Biashara inayokwisha na biashara isiyoisha

Jul 3, 2012
35
95
Salaam wanajukwaa..
Naomba kuweka uzi huu mfupi.

Ktk biashara kuna biashara ambayo bidhaa zake zinakwisha, na biashara ambayo haiishi.

Biashara ambayo bidhaa inakwisha ni kama duka, unajaza bidhaa kama bahasha, vocha, pipi unga, maharage, n.k

Biashara ambayo haiishi ni kama mashine kama kuwa na mashine za kufyatua matofali, mashine ya kusaga wewe kazi yako ni kusagisha na kukoboresha nafaka na kuzipeleka kwenye mfumo wa biashara inayokwisha.

Lengo la kuandika huu uzi ni kwasababu nimeona kuna posts zinazoulizia aina zipi mtu anaweza kuanzisha biashara za namna hii. Yaani biashara isiyoisha.
Kwa namna nyingine unaweza kusema ni kuwa producer na sio kuwa sana kwenye retailer business, japokuwa hata huku kwenye producer unaweza kuwa retailer kwasababu ukifyatua matofari 10,000, akija mtu anahitaji matofali 20 unaweza kuuza, au ukiwa unasaga mahindi na kupata unga kama kilo 500, mtu akija anataka kilo 10, unamuuzia..

Kwahiyo nashauri sana kwa watu wapya wanaotaka kuingia kwenye biashara waangalie zaidi biashara yenye mfumo wa isiyoisha.. Yaani producer.

Binafsi napenda sana biashara isiyokwisha. Sipendi biashara inayokwisha kwasababu naamini ni rahisi kuleta hasara.
Mfano: ukiwa unauza vocha, na ikiwa vocha moja itapotea basi hasara yake inabeba vocha nyingine nyingi.

Biashara isiyoisha ni biashara ambayo faida yake haihesabiki, yaani ukiwa na mashine ya matofari, utafyatua matofali kila leo kwa kiasi kinachohitajika. Lkn biashara inayoisha faida yake inahesabika., inajulikana.

Biashara isiyoisha inahitaji utunzaji ili idumu.. Japo biashara inayoisha pia inahitaji umakini zaidi ili kulinda dhamani uabidhaa kwaajili ya kulinda faida.

Ahsante

Sent using Jamii Forums mobile app
 

busha

JF-Expert Member
Jan 21, 2019
1,647
2,000
Wengi wanashindwa biashara ya kuproduce bidhaa kwa sababu ya milolongo mingi,,,,,

Mfano,,wewe fyatua tofali alafu mi nazilangua kwa bei nafuu naenda kuuza tofali zilizo kamilika,,

Wakati ww ulieniuzia producer ukatefte mchanga,ukanunue siment,vibarua na mambo mengine meengi,,


Sent using Jamii Forums mobile app
 

mvuv

JF-Expert Member
Feb 12, 2013
2,757
2,000
Umeangalia sana upande wa hasara lakin umesahau kwamba hakuna biashara isiyo na hasara. Hiyo unayoiita isiyoisha mashine ikiharibika kuna hasara, ikiibiwa n.k
 
Jul 3, 2012
35
95
Wengi wanashindwa biashara ya kuproduce bidhaa kwa sababu ya milolongo mingi,,,,,

Mfano,,wewe fyatua tofali alafu mi nazilangua kwa bei nafuu naenda kuuza tofali zilizo kamilika,,

Wakati ww ulieniuzia producer ukatefte mchanga,ukanunue siment,vibarua na mambo mengine meengi,,


Sent using Jamii Forums mobile app
Kumbuka kule unakokwenda kulangua ni kwa producer. Kwahiyo umesuport kwamba producer atauza kwa wingi na kwa kila mara, sababu ukishauza utarudi tene kwake.
Sasa wewe retailer unahitaji transport, muda wa kusubiri mteja, so utatakiwa kuwa na sehemu ya kuuzia bidhaa, na zaidi itakupasa kuwaamnia watu bidhaa ulizonazo.. Hapo unanisaidia producer kutangaza.


Sent using Jamii Forums mobile app
 

free lander

JF-Expert Member
Nov 7, 2018
253
250
Huduma haina kipato..
Biashara isiyoisha inakuingizia kipato. Tena huyu anaefanya biashara isiyoisha ndio moangaji wa bei. Yaani anauza kwa bei anayotaka iwe sokoni. Ukifikiria kwa makini utaona ninachomaanisha

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa nilivyoona uzi wako, iyo biashara isiyoisha ni huduma kama huduma zingine. na sababu eti huduma haina kipato si kweli ila tu ni kuwa aihamishiki "non transferrable" na unayoita biashara ya kuisha ni kuuza bidhaa ( tangible products) ambayo hata matofali yapo

Sent using Jamii Forums mobile app
 

MC RAS PAROKO

JF-Expert Member
Feb 14, 2013
505
500
Kwa nilivyoona uzi wako, iyo biashara isiyoisha ni huduma kama huduma zingine. na sababu eti huduma haina kipato si kweli ila tu ni kuwa aihamishiki "non transferrable" na unayoita biashara ya kuisha ni kuuza bidhaa ( tangible products) ambayo hata matofali yapo

Sent using Jamii Forums mobile app
Bora. Nimejaribu kumwambia akaniambia huduma haina kipato nikaona ni vyema nimuache kwanza..

Kwa mfano watu wamekuoshea gari ikawalipa wamekuuzia nini?

Au dry cleaner wamekufulia ukalipa nini walichookuzia?

Mtoa mada amepotoka wajameni..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jul 3, 2012
35
95
Kama kuosha gari ukapata jela
Bora. Nimejaribu kumwambia akaniambia huduma haina kipato nikaona ni vyema nimuache kwanza..

Kwa mfano watu wamekuoshea gari ikawalipa wamekuuzia nini?

Au dry cleaner wamekufulia ukalipa nini walichookuzia?

Mtoa mada amepotoka wajameni..

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama kuosha gari ukalipwa pesa ni service, je mjumbe wa nyumba kumi mtaani kwenu itaitwaje?

Mfano ninaamua kupanga ardhi kwa mkataba wa miaka 70 na serikali, kisha nikajenga barabara imara toka Dar mpaka Morogoro, nikaweka points za kulipia kwa anaepita. Biashara hii nikaifanya kwa miaka hiyo 70, unadhani hiyo ni huduma?
Maana mtanunua magari yatachakaa mimi barabara ni ukarabati mdogomdogo tu.

Namaanisha producers vs retailers.
Producer namuona ananufaika kibiashara kuliko retailer.
Siongelei services, labda services in business. Mf. Ktk bar kunakuwa na wahudumu ambao costs za zipo kwenye price of goods japokuwa pale wanafanya service.


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom