Robot la Matope
JF-Expert Member
- Apr 10, 2015
- 7,888
- 16,120
Kama leo wakifika wale wamissionari wa biashara ya utumwa kama walee enzi zilee za kina VASCO DAGAMA na akina CARL PETER'S kwamba wanataka watumwa wakwenda kuwafanyisha kazi huko ng'ambo ya mbali hakiyanani naapa watu wangejitolea kwa hiyari kwenda kutumikishwa huko na Mimi nikiwemo.
Kwanini umoja wa mataifa usitoe pendekezo la kwamba biashara ya utumwa iwe ya hiyari anayetaka kuwa mtumwa anajipeleka mwenyewe kwenye soko ili akanunuliwe nakusafilishwa mpaka huko ng'ambo ya mbali, nakuambia huko uraya mpaka wangetukataa.
Kwa nini nasema hivyo kwamba biashara ya utumwa irudi...? Kwa sababu nchi za kiafrika leo zipo huru zote lakini raia wake wanaishi zaidi ya watumwa wa kipindi kile cha mkoloni mweupe mzungu akisaidiwa na mwafrika mweusi, Leo tupo huru lakini maisha tunayoishi nimaigizo viongozi wa kiafrika karibia nusu au robo tatu hawataki kusikia mawazo chanya kutoka kokote hasa kwa vyama vya upinzani.
Majeshi yetu yamekuwa fimbo yakutuchapia hata wakisikia wanafunzi wa primary au secondary wamegoma kula watafurumushwa na mabomu ya machozi na kipigo juu bilq kuzingatia haki za binadamu.
Kama utumwa ukirudi leo Mimi binafsi naweza kuishauri familia yangu au ukoo wangu tukawe watumwa nchi za mbali maana tunashuhudia utengano na mipasuko isiyokuwa ya lazima huku wanao hoji na kuleta mawazo mbadala juu ya watawala wanaitwa siyo wazalrnfo, tunahitaji uzalendo upi ambao tunautaka..? Tunahitaji kuwa watu wa aina gani ili tupige hatua kutoka tulipo kwenda sehemu nyingine..?
Kwanini leo Afrika nzima tupo huru lakini tunashuhudia mambo mabaya yakinyanyasaji na yasiyovumilika mbele za macho ya mwanadamu mpaka ajiite yupo huru na anafurahia matunda ya nchi yake? Tumeshuhudia karibia nchi zote za kiafrika hasa zenye mifumo ya vyama vingi wapinzani wakishurutishwa na kunyimwa Uhuru wa kufanya chochote kile kisa ni mwanachama wa chama cha upinzani.
Naona ni bora utumwa ule nilio usoma kwenye vitabu shuleni enzi zile kuliko Uhuru huu wa mwana wa Afrika anayeteswa na waafrika wenzake kisa utofauti wa itikadi.
Nani alituloga waafrika hatupendani sisi kwa sisi kwa sababu ambazo hazina mashiko watawala wanatumia dora hata sehemu isiyofaa, watawala anawabagua waafrika na kujenga matabaka ya ukanda, ukabira na uchama nani aliyetuloga sisi waafrika?
Ni bora utumwa wa mtu mweupwe urudi kuliko maisha anayoishi mwafrika ndani ya nchi take iliyohuru na yenye katiba Mama ambayo ndiyo muongozo wa mambo yote, inafikia mda unajiuliza hivi sisi wenye ngozi nyeusi Nani katuloga kiasi hiki ? Kwanini hatuhitaji kuwa wamoja natukajenga umoja ulio tukuka na mshikamano dhabiti?
Moyo wangu huwa unalia kwa ndani ninapoona Uhuru wa mtu unapokwa, Uhuru wa mtu unabadilishwa inakuwa jinai, Uhuru wa mtu unabadilishwa yanakuwa majuto, Uhuru wa mtu unabadilishwa unakuwa yoga , angalia Besige wa Uganda na watu wengine kadha wa kadha ndani ya nchi zao hawawezi hata kutembea kwa mguu kwenda popote wataambiwa wamehatarisha amani...!!
Moyo wangu bado unazidi kutoamini kwamba Uhuru wa mwafrika kumuondoa mkoloni Muzungu ndiyo huu tuliokuwa tunauhitaji na kama mwafrika yulee aliyepigania Uhuru wa nchi hizi za afrika kama angejua baada ya miaka kadhaa ya Uhuru mambo yatakuwa hivi naapa hakuna mtu angethubutu kuimba tunataka Uhuru tujitawale wenyewe.
Nina mengi yakuandika na yanasikitisha lakini kwa leo naona karamu yangu ikomee hapa na niweze kushauri tu kwamba kwa sisi Watanzania na viongozi wetu wote wawe Wa dini wa serikali na vyama vote nawaomba tuuimbe mushikamano ulioasisiwa na wazee wetu kipindi wakisaka Uhuru wa Taifa hili ili tuwe mfano wakuigwa na mataifa mengine, viongozi Wa serikali nawaomba muache kutumia vyombo vya dola kama fimbo yakumuchapia asiye na mamulaka au nafasi yeyote serikalini.
Tukizingatia haya hata ndoto yangu yakuomba ukoloni Wa mweupe uje itafutika ndani yakichwa changu maana nitakuwa huru kama madhumuni yakusaka Uhuru yalivyokusudiwa, mwisho kabisa kila mmoja wetu nilazima kutii sheria za nchi awe RAIA, Mkuu Wa mkoa, Wilaya , Raisi na kila mmoja aliyepo hapa kwa mjibu Wa sheria.
Asnteni niwatakie tafakuri njema.
By Michael S. Mbiti Jr.