Biashara yakukodisha gari ALPHAD

malembeka18

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2018
Posts
3,789
Reaction score
4,480
Wakuu ushauri wenu tafadhali nataka kununua gari aina ya ALPHAD kwa ajili ya biashara yakuwakodishia watu wenye safar zakifamilia kama kwenda kwenye harusi,misiba,shughuli binafsi,
Wazoefu hii biashara ikoje
 
Wazo zuri, lakini unamfanyia nani? Maana matajiri wana magari yao, na walala hoi wataona bei yako ni kubwa, inabidi uwe na connection ya maana sana.
Hapa mkoani nilipo Nina baba yangu mkubwa ana ALPHAD Sasa gari yake huwa wanataka sana watu kiukodi ila yeye hataki,Namwanae huwa Niko nae gari unakuta anapigiwa sm nawatu wanahitaji gari kwenda dar mbeya,au wanamgonjwa ila mshkaji akipimgia Mzee wake Mzee anakataa anasema gari kanunua kwa ajili yake sio biashara,ukiangalia Mzee mwenyewe hata Hela yakuweka mafuta sometime hana,anakataa sababu wanae huwa wanampa Hela ndogo wakishapata mteja wakupelekwa safar
 
1. Kama utaendesha mwenyewe
2. Sio unayoitegemea kwa kipato cha kila siku uwe na kazi zingine yenyewe ni inapotokea tu imekuja fursa yani ni pressure
3. Kazi yake iwe hiyo tu sio unapigia misele
4. Uwe na uwezo ukipata pesa yake walau 70% itunzike
Kinyume na hapo utalia utatafuta mteja wa kumuuzia usimuone
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…