Bidhaa za Ramadhan bei juu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bidhaa za Ramadhan bei juu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by abdulahsaf, Jul 13, 2012.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Jul 13, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  [h=3][​IMG][/h]


  Na Kijakazi Abdalla, ZJMMC  WAKATI mwezi wa mfungo mtukufu wa Ramadhani ukikaribia bei za bidhaa mbalimbali zinaonekana kupanda zaidi ikilinganishwa na miezi ya nyuma.


  Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa nyakati tofauti, baadhi ya wafanyabiashara wa soko la Mwanakwerekwe la mjini hapa, wamesema kuwa bei za bidhaa muhimu kwa mwezi huu zimepanda bei.


  Walisema kuwa bei ambazo ni muhimu kwa mwezi mtukufu hasa nazi zinapatikana kwa bei ya shilingi 550 hadi 600 kwa jumla kwa nazi moja, mkungu wa ndizi ni shilingi 20,000 ambapo kwa chana moja ni shilingi 2,000 hadi 1,500 ndizi mkono wa tembo dole moja inauzwa kwa bei ya shilingi 1,500 hadi 1,600 muhogo polo shilingi 12,000 hadi 14,000.


  Kwa upande wa bidhaa za nafaka kama maharage kilo moja ni shilingi 1,600, njugu mawe kilo moja ni shilingi 1,900 kunde kilomoja shilingi 1,400 ambapo mtama kwa kilo unauzwa shilingi 900.


  Aidha wafanyabiashara hao walisema kwa upande wa bidhaa za matunda kama mananasi linauzwa kwa bei ya shilingi 2,500 hadi 4,000, ambapo embe boribo kwa tenga moja zinauzwa shilingi 18,000 hadi 20,000.


  Tikiti moja katika soko hilo linauzwa kati ya shilingi 1,500 na 2,000 hata hivyo inategemea kwa ukubwa wa tunda lenyewe, matunda ya pesheni kwa kilo linauzwa shilingi 2,000 hadi 1,500.


  Akizungumza na Gazeti hili, Kaimu Meneja mkuu wa soko hilo, Said Omar Talib, alikiri kuwepo na upandaji wa bidhaa hizo, ambapo alisema inatokana na baadhi ya bidhaa hizo kutoka Tanzania Bara.


  Aidha aliwataka wafanyabiashara kutowakomoa wananchi kwa kuwauzia bidhaa hizo kwa bei ya juu, jambo ambalo litawashinda kumudu bei hizo hasa katika mwezi huo wa Ramadhan ambapo mahitaji yanaongezeka.


  “Tunawaomba wakulima wasivune mazao machanga kwa ajili ya kufanya biashara, kwani kufanya hivyo ni hasara kwa pande zote mbili kati ya muuzaji na mnunuzi,” alisema.
  Imewekwa na MAPARA at 6:18 PM
   
 2. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #2
  Jul 13, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,749
  Likes Received: 6,021
  Trophy Points: 280
  Shida huwa mnajisahau na kudhani hii nchi ni ya kidini. Mbona kila kitu bei juu hadi nyasi za kulishia wanyama? Mkuu ni kila kitu kime-shoot sio bidhaa za Ramadhani tu. Tusitake kufanya ugumu wa maisha uliopo kwa kila mtanzania hadi wanyama kuwa suala la kidini.
   
 3. m

  mashambani kwao JF-Expert Member

  #3
  Jul 14, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  liwalo na liwe
   
Loading...