Bia za TBL na afya ya wanywaji

taffu69

JF-Expert Member
Feb 26, 2007
2,094
538
Katika siku za hivi karibuni nimeshuhudia vifuniko ambavyo vinatumika kufunika bia za TBL vikiwa na kutu kwa kiwango kikubwa. Bia ambazo nimekumbana nazo binafsi ni Kilimanjaro na Ndovu ambapo mara inapofunguliwa unakumbana na layer kubwa ya kutu kwenye mdomo wa chupa na kifuniko chenyewe na wakati mwingine chupa ikiwa imelika kwa kiwango fulani.

Naomba kupata ufafanuzi kutoka kwa wahusika wa TBL kama tatizo hilo wameshaligundua na hatua ambazo wamechukua ili kukabiliana nalo. Jambo hili limenishtua sana kwani kwa wale wanywaji ambao hawatumii glass wanahatarisha afya zao kwa kiwango kikubwa kwani wanakuwa wanameza uchafu huo moja kwa moja. Kwa upande mwingine hata wale wanaotumia glass wanaweza kuwa hatarini pia pale wanapojimiminia kinywaji hicho bila kufuta chupa hiyo kwa makini ili kuondoa uchafu huo.

Swali la kujiuliza ni kuwa wahusika wa TBS hawajaona tatizo hili ama wanasubiri madhara yatakapotokea ndiyo waanze kuchukua hatua?. Nimezungumzia suala la bia kutoka TBL lakini inawezekana kwamba hata bia zinazozalishwa na makampuni mengine zina tatizo linalofanana na hilo pia.
 
Hasa bia za NDOVU amabzo0 zinafunikwa na karartasi za rangi ya gold. Hivi hivyo vizibo huwa TBL wanaokota au wana recycle lakini hawazisafishi? afya zetu ziko hatarini. mimi nimeaxzha kunywa ndovu sababu ya hiyo kutu
 
Omba tishu ufute wewe, kwani hujui reaction za chuma na vitu vingine ambapo Oxygen haikosekani? Basi TBL watumiwe vizibo vya Aluminium au Stainless steel ndo utakosa kutu. Hebu Fimbo Butallah atuelekeze hapa.
 
Ni kweli kabisa hili swala la vizibo ni la muda mrefu, mwanzoni walioanzisha Ndovu hii vizibo vilikuwa vipo bomba pasipo kutu..ila kwa sasa naona sijui zinakaa muda mrefu kwenye shelf zao ...Ila ni kweli ENG. hapo amenena ukweli wa kemia reaction ya O2 na chuma! lazima kutokee rust
 
Hasa bia za NDOVU amabzo0 zinafunikwa na karartasi za rangi ya gold. Hivi hivyo vizibo huwa TBL wanaokota au wana recycle lakini hawazisafishi? afya zetu ziko hatarini. mimi nimeaxzha kunywa ndovu sababu ya hiyo kutu

Ukweli ni kuwa vizibo vinavyotumika ni vipya(not re-usable), tatizo ni kuwa baada ya pasteurization bia inakuwa na maji maji. Kinachotakiwa kufanyika ni kuzikausha kwa upepo (air blowing) kitu ambacho hakifanyiki/kinapuuziwa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom