Biashara ya nje ya China yakua kwa kasi katika miezi mwili iliyopita

Biashara ya nje ya China yakua kwa kasi katika miezi mwili iliyopita

Yoyo Zhou

Senior Member
Joined
Jun 16, 2020
Posts
169
Reaction score
287
VCG111627282000.jpg
Idara Kuu ya Forodha ya China hivi karibuni ilitoa takwimu kuhusu biashara ya nje ya China katika miezi miwili ya kwanza ya mwaka huu, ikionesha kuwa, katika miezi hiyo, thamani ya biashara ya nje ya China ilifikia Renminbi yuan trilioni 7.73, ambalo ni ongezeko la asilimia 18.3 ikilinganishwa na mwaka jana kipindi kama hiki. Miongoni mwao, mauzo ya nje yalifikia yuan trilioni 4.62, ambalo ni ongezeko la asilimia 19.2, huku uagizaji ukifikia yuan trilioni 3.11, ambalo ni ongezeko la asilimia 17.1.

Hivi leo dunia inakabiliwa na ongezeko la vitendo vya kujilinda kibiashara, na hali ya biashara ya kimataifa ni ngumu na ya kutatanisha. Kwa nini biashara ya nje ya China inaweza kukua kwa kasi namna hiyo?

Siri ya Kwanza, ni kwamba muundo wa biashara ya nje ya China umebadilika kabisa.

Zamani, watu walipozungumzia bidhaa zinazotengenezwa na China, walitaja soksi, nguo, na bidhaa nyingine ndogo ndogo zenye bei rahisi. Lakini sasa, hali imebadilika kabisa! Katika miezi miwili ya kwanza mwaka huu, mauzo ya nje ya bidhaa za kielektroniki na bidhaa nyingine za teknolojia ya hali ya juu zinazotengenezwa na China yameongezeka kwa zaidi ya asilimia 27 ikilinganishwa na mwaka jana kipindi kama hiki, haswa mauzo ya magari, ambayo yameongezeka kwa zaidi ya asilimia 50. Hali hii inaonesha kwamba sehemu kuu ya mauzo ya nje ya China imebadilika kutoka bidhaa zinazotumia nguvukazi nyingi hadi zile zinazotumia teknolojia nyingi za ubora wa juu.

Siri ya pili, washirika wakubwa wa kibiashara wa China wameongezeka.

Kwa kuzingatia mazingira magumu ya biashara ya kimataifa, haswa kutokana na vita ya ushuru iliyoanzishwa na Marekani, China haijaweka mayai yake yote kwenye kikapu kimoja. Umoja wa Nchi za Kusini Mashariki mwa Asia (ASEAN) umeendelea kuwa mshirika mkubwa zaidi wa biashara wa China. Katika miezi miwili ya kwanza, jumla ya thamani ya biashara kati ya China na ASEAN ilifikia yuan trilioni 1.24, ambalo ni ongezeko la asilimia 20.3, huku biashara na Umoja wa Ulaya ikifikia yuan bilioni 998.94, ambalo ni ongezeko la asilimia 19.9. Wakati huohuo, biashara kati ya China na nchi zinazoshiriki katika Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja, ikiwa ni pamoja na Afrika, ilifikia yuan trilioni 4.02, ambalo ni ongezeko la asilimia 20.

Siri ya tatu, mnyororo wa usambazaji wa China unagusa dunia nzima. Baadhi ya watu wana shaka kwamba, viwanda vingi vya China vimehamia nchi nyingine zinazoendelea, sasa kwa nini biashara yake ya nje bado inakua kwa kasi kubwa namna hiyo? Hawajui kwamba vipengele vingi muhimu na malighafi za usahihi wa hali ya juu za viwanda hivyo bado zinahitaji kununuliwa kutoka nchini China. Katika miaka kadhaa iliyopita, vipuri muhimu vilivyotengenezwa nchini China na kuuzwa kwa ASEAN na Amerika Kusini vimedumisha ongezeko la zaidi ya asilimia 10 kila mwaka. Hali hii inaonesha kwamba China imekuwa kiini cha mfumo wa uzalishaji wa kimataifa.

Ikiwa nchi kubwa zaidi ya kibiashara duniani, ukuaji wa kasi wa biashara ya nje ya China si kama tu utaweka msingi thabiti wa maendeleo ya uchumi wa China, bali pia utaendelea kuleta uhakika muhimu kwa ukuaji wa uchumi wa dunia wenye misukosuko mbalimbali.
 
Back
Top Bottom