Biashara za machinga zinaikosesha serikali mapato

shikulaushinye

JF-Expert Member
Aug 29, 2014
828
456
Mheshimiwa Rais wangu JPM, kwanza nikupe hongera kwa kazi nzuri unayoifanya na team yako ya mawaziri, me km mfanyabiashara kwa muda mrefu tumekuwa tukisuguana kuhusu matumizi ya mashine za EFD.

Wafanya biashara waliokwenye maeneo maalumu hawapaswi kuwa tu sehemu ya walipo kodi, lakini pia wafanya biashara ndogo ndogo maarufu km wamachinga nao wanaitia serikali hasara kwaani hawalipi kodo wala ushuru wowote zaidi ya kuzarisha takataka. Ili wafanyabiashara wafaidi kodi zao serikali haina budi kuliangalia hili kwaani nalo ni jibu.

Kama wanataka kufanya bishara watafutiwe maeneo maalum ili na wao walipe kodi lakini siyo kutandika biashara zao chini. mfano ukienda kando ya barabara ya mwenge, ubungo, kariakoo na nk utawakuta kwa wingi.

Serikalia inakosa mapato kwenye hii biashara holela.
 
Hao watarudiwa awamu nyingine mkuu, kwa sasa tuwaache kwanza wapambane na upotevu wa makontena. Huko ndio kodi kodi nyingi inapotea!
 
Hao watarudiwa awamu nyingine mkuu, kwa sasa tuwaache kwanza wapambane na upotevu wa makontena. Huko ndio kodi kodi nyingi inapotea!

Nakubaliana na wewe, huko ndiyo kuna pesa nyingi zinapotea, lkn wafanyabaishara nao wanalalamika kwaani nje ya maduka kuna machinga wanauza the same bidhaa kwa bei ya chini kuliko ya dukani huku hawalipi kodi. hizo machine za EFD zinakubalika? tunataka nchi ikusanye kodi kila mtu anayepaswa kulipa na alipe nchi insinge mbele.
 
machinga nimajipu mengine, nguo wanauza chini sana kiasi wamba wakiweka mlangoni kwako wewe mwenye EFD hauuzi kitu, kwanza wanawavuta wateja kwa kuwaimbia nguo ni mia tatu tu.
 
Nakubaliana na wewe, huko ndiyo kuna pesa nyingi zinapotea, lkn wafanyabaishara nao wanalalamika kwaani nje ya maduka kuna machinga wanauza the same bidhaa kwa bei ya chini kuliko ya dukani huku hawalipi kodi. hizo machine za EFD zinakubalika? tunataka nchi ikusanye kodi kila mtu anayepaswa kulipa na alipe nchi insinge mbele.

Nafikiri wanaenda hatua kwa hatua, na ingefaa wakapanga na kuwa na mikakati bora ya namna ya kukabiliana na ukwepa kodi katika maeneo yote. Wakati mwingine maamuzi ya kukurupuka huwa hayaleti matokeo chanya ya kudumu. Tatizo lingine usije ukakuta hii vita inakua ngumu kwa sababu wanaotakiwa kuzuia ukwepaji wa kulipa kodi ndio hao hao wanaokwepa mkuu.
 
Back
Top Bottom