Big results now! Malaysia na Tanzania

Big results now! Malaysia na Tanzania

Kaliro X

JF-Expert Member
Joined
Apr 18, 2013
Posts
749
Reaction score
440
Kwanza kabisa kila mtanzania kwa sasa anajua na kulisikia sana neno hili la "Big Results Now" Matokeo makubwa sasa. Mfumo huu serikali imeamua kuuchukua kutoka nchi ya Malaysia ambako ilionekana kuwanufaisha na kukuza uchumi wao kwa haraka. Hebu tuziangalie hizi nchi mbili sasa.

Wakati Tanganyika inapata uhuru mwaka 1961, nchi ya Malaya ilikuwa tayari ina uhuru mwaka 1957. Malaya ilijiunga na Singapore, Sabah na Sarawak mwaka 1963 na kuunda Malaysia. Tanganyika yenyewe ilijiunga Zanzibar 1964 kuunda Tanzania. Hata hivyo Singapore ilifukuzwa katika muungano huo mwaka 1965. Nchi zote hizi mbili zilitawaliwa na Mwingereza.

Wakati Tanzania inaundwa mwaka 1964, pato la wastani la mtu mmoja lilikuwa ni USdolar 63, wakati Malaysia ilikuwa USdolar 113. Kimsingi nchi hizi zilikuwa sawa kimaendeleo ingawa Tanzania ni kubwa mara tatu ya Malaysia.

Hivi sasa Malaysia kipato cha wastani cha mwananchi ni USdolar10,000 na Tanzania ni USdolar 600. Kwa Tanzania pato limeongezeka mara kumi na Malaysia limeongezeka mara elfu moja.
Nini tofauti ya mikakati ya nchi hizi mbili?

Leo hebu tuangalie eneo moja tu la Kilimo, na namna Kilimo kilivyoweza kuivusha nchi ya Malaysia na Kilimo hicho hicho bado hakijaweza kuivusha Tanzania.
Malaysia iliunda Shirika la Umma, Federal Land Development Authority, (FELDA) likiwa na wajibu mmoja mkubwa wa kuhakikisha wananchi masikini wanapata ardhi, wanlima kisasa na kuongeza uzalishaji, kisha kufuta umasikini.

Kila mwananchi masikini aligawiwa hekta 4.1, ardhi ikasafishwa na kuwekewa miundombinu ya muhimu, ikapandwa michikichi na mwananchi akapata huduma za ugani ili kukuza michikichi hiyo. Shughuli zote hizi zilifanywa kwa gharama za Serikali na wananchi wote waliowezeshwa wakapewa kama mkopo ambao walikuwa wanaulipa kidogo kidogo kila wanapovuna na kuuza Mawese kwa Shirika hili la Serikali. Hivi sasa Shirika hili ni kubwa sana, lina thamani USdolar bilioni 3.5 na kupitia ushirika wao wananchi hawa waliopewa ardhi ya kulima michikichi sasa wanamiliki 20% ya Shirika hili.

Malaysia iliweza kuondoa umasikini kutoka 57% ya wananchi wanaoishi kwenye dimbwi la umasikini mwaka 1965 mpaka chini ya 3% mwaka 2012.

FELDA sasa ni Shirika la Kimataifa maana linaanza kuwekeza duniani kote. FELDA ilipouza hisa zake kwenye masoko ya mitaji, IPO yake ilikuwa ni ya tatu kwa ukubwa baada ya Facebook na Japanese Airlines. Shirika la Umma linalomilikiwa na Serikali, Wakulima na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (EPF) na linaloendeshwa kwa misingkini ya utawala wa Makampuni limeweza kufuta umasikini kwa zao moja tu la Michikichi. Malaysia leo inaongoza kwa kuuza Mawese duniani. Michikichi hiyo ilitoka Tanzania na kupelekwa Malaya na waingereza miaka ya hamsini.

Tanzania nasi tulikuwa na Shirika la Umma kwa ajili ya Kilimo. Tuchukulie Shirika la NARCO kama FELDA, NARCO walichukua ardhi kubwa maeneo kadhaa nchini. Tofauti na FELDA wao walilima wenyewe mashamba haya na kuweka miundombinu ya Kilimo.

Tuchukulie mfano wa mashamba ya mpunga kule Kapunga, wilaya ya Mbalali Mkoa wa Mbeya. Mwaka 1985 NARCO walikwenda kijijini Kapunga kuwaomba wananchi wawape ardhi ya kulima mpunga. Wananchi wakawapa hekta 3000 hivi. NARCO wakapata msaada kutoka katika Serikali ya Japani na uwekezaji mkubwa ukafanyika ikiwemo kuweka kinu cha kukoboa mpunga cha kisasa kabisa.

Hata hivyo NARCO ilijiendesha kwa hasara na ilipofika katikati ya miaka ya 90 ikaamriwa kubinafsishwa. NARCO ikauza mashamba yale kwa mpango wa ubinafsishwaji kwa Makampuni binafsi. Katika uuzaji huo NARCO waliuza hekta 3500 badala ya 3000 walizopewa na wananchi, kwa maana hiyo kijiji cha Kapunga nacho kiliuzwa.

