Biharamulo inatafunwa na kikundi cha watu wachache

Biharamulo inatafunwa na kikundi cha watu wachache

SANZIKI

Member
Joined
Aug 17, 2018
Posts
7
Reaction score
16
Habari ya Muda huu wadau wa Maendeleo ya Biharamulo.

Nimekaa kimya kwa Muda Mrefu juu ya Kikundi kinajiita Albatross kilichojitengeneza kwaajili ya jimbo la Biharamulo.

Leo nitazungumza ilivokua kwa Mwanachama Mmoja aliyejitoa.

"Baada ya kupoteza nafasi ua Ubunge Mwaka 1990 Mh. JPM ilibidi Mwaka 1994 Ajiunge na Albatross.

Wakati anajiunga Mwaka 1994 Hakujua Nini? Hasa Malengo ya Albatross lakini kwasababu aliaminishwa na Ndugu Stanslaus Kasusula kuwa ili Mbunge wa Biharamulo lazima uwe mwanachama wa Albatross.

Mwaka 1995 alifanikiwa kuingia kwa Mara ya Kwanza Bungeni Kupitia CCM akiwawakilisha wananchi wa Jimbo la Biharamulo Mashariki/Chato.

Hali ilikua Tofauti sana Baada ya kufanikiwa kuingia Bungeni. Hakutakia kabisa kutimiza matakwa ya Albatross kitu ambocho kilianza kumpa upinzani ndani ya Chama. Upinzani huo uliibuka Baada ya Albatross kutafta Mtu na kumdhamini pesa ili akaanze kujiweka karibu na Wananchi wa Jimbo la Biharamulo Mashariki.

Mh. JPM aligundua mbinu hizo mapema akaanza kuwa mkali kwa kila aliyeanza kunyemelea Jimbo lake. Mungu ni mwema alifanikiwa kudhibiti hilo .

Hakuishia hapa Bali alianza harakati za kujitenga na kuhakikisha Chato inabaki kama Chato na si sehemu ya Biharamulo.

Albatross walichukia sana hata baada ya Ndg Kasazi kuingia Bungeni walitaka kumtumia ili kumdhoofisha Mh. JPM ndio maana kuna wakati walirushiana Maneno sana Bungeni .

Mh JPM alikataa Kuchangia kabisa Million 20 za Kila Mwaka kama Mwanachama na Matokeo yake albatross walimtimua kabisa na kumfuta Wanachama. Hii ilimchefua sana Mh. JPM na kuwachukia sana watu hawa (Sina Uhakika kama aliwachukia hadi wana Biharamulo. )

Albertross wanaendelea na Mchezo huo mpaka leo na hawa si wazuri.

Mwaka 2020 Albatross wameweka watu wao pia kwenye mchakato wa kulitafta Jimbo.

Wapo Wagombea 4 ni Wanachama wa Albatross.

Hii ndio Biharamulo halisi inayotafunwa na kikundi cha watu wachache waliojikalia Dar es salaam na kutaka kula Biharamulo"
 
Walikuwa wanamdhamini Dr sende?

Huyo kasaizi alizingua hadi mzee pombe akampambania Mwl kashemezi kuwa mbunge !!!


Hiyo ndiyo biharamulo ya wasubi wasiosoma lakini wabaguz hatari.

Nipo rukaragata.
 
Walikuwa wanamdhamini Dr sende?

Huyo kasaizi alizingua hadi mzee pombe akampambania Mwl kashemezi kuwa mbunge !!!


Hiyo ndiyo biharamulo ya wasubi wasiosoma lakini wabaguz hatari.

Nipo rukaragata.
Uchaguzi wa Mwaka huu kuna
1- James Kasusula
2- King Ezrah

Na wengine wawili ambao natafta majina yao halisi.........

Makubaliano ya Albatross ni kutoa 20 kila mwaka
 
Unakimbilia wapi mkuu,,,hebu andika fresh boss.

Mods rekebisheni kichwa cha habari.
 
Kwani unakimbizwa? Papara za nini chief? Tulia kisha ulete mburi (figisu figisu)mezani.
 
Biharamulo inatafunwa kivipi? au kujiunga na kikundi hicho ndio kutafunwa kwenyewe? .
 
Vip dr sebuyoya si ndio ameongoza kura za maoni iweje hao akina james KASUSURA
 
Biharamulo inatafunwa kivipi? au kujiunga na kikundi hicho ndio kutafunwa kwenyewe? .
Kikundi hiki kilianzishwa na watu wachache.


Watu hawa wana miliki Biashara na wao wapo tayari kukusaidia pesa kwaajili ya Uchaguzi kwa Makubaliano maalumu
 
Vip dr sebuyoya si ndio ameongoza kura za maoni iweje hao akina james KASUSURA
Ni Sahihi kabisa Dr. SSEBUYOYA kaongoza Kura za Maoni.


Kikundi hiki kiko Strategically sana hakitoi pesa kama maharage.... mara nyingi hukupa nguvu zaidi ya kipesa unapopita kura za maoni.

Unapokuwa umepita Kura za Maoni kikundi hiki hukupatia Pesa kati ya Tsh. 20-40 Millions ili ufanye kampeni.

Ukishinda lazima Utoe 20 Million kila Mwaka..... ukishindwa yapo mawili either uweke rehani Thamani zako ama ukasimamie Miradi ya Miaka 3 bila malipo lakini ukipewa pesa kwaajili ya kujikimu
 
Kikundi hiki kilianzishwa na watu wachache.


Watu hawa wana miliki Biashara na wao wapo tayari kukusaidia pesa kwaajili ya Uchaguzi kwa Makubaliano maalumu
Kama ni hivyo basi ambaye atakuwa alipona na kikundi hicho atakuwa ni marehemu Kabuye peke yake, maana yake huyu mzee alikuwa anaendesha kampeni zake kwa hali ya umasikini mkubwa sana, hata kagari kenyewe alikokuja nako baada ya kumaliza ubunge wake kalikuwa kanaonyesha hali yake halisi ya umasikini.
 
Back
Top Bottom