA ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) imetenga Sh bilioni 11 kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Loduare hadi Golini kwa kiwango cha lami, yenye urefu wa kilometa 88 katika eneo la kushukia bonde la hifadhi hiyo.
Lengo la kujenga barabara hiyo katika kipindi cha mwaka huu ni kuondoa usumbufu wanaopata madereva wanaoendesha magari ya utalii, sambamba na watalii wanaoingia ndani ya hifadhi hiyo kujionea vivutio vya utalii vilivyopo ndani ya hifadhi ya Ngorongoro.
Mhifadhi Mkuu wa mamlaka hiyo, Dk Fredy Manongi amewaeleza waandishi wa habari sema ujenzi wa barabara hiyo utawezesha kuondoa kero wanazopata watalii na madereva kwani barabara hiyo wakati wa mvua ina changamoto zake na hata nyakati za jua.
Barabara itakayojengwa ni kutoka Loduare hadi Golini kwa kilometa 88 na wanashukuru Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (Unesco) kwa kukubali barabara hiyo kujengwa pamoja na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (Nemc) kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo ndani ya hifadhi.
“Naomba madereva wanaoshuka kwenda kreta kuwa makini wakati wanapotumia barabara hii na hivi sasa tunasubiri mkandarasi atakayeshinda zabuni aanze kujenga barabara hii kwani fedha tayari tunazo,” amesema. Shabani Felician ambaye ni fundi sanifu wa NCAA, amesema mamlaka hiyo kila mwaka hutumia zaidi ya Sh bilioni tatu hadi bilioni tano kwa ajili ya kutengeneza barabara zilizopo ndani ya hifadhi hiyo, hivyo endapo watajenga barabara hizo kwa kiwango cha lami wataokoa mabilioni ya fedha. Alisema baadhi ya barabara zitajengwa kwa kiwango cha zege huku nyingine zitajengwa kwa kiwango cha lami ili kuokoa mazingira pamoja na uhifadhi katika hifadhi hiyo.
Hapo hata mm sijaelewa,wastani wa km 1 ni 700mio to 1b,sasa cjui hapo inakuwajeBillion 11 Zinajenga km. 88???? How?? Au ndo lami zile mvua ikinyesha inakuwa Mashimo.?? Binafsi sijaelewa vizuri.
Sent using Jamii Forums mobile app
Kumbuka hapa hawajasema kipande cha serengeti ambacho bado kitakuwa ni changarawe kama kawa.Ni wazo zuri sana. Wengi wa wasafiri kutoka Mwanza, Musoma, Shinyanga kwenda Arusha tutakuwa tunatumia barabara hii ambayo itapunguza sana masaa mengi kufika Karatu, Mto wa Mbu, Makuyuni na hatimaye Arusha.
wakuu, barabara za kule hazipitishi magar ya mizigo....Hapo hata mm sijaelewa,wastani wa km 1 ni 700mio to 1b,sasa cjui hapo inakuwaje