Mifano hii miwili inaonyesha tofuti kubwa za kifikra kimaendeleo kati ya nchi zetu hizi mbili. Moja iliwezesha wananchi kumiliki ardhi na imefanikiwa. Na nyingine iliamua kufanya kupitia Shirika la Umma na baada ya kushindwa, badala ya kurejesha ardhi kwa wananchi na kuwawezesha kulima, ardhi ile ikauzwa kwa kampuni ya mtu mmoja. Mfano wa Kapunga uko pia huko wilayani Hanang kwenye mashamba ya Ngano ya Basotu n.k.

Hata kwenye mpango wa SACGOTT bado fikra ni za wakulima wakubwa wenye mashamba makubwa badala ya kuwawezesha wananchi kumiliki ardhi na kulima kwa mfumo ambao huduma zitatolewa kwa pamoja. Ujamaa wa Malaysia ulikuwa ni wa kumilikisha wananchi wao ardhi na kuwawezesha kuzalisha.

UJamaa wetu ulikuwa ni wa kumiliki kwa pamoja na hivyo kukosa uwajibikaji. Badala ya kuboresha na kuwawezesha wakulima wadogo wadogo, wakubwa wanaona ni bora kwwenda kwa wakulima wakubwa na kugawa ardhi hovyo bila mpango.

Kwa mantiki hiyo kweli "Big Results Now" itafanikiwa? Kosa ninaloliona mimi hapa, Serikali imechukua mfumo huu kutoka Malaysia ambao wao wliweka mpango dhabiti na kuuandikikia kitabu wakikiita "Big Fast Results" huku wakiweka miundombinu ya kutosha kuuwezesha mpango kutimia. Wakati sisi tunaoiga mfumo huu tunataka" matokeo makubwa sasa" lakini hatuna mipango ya kupata hayo matokeo sasa.

Je, hatuwezi kujifunza kwa wenzetu kweli? Lini tutaacha Umazwazwa?
 
Sio kila jambo ni kosa la serikali, na sisi pia wananchi ni mizigo. Tunaendekeza sana udokozi na kupenda vya mteremko.Wamalay wana nia ya kweli kutoka kwenye umasikini na ndio maana walipo pata nafasi wakaitumia. Sie tutaiba mpaka spea za trecta. Basutu watu wameiba mpaka bati, trecta zimebaki fremu.
 
Sio kila jambo ni kosa la serikali, na sisi pia wananchi ni mizigo. Tunaendekeza sana udokozi na kupenda vya mteremko.Wamalay wana nia ya kweli kutoka kwenye umasikini na ndio maana walipo pata nafasi wakaitumia. Sie tutaiba mpaka spea za trecta. Basutu watu wameiba mpaka bati, trecta zimebaki fremu.
Kama serikali ni legelege inafuga wezi unategemea nini?
 
Muongozaji wa BRN hajui nini cha kufanya yuko bize na akina Shilole,JB,Dimond nk muulize stimulus package iliishia mifukoni kwa nani
 
Nimeipenda hii thread. Nagundua tatizo ni siasa kuwekwa mbele hata ktk maswala ya kitaalam. BRN hapa imeletwa kisiasa na imeandaliwa kutekelezwa na wanasiasa. Hii haiwezekani kbs.. Mambo kama haya waachiwe wataalam na yafanyike kwa kuzingatia muda maalum. Tuwe na priorities chache zinazotekelezeka.
 
Asee thread nzuri sana! Kuna ndugu mmoja anauliza kwanini wachangiaji wachache! Watnzn wengi ni washabiki wa udaku na mambo ya kipuuzi puuzi tu....
 
Mpango kama huu wa BRN..wanapewa wanasiasa kuusimamia na kupanga namna ya kuutekeleza wakati tuna taasisi za sayansi na teknlojia zilizo na wataalamu wanaoweza kutengeneza plan kuringana na uhitaji wetu na rasilimali zetu..

Mabadiliko makubwa yanahitajika sasa...
 
Unaweza kuona jinsi RUBADA inavyoliangalia tu bonde la rufiji na hakuna kinachofanyika cha maana.

Hilo la maadili limekuwatatizo kubwa sana. Leo hii hata mwanafunzi wa chuo badala ya kutafuta field practice mahali pa kujifunza zaidi yeye anatafuta wapi atalipwa hata kama hatajifunza kwa vitendo.
Akishahitimu na kuajiriwa interest yake yote ni kuangalia namna gani ataiba hela.
 
Kutatua matatizo ya ajira na nchi kuendelea ni Kilimo kwanza. Kilimo kina zaa Viwanda. Viwanda vinatoa ajira na kipato kupitia kilimo na ajira zinaongezeka.

Na kilimo ninacho maanisha hapa ni kilimo cha umwagiliaji, miundo mbinu safi, na wakulima walio wezeshwa(elimu kutipitia bwana shamba, mbolea, matrekta, madawa, na mitaji). Viwanda vyote vya kilimo vifufuliwe upya.

