Biashara ya pembe za Tembo kuishi ni ngumu, liko kiimani zaidi kwenye jamii ya Wachina na Thailand

Mkata Mtaa

Senior Member
Jun 10, 2016
136
142
Biashara ya pembe za Tembo kuishi ni ngumu sana, liko kiimani zaidi kwenye jamii ya wachina na Thailand, Wachina na Wathailand wanaomini dini ya Buddha sana zinachongwa kwa ni kwa kutumia pembe za ndovu.

Mapambo yote kwa jamii mengi wanatumia pembe za ndovu.
Ili kwenye jamii hiyo uonekane kiimani umekamilika lazima uwe na sanamu zilizochongwa kwa pembe, zinakuwepo ofisini unapoingia na nyuma ya kiti anachokaa, nyumbani unapoingia na sebuleni, kwenye Temple zao ndio ziko nyingi zaidi.

Buddha hawapungui, wanaongezeka zaidi maana familia za Buddha's zinazaa jamii ya Buddha, Hatari ninayo ona ni kwa Tembo wetu kuendelea kuangamia kila wakati, watajifanya wapiga marufuku kwao uko China lakini sio kweli, sababu wachongaji wa hizo sanamu wanajulikana bado wapo, Kwa Wathailand sio tishio kama wachina, sababu hawana mtandao mkubwa kwa nchi za Afirika Mashiriki na hawana pesa kama Wachina,

Viongozi wao wanajua na baadhi yao wanazo kwenye nyumba zao na wanavyokwenda kwenye Temple za Buddha wanaziona, Na hawakemei viongozi wa dini au watu wao waache kutumia sanamu na mapambo yanayotengezwa kwa kutumia pembe za Tembo maana liko kiimani zaidi.

Wanawasilisha.

IMG-20160505-WA0105.jpg
 
Unatofautishaje kwamba hawa wamekufa kifo cha kawaida au kwa ujangili? Jangili atakwambia hizi pembe zimepatikana kwa njia haramu?!
 
Wanaotumia pembe ni kwa ajili ya ugumu wake na haziharibiki hata miaka elfu.

Lakini la kushangaza mbona sioni wanashika kucha za tembo? Maana zinatumika kama ala za visu vidogo ingawa hatuoni faida zake huku
 
kweli, wanazitumia ili wapate utajiri, nakwambia kuna watu nawafahamu nao pia walikuwa nazo majumbani mwao... trust me wale watu wote wamekufa! hivi vitu huwa vina backfire vibaya sana...ndiyo maana namwomba MWENYE ENZI MUNGU awamalize wote wanao fanya ujangili huu pamoja na hao wanaoamini!
 
Back
Top Bottom