wewe pia mdini. kwani mapdri sio pekee ndio wenye mamlaka nchi hii?
Hakika wewe ni kiboko, kila kitu unapinga bila kujadili hoja. Hebu jaribu kujadili hoja kwanza n kisha onesha msimamo wako. Je wewe unalishwa na rais kwa sababu ni wa dini yako. Ni muhimu kama wadau kubadilishana uelewa wa jambo linawekwa mezani kwa kujadili ubaya na uzuri bila kukimbilia kuunga mkono au kupinga hoja. Kwa ujumla masuala yoyote yanayohusu dini hayana faida kwa Taifa hili, na hakuna mtu ambaye atashinda nafasi ya Urais kwa kutegemea kundi la wanadini wenzake.
Nchi inhitaji kutafutia suluhisho tatizo la udini. Je kuna mtu anaweza kuwa hana imani yoyote katika maisha yake. Je tutamweka wapi mtu ambaye hana imani yoyote, je imani ya mtu ndiyo iwe sifa ya kuwa kiongozi wetu? Hebu tujadili kwa staili hii, je kwa kuwa muislamu, Mhindu, mpagani au mkristo inakufanya kuwa kiongozi mzuri kwa Taifa hili?
Taifa linakumbwa na matatizo mengi ambayo yanatuumiza wote bila kujali dini ya mtu. Je foleni ya magari Dar es Salaam inajali kwamba wewe ni muislam au Mkristo? Je ukosefu wa maji, barabara, huduma bora za afya,elimu bora zinachagua dini ya mtu? Ni muhimu tukawa tayari kujadili hoja kwa nia
1. kuelimisha wengine juu ya ufahamu wako kuhusu hoja iliyopo jukwaani,
2. kutushirikisha uelewa wako kuhusu tatizo na kupendekeza namna tunavyoweza kuliondoa tatizo husika
3. Tushirikishe msimamo wako kuhusiana na tatizo lililopo.
Kwa njia hii jukwaa linakuwa chanzo cha elimu na maarifa, pia tutajua namna ya kuchambua masuala mbalimbali kupitia michango ya wengine, lakini kwa staili ya Malaria Sugu hatoi fursa hiyo kwa wengine.
Lakini naamini anacheza kwenye sehemu yake ya kujidai "Uhuru wa kutoa maoni"