Hata Great Britain, kabla ya Industrialization walianzia Green Revolution (Agriculture).

Sijawahi kuona usanii mzr kama wa bendi inayo itwa CCM!
 
Tulileta BRN si kimikakati ya kumkomboa Mtanzania. Bali tu kama mwenendo wa kisiasa kuwapuuzisha tu watu Fulani kwa kuwapa matumaini mfu.
Ila linaloniuma zaidi ni kwamba pamoja na yote hayo. Bado watanzania tu wajinga mno. Hatujui wapi tunapokosea. Na hata hatuonyeshi jitihada zozote kujikomboa.
Jamani CCM...CCM...CCM!
 
BRN Iliendeshwa kiasasa zaidi badala ya kisomi. Matokeo yake wakashusha madaraja ya watoto kufaulu na wakafaulu sana. Hiyo ni BIG RESULT but negative. Inaendelea kuongeza malofa wa wa Mkapa. Quality and quantity must go together sio mambo ya kiswahili swahili na mipasho isiyo na maana.
 
Thread nzuri kama hizi huwa hazipati wachangiaji.Hapo unaweza ukajua ni kwa nini nchi yetu haiendelei.
wwe umechangia nni hapo sasa???
:focus:
Ninachokiona hapa Tanzaniaaa tunaiga tu mambo bila kuwa na mwelekeo thabiti
Hiyo BRN imekuja kwa mbwembwe bia kuainisha vyanzo vya pesa kwaajili ya utekelezaji ni nni???
Ukienda kwenye maofisi ya serikali utaona BRN imeishia kubandika vibandiko tu kwenye milango na kwenye mbao za matangazo,

Tukiacha usanii tutafika mbali
 
Sio kila jambo ni kosa la serikali, na sisi pia wananchi ni mizigo. Tunaendekeza sana udokozi na kupenda vya mteremko.Wamalay wana nia ya kweli kutoka kwenye umasikini na ndio maana walipo pata nafasi wakaitumia. Sie tutaiba mpaka spea za trecta. Basutu watu wameiba mpaka bati, trecta zimebaki fremu.

Kama serikali haisimamii vizuri watu wake hayo maendeleo yatatoka wapi?
Tatizo kubwa la Tanzania ni serikali iliyojaa wezi na mafisadi.
Watu hawana shida kama kutakuwa na uwajibikaji katika levels zote.
 
Tulileta BRN si kimikakati ya kumkomboa Mtanzania. Bali tu kama mwenendo wa kisiasa kuwapuuzisha tu watu Fulani kwa kuwapa matumaini mfu.
Ila linaloniuma zaidi ni kwamba pamoja na yote hayo. Bado watanzania tu wajinga mno. Hatujui wapi tunapokosea. Na hata hatuonyeshi jitihada zozote kujikomboa.
Jamani CCM...CCM...CCM!

Na wanaowapa kura CCM ni hao walioitwa 'wapumbavu' na 'malofa'. Watu wenye kujiweza hawawezi kuwapa kura CCM.
 
kwa uzoefu wangu kwa watanzania,hata wakipewa ardhi hawatalima,hata wakipewa madawa na mbolea hawatamwagia mazao.

Ni hivi maeneo mengi sasa kwa ngazi ya kijiji wanamatrekta ya kilimo.madawa ya kuuwa wadudu sasa ni bei nafuu,na mbolea nayo ni bei nafuu. ardhi ipo kubwa tu nchi hii na inapatikana still watu hawataki kulima.ukiwalimia kwa trekta bure kufanya palizi wenyewe hawataki. tatizo la watanzania ni uvivu na ujinga umewajaa
 
Kwa ccm hii! BRN ni mtaji wa kuwamkapisha wstanzania. Kwanza wameshusha viwango vya ufaulu ili waziri anapotangaza matokeo aseme ufaulu umepanda kwa % blah blah! Kwenye kilimo ndo hoi kabisa, ni kuongeza takwmu tu hapo wstanzania unakua umewakamata.
 
Serikali duniani kote lazima ionyeshe njia na kusimamia kwa dhati mipango yote yenye lengo la kuleta maendeleo kwa watu wake.
Tabia zote tulizonazo watanzania zinatokana na mwenendo wa aina ya uongozi tulio nao.
Usitegemee popote duniani wananchi kujiletea maendeleo bila kuwa na UONGOZI WENYE NIA YA DHATI NA MAONO YA KWELI KATIKA KUSIMAMIA JUHUDI HIZO.

Sio kila jambo ni kosa la serikali, na sisi pia wananchi ni mizigo. Tunaendekeza sana udokozi na kupenda vya mteremko.Wamalay wana nia ya kweli kutoka kwenye umasikini na ndio maana walipo pata nafasi wakaitumia. Sie tutaiba mpaka spea za trecta. Basutu watu wameiba mpaka bati, trecta zimebaki fremu.
 
Kwa ufupi hawajui wanachofanya.tazama kwenye elimu walivyojikita kwenye ubadilishaji wa alama ili wanafunzi waonekane wamefaulu.ndio big result now.Shame!!!
 
Back
Top Bottom