Bibi wa Miaka 102 Aanza Shule ya Msingi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bibi wa Miaka 102 Aanza Shule ya Msingi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Apr 13, 2010.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Apr 13, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Bibi mmoja nchini China amekuwa mwanafunzi mwenye umri mkubwa kuliko wote duniani baada ya kuamua kuanza darasa la kwanza akiwa na umri wa miaka 102.
  Ma Xiuxian, kutoka Jinan, katika jimbo la Shandong alifanikiwa kutimiza ndoto yake ya kuanza elimu ya msingi akiwa na umri wa miaka 102.

  Ma alianza kufanya kazi kwenye kiwanda cha nguo tangia alipokuwa na umri wa miaka 13 na kwa miaka yote aliendelea kufanya kazi huku akiwa na ndoto ya kuwa na angalau elimu ya shule ya msingi.

  Ma aliolewa akiwa na umri wa miaka 18 na alifanikiwa kupata watoto tisa, saba kati yao ni wahitimu wa shahada ya kwanza ya chuo kikuu.

  Ma alipewa nafasi ya kusoma kwenye shule hiyo baada ya kulieleza gazeti moja la mjini mwake kuwa alikuwa na ndoto ya muda mrefu sana ya kwenda shule.

  "Nina furaha sana nimeweza kutimiza ndoto yangu ya kwenda shule ingawa katika umri huu", alisema Ma.

  Ma alienda shuleni akisindikizwa na mwanae wa mwisho wa kiume Yi Fengxin mwenye umri wa miaka 58.

  Katika somo lake la kwanza katika shule yake ya Weishan Road Primary School, Ma alisema "Nawashukuru walimu wangu, nawashukuru wanafunzi wenzangu nawaahidi nitajisomea kwa nguvu zote na nikimaliza shule nitasaidia kulijenga taifa".

  Ma anatumia kifaa cha kumsaidia kusikia vyema ili aweze kuwasikia walimuwa wake vizuri na huwatumia wanafunzi wenzake kumsaidia kusoma vitabu vya masomo yake.

  Ma ameingia kwenye rekodi za dunia kwa kuwa mwanafunzi mzee kuliko wanafunzi wote duniani.
   
 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #2
  Apr 13, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,263
  Likes Received: 21,990
  Trophy Points: 280
  Bibi kauona umuhimu wa elimu.
  Leo nawashangaa ambao hawataki kusikia kitu kuhusu elimu.
  Biblia inasema, tuishike sana elimu.
  Kukosa elimu ukiwa unawezxa kuipata ni dhambi.
  Mshahara wa dhambi ni mauti.
   
Loading...