Biashara gani inalipa kati ya hizi?

komanyahenry

JF-Expert Member
Sep 15, 2017
903
1,352
Nahitaji kumfungulia wife biashara, baada ya kuongea nae yy binafsi ana wazo la kufungua duka la kuuza na kuoka cake za harusi, send off, birthday n.k ila mm binafsi nilikuwa nafikiria kumfungulia duka la kuuza simu na accessories zake. Naomba ushauri juu ya idea hizi mbili. Idea mpya ruhusa. Expected capital ni tshs 10 mil
 
Nashauri mfungulie hiyo ya Keki za Harusi, Send Off na Birthday kwakuwa ina ' wigo ' mpaka wa ' Kiuhitaji ' kuliko hiyo ya Simu na Accessories zake. Kila la kheri Mkuu.
 
Mfungulie alicho kitaka yeye atakifanya Kwa moyo mmoja.

Pia usikubali kuwa na ushirikiano wa moja kwa moja kwenye biashara ya mke wako. Muache afanye biashara yake, usiwe siku nyingine unauza wewe, sku nyingine yeye. Hapana inaweza kukugarimu mda mwingne.
 
Vp kama tutaamua kuongeza na mapambo ya sherehe pamoja na kukodisha mahema pamoja na viti?
Hadi mziki, in short inalipa na keki huwa zinatengenezwa kwa oda, na chakula hivo hivo tu.. Mnaweza uza chakula kwa oda hadi kwa wenye mikutano.

Munaweza kodisha hadi projectors, screen etc.. Ni wazo zuri sana.
 
Mkuu, kidogo minipo tofauti na wachangiaji waliitangulia.
Kwanza naomba nikuulize, wewe upo wapi, mkoa gani, wilaya gani?
Baada ya hapo itakua nivyema tukakushauri kutokana na eneo ulipo.
 
Mkuu, kidogo minipo tofauti na wachangiaji waliitangulia.
Kwanza naomba nikuulize, wewe upo wapi, mkoa gani, wilaya gani?
Baada ya hapo itakua nivyema tukakushauri kutokana na eneo ulipo.
Nipo DSM wilaya ya Kinondoni maeneo ya Mbezi Tangi Bovu
 
Niazime hiyo pesa mkuu, nitakurudishia mwezi november, halafu nitakupa na idea
Moyo huo kama wa yesu wa kupigwa kofi shavu la kulia kugeuza na la kushoto cdhani kama ninao kaka, labda unifanyie mfungo na maombi ninaweza badilika, mwenyewe vyuma vimekaza nimeamua kuongeza kipato cha familia kwa kutafuta biashara
 
Ningeshauri umsikilize yeye, mpaka kufikia kuomba alichoomba kaishajiandaa vya kutosha na ana uhakika wa anachotaka kukifanya..

Na kama ni mtu wa shughuli shughuli atakuwa na wigo mpana wa kupata wateja (oda).
 
Nahitaji kumfungulia wife biashara, baada ya kuongea nae yy binafsi ana wazo la kufungua duka la kuuza na kuoka cake za harusi, send off, birthday n.k ila mm binafsi nilikuwa nafikiria kumfungulia duka la kuuza simu na accessories zake. Naomba ushauri juu ya idea hizi mbili. Idea mpya ruhusa. Expected capital ni tshs 10 mil
Fungua kampuni ya kukodisha Mahema,Vitu,Maturubai, Vyombo vya harusi,Mapambo Ya harusi N.K

Lakini Pia baadhi pia ya huduma kwenye kampuni hiyo kama si nyingi zitakuwa zinapatikana pia kwenye misiba,sherehe na hafla za kila namna. Nakuhakikishia usipotusua kwenye biashara hii basi nitaamini bombadier ni carina TI.

Anza hiyo project in small scale, proportionately to your CAPITAL ila kwa lengo la kukua zaidi na zaidi. Na siku ikikua unaongeza na huduma za catering pia.

Kuna shughuli nimewahi fanya nikawa na interaction na hawa watu na kampuni zao. Kiukweli hela ipo cha msingi ni kuwa creative kutokufanana na huduma hizi hizi zitolewazo. KWa mfano kampuni ninezokutana nazo wanatoza nauli kubwa ya kukuletea viti au matent. Wewe unaweza kujipanga nauli ikawa inclusive kwenye hela ya kukodisha matents halafu unatangaza ni free delivery.

Pleaese ukiwa smart utatusua
 
Mfungulie hiyo kazi anayoitaka yeye ila uongeze na vitu vingine kama kukodisha viti na matent ila umuache afanye mwenyewe na umwambie kabisa awe siliasi kwa maana kuwa akicheza hela ikapotea maanake ameua familia maana kuna wanawake wengine huwa hawako siliasi kwa kujua kuwa mume wake yupo ataleta pesa,kila la heri!!
 
Kwa wakati huu kuna biashara ambazo ni direct consumable kama hiyo ya keki.
Ila simu mmh!!! kwa vyuma hivi atapatatabusana
 
Back
Top Bottom