Biashara ipi ya meno ya tembo kuzuiliwa leo ?

Biashara ipi ya meno ya tembo kuzuiliwa leo ?

Joined
Feb 14, 2014
Posts
6
Reaction score
0
Tumeona mijadala mikubwa ya upigaji marufuku biashara ya meno ya TEMBO ikiendelea duniani na kutoa tumaini fulani la kutokomeza biashara hiyo.
Pamoja na mijadala hiyo kuendelea na kuendeshwa na watu maarufu lakini bado tumaini kuu la kutokomeza biashara hiyo halionekani kutokana na kwamba siyo mara ya kwanza watu kukaa na kutoa maoni yao juu ya usitishwaji wa biashara hiyo.
Kwanza kabisa niwapongeze wale wote waloona mbali ktk hilo na kuamua kukaa chini kuzungumzia JANGA HILO LA MAUAJI YA TEMBO ambalo linazidi kuwakumba wanyama hao ambao leo wanaishi ktk hali ya wasi wasi na mashaka ya kutoweka duniani na kubaki historia tu kama ya kina dinosaur na wenzake.
Mwanzo kabisa paliwekwa sheri chini ya CITES juu ya kuzuia kabisa biashara ya meno ya tembo na sheria hiyo ilijulikana kama "CITES APPENDEX 2" ambayo ilipiga marufuku biashara hiyo lakini pamoja hilo bado biashara hiyo iliendelea kufanyika huku nchi zinazoruhusu meno hayo kufanyiwa biashara ktk ardhi yake zikijulikana na zikiachwa bila ya kuchukulia hatua za kinadhamu na zakushikisha adabu.
Lazima tuamini kuwa jitihadi za makusudi zinahitajika ili kusaidia kuondoa janga hili la BIASHARA YA MENO YA TEMBO.
BIASHARA YA MENO YA TEMBO NI JANGA ambalo linahitaji kuzuiwa haraka kabla halijaleta madhara na madhara makubwa ya janga hilo ni kutoweka kwa wanyama hao.
Pongezi zangu ziwafikie wale wote ambao kwa namna moja au nyingine wanajitoa kupambana na biashara hiyo.
Kwa maoni wasiliana nasi kwa email=ningawildlifefoundation@gmail.com
 
Back
Top Bottom