Biashara ya kuuza pumba

kiri12

JF-Expert Member
Dec 21, 2013
376
250
Habari wapendwa, nilikuwa nahitaji msaada mwenye kujua hii biashara ya kuuza pumba na chakula cha kuku imekaaje faida zake na mtu anatakiwa awe na mtaji wa kuanzia ngapi, na gharama zake gunia la pumba kwa bei ya jumla ni kiasi gani, mi nipo Dar maeneo ya Mbezi Louis.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Bwana PGO

JF-Expert Member
Mar 17, 2008
45,525
2,000
So far najua iko vizuri sana kwa mfano saa hizi pumba zimekua adimu sana
 

Mla Bata

JF-Expert Member
Jan 24, 2013
5,272
2,000
Hizo ni biashara mbili tofauti mkuu, pumba inasimama kama pumba na chakula cha kuku ni biashara nyingine ambayo kuna kipindi fulani ilikuwa inalipa sana kutokana na kila mtu kufuga kuku hasa wa nyama & mayai, nadhani ungespecify vizuri mkuu.
 

Mega Mind Nyerere

JF-Expert Member
Aug 10, 2017
2,209
2,000
Nenda kwenye mashine za kukoboa mahindi na nafaka mkuu. Kule utapewa ramani nzima. Watakuja mda sio mrefu wajuzi lakini.
 

The Monk

Platinum Member
Oct 12, 2012
17,253
2,000
Kama unamaanisha kweli na unataka kuifanya hiyo biashara, sitegemei utafanya maamuzi mazito ya kuwekeza kwa kuamini maneno ya hapa JF, hapa watu wote wanajua kila kitu lakini ukimuuliza mtu maswali ya msingi unaona kabisa hana uelewa na hajawahi kabisa kufanya kitu anachokielezea.

Ulizia hapo mtaani bei zikoje, nenda mashine wanazokoboa ulizia bei zikoje, fuatililia gharama za usafirishaji, kuhifadhi kisha upige mahesabu kama kuna faida. Kuna vitu lazima mwenyewe uchukue jukumu kupata habari za kuaminika na uhakika kabla ya kufanya maamuzi.

Ukipata muungwana anaefanya hiyo biashara akawa muwazi kukupa muongozo itapendeza sana.


carbamazepine
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom