Mimi nikiona mtu anatapel mtandaon namuona haha akili...sababu mtandain hujui unamuuzia nani ao unakuwa unajiweka kwenye hatar sana
Mimi nauza bidhaa online
Kuna matukuo yashawahi kunitokea ikanifanya niwe muaminifu mara 100 zaidi
Kuna mteja alinifwata Facebook inbox akawa anaitaji saa (Ilikuwa ni kipindi kile corona imepamba moto) mteja alikuwa dodoma alikuwa anaitaji Saa, chat zetu hazikuwa ndefu yani alikuja messenger akataka kuona picha za saa vizuri baada ya kumtumia akataka kujua mzigo unamfikiaje maana alikuwa Dodoma nikamuelezea then akaomba namba yakutuma pesa apo n messenger (nilishangaa kwa mteja wa mkoani kuwa direct vile, nishazoea wateja wa mikoan ad uwaaminishe sana kuhusu uwaminifu wako ndio watume pesa) Basi nikamtumia yule mzee namba ya kutuma pesa, dakika mbili nyingi muamala ukasoma baada ya muamala kusoma nikaona jina kwanza nikashangaa uyu ndio mwenyewe au ni majina tu yanafanana, basi nikaandaa mzigo then nikamwambia anitumie ma jina ya kuandika kwenye mzigo na namba ya simu
lahaulla si akaamua kunitumia na picha kabisa na jina la utambulisho na kila kitu
basi nikautuma mzigo adi dom saa zikafika alifurahi sana saa zilikuwa nzuri sana asa ya mke wake aliipenda sana (kiukwel mpaka time hii sikuamin kama ni yule mzee kweli nilijua labda mtu tu wanafanana majina kaamua kunichekecha ili asatapeliwe)
Basi bwana siku zikapita akawa anaona Status zangu yeye alikuwa sio mtu wakuweka ata Status, tuliendelea kufanya biashara akiitaji Saa nikawa namtumia
Asa kuna kipindi akaja dar alikuwa yupo bize sana ila alikuwa anaitaji saa, akaweka oda ya saa 2 kama kawaida ya kwake na mkewe si nikampelekea bale bana ndio namkuta ni yeye mwenyewe nikasema eeeeeh ni kwel yan
Hii kitu ilinifundisha uaminifu sana, nilijiuliza lqbda ningekuwa tapeli yan yule mzee asingetumia ata nguvu kunikamata maana yeye mwenyewe ananguvu
Ninachoshukuru yule mzee alitokea kuniamin yan vitu vyake vingi akiwa ananunua kama vinaitaji kukaguliwa lazima aniagize mimi nivi check
Yan namba yake ndio namba ya mtu mzito sana kwenye hii nchi niliyo nayo