Nimeuliza huku na kule kuhusu biashara inayolipa zaidi na majibu niliyopata ni mengi mpaka nachanganyikiwa.
Kuuza silaha katika soko jeusi, Uganga wa kienyeji wakati wa uchaguzi, Danguro la siri, Uongozi wa kisiasa, Guest House ndani ya Dar na Dodoma, Madawa ya kulevya, viwanda vya bidhaa feki,
Wengine wakasema Kuuza majenereta ya umeme, kubadilisha fedha za kigeni, mambo ya forodha, uandishi wa habari za kichunguzi, benki, uigizaji filamu
Walionichanganya kabisa ni waliosema nifungue kanisa halafu nitangaze kuwa mambo haya yanafanyika:
Misukule wanarudishwa, njoo upate mume unaemtaka, njoo utapata kazi mara moja, kupandishwa cheo mara dufu, kupona ukimwi, kupona kansa, kupona kisukari, kupata ubunge, kuheshimiwa, kuwa bilionea, kushinda kesi, kupata mtoto, kufufua au kuongeza nguvu za kiume, kurudisha ubikira, kumrudisha mpenzi aliyepotea, kumtawala mume wako, kurudishwa kazini, kununuliwa VX V8 kilimo kwanza na serikali hata kama cheo chako kidogo, kufuta laana zote na nuksi, kuondolewa mapepo na majini, kuongezewa uzuri wa sura, kupewa shepu inayovutia, kurefusha nywele, kurefushwa kimo cha kiungo chochote na upana, kuongezewa weupe, kupewa ndevu staili ya O kwa wanaume, kupendwa, kurudishiwa ujana, kupewa upako wa kwenda ulaya, Upako wa kuzungumza kiingereza fasaha na upako wa kutokufa.
Wanajamvi bado natafuta biashara ya kufanya, hawa washauri wamenichanganya naomba mnisaidie biashara gani inalipa?