Biashara kwenye mataa Dar marufuku

kalulukalunde

JF-Expert Member
May 27, 2016
1,056
1,083
WAZIRI wa Nchi katika Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kushirikiana na viongozi wa Mkoa kuhakikisha kuanzia leo hakuna mfanyabiashara atakayefanya biashara katika maeneo ya ‘mataa’.

Alimtaka pia kuhakikisha anawaondoa ombaomba wote waliopo katika makutano hayo na katikati ya jiji. Simbachawene alitoa agizo hilo jana alipofanya ziara katika Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka (UDART).

Alisema lengo la kuwaondoa wafanyabiashara na ombaomba hao ni kutaka kulifanya Jiji la Dar es Salaam kuwa na mwonekano mzuri.

“Kuanzia kesho (leo) sitaki kumuona mfanyabiashara katika maeneo hayo ya makutano na pembezoni mwa barabara watafutieni utaratibu ambao utawafanya wakae maeneo ambayo ni tofauti,” alisema na kuongeza kuwa, anataka katika maeneo hayo kuwepo na askari saa 24 ambao watahakikisha hakuna mfanyabiashara atakayefanya biashara baada ya kuondolewa.

“Acheni kukamata mama ntilie nataka askari hao watumike kuwakamata wafanyabiashara hao.., nataka askari hao wakae hapo saa 24,” alisema Simbachawene na kuongeza kuwa uchafuzi wa mazingira katika maeneo ya jiji kunachangiwa na uwepo wa biashara zinazofanywa katika mazingira ambayo sio rasmi.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alimuahidi Waziri huyo kuwa watatekeleza maagizo yote na kuahidi kuanza operesheni hiyo leo kama alivyomuelekeza. Simbachawene pia amewataka wamiliki wa vyombo vya usafiri kufuata sheria na kuacha kutumia barabara za mwendo kasi hususani pikipiki na maguta.

Alisema ili pia kukabiliana na changamoto ya foleni, serikali imejipanga kusimamia awamu ya pili ya utekelezaji wa barabara za mabasi yaendayo haraka inayotarajiwa kuanza mwakani. Simbachawene alisema tayari wameshafanya tathmini na utatumia miaka miwili hadi kukamilika kwake pia wapo katika mchakato wa kumtafuta mkandarasi kwa ajili ya ujenzi.

“Hii awamu ya pili itaanzia katika barabara ya Sokoine kuelekea barabara ya Kilwa hadi Mbagala na kutakuwa na barabara za juu katika makutano ya barabara ya Kawawa na Nyerere,” aliongeza
 
Omba omba pale moroko wapo kibao.. Makonda alikuja kwa mbwembwe nyingi siku hizi ni mtu wa kualikwa futari tu.. Mara yupo clouds anauza sura mara yupo na bosi wa GSM dahh!! Huyu jamaa.. Mbwembwe zilikuwa nyingi sana ..
Mwenzake naye anakimbia nimesikia anatembea usiku na askari kwenye bar zinazopoga mziki
 
WAZIRI wa Nchi katika Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kushirikiana na viongozi wa Mkoa kuhakikisha kuanzia leo hakuna mfanyabiashara atakayefanya biashara katika maeneo ya ‘mataa’.

Duh hapo ndio balaa hawajapewa hata notice au muda wa kujipanga, japo hao vijana huleta kero za hapa na pale barabarani kwa waendesha vyombo vya moto lakini inabidi kuwaondoa kwa ustaarabu.

Kuwapa muda kidogo wa kujipanga kuondoka si mbaya, ukiwafurumusha wengi wao wataishia kuwa frustrated na maisha na kujiingiza kwenye shughuli hatarishi kama ujambazi, uuzaji na utumiaji wa madawa ya kulevya etc. Kundi hili la "wafanyabiashara" hao ni rahisi sana kuingia kwenye vitendo hivyo maana tunajua wengi wao hawana elimu/ujuzi/kipato wala pakukimbilia.

Kwa upande mwingine wa shilingi labda ni tamko tu, maana hata omba omba walipigwa marufuku mkoa wa Dar es salaam na Mh. Paul Makonda lakini mpaka leo bado wapo kama kawaida,muda ndio utatupa majibu sahihi, tungoje tuone jinsi watakavyoondoshwa:rolleyes:
 
Ni bora hawa wa kwenye mataa kuliko wale wa kwenye railway crossing na mabango yanayowekwa karibu na barabara. Huzuia kuona treni kama inakuja na mbaya zaidi honi na vizuizi vya kuashiria treni kuja huwa havifanyi kazi. Ni sheeeedaaahhh!!!
 
Serikali wasimamie sheria bila kujali mtu, awe kilema au hajiwezi sheria lazima ichukue mkondo wake

Mmesikia yule aliye gongwa kariakoo,
 
Duh hapo ndio balaa hawajapewa hata notice au muda wa kujipanga, japo hao vijana huleta kero za hapa na pale barabarani kwa waendesha vyombo vya moto lakini inabidi kuwaondoa kwa ustaarabu.

Kuwapa muda kidogo wa kujipanga kuondoka si mbaya, ukiwafurumusha wengi wao wataishia kuwa frustrated na maisha na kujiingiza kwenye shughuli hatarishi kama ujambazi, uuzaji na utumiaji wa madawa ya kulevya etc. Kundi hili la "wafanyabiashara" hao ni rahisi sana kuingia kwenye vitendo hivyo maana tunajua wengi wao hawana elimu/ujuzi/kipato wala pakukimbilia.

Kwa upande mwingine wa shilingi labda ni tamko tu, maana hata omba omba walipigwa marufuku mkoa wa Dar es salaam na Mh. Paul Makonda lakini mpaka leo bado wapo kama kawaida,muda ndio utatupa majibu sahihi, tungoje tuone jinsi watakavyoondoshwa:rolleyes:
Muda ndio msema kweli cku zote
 
Aisee hii nchi hakuna anayeipenda!! Yani yule jamaa mhujumu wa uchumi ila Makonda anamuabudu khaaa!!!
1466248528597.jpg

Ona anavyo ogopa picha utadhani mwizi
 
“Hii awamu ya pili itaanzia katika barabara ya Sokoine kuelekea barabara ya Kilwa hadi Mbagala na kutakuwa na barabara za juu katika makutano ya barabara ya Kawawa na Nyerere,” aliongeza
Kama flyover kwenye makutano ya barabara ya Kawawa na Nyerere iko kwenye awamu ya pili ina maana ujenzi wa flyover ya makutano ya barabara ya Mandela na Nyerere Pale Tazara unahesabika kama uko kwenye awamu ya kwanza? Au hizo flyovers zote mbili ziko katika awamu ya pili?

Ila kiukweli uuzaji wa bidhaa kwenye makutano ya barabara upigwe tu marufuku. Utakuta wamachinga wanatembeza hadi mapanga na visu madirishani upande wa dereva jambo ambalo ni hatari kiusalama.
 
Kuna jamaa wawili pale Ubongo mataa mmoja anauza Korosho mwingine vitabu huwa wananifurahisha sana hasa huyu wa vitabu.

Utasiki mnunulie kitabu mwanao ajue kusoma anaanza "Mba mbe Mbi hiyo inauofuatia anaivuta kwanguvu kweli na sauti kali MBOOOOO
 
Back
Top Bottom