Mkuu usiogope hata kidogo kwa hawa ndg zetu, mama zetu, wake zetu, dada zetu nk hicho ni kitu unaweza kusema ni common kwao. Binafsi ukiniuliza huwa ni kitu gani kwa kweli sujui hata kidogo na kwa sasa sidhani kama nahitaji kujua huwa wanasumbuliwa na kitu gani. Ila ukweli inasumbua sana, inakera sana pindi hiyo hali inapotokea na mbaya zaidi majibu yao ni kama ulivyomnukuu huyo mchumba wako, kwamba hakuna tatizo ili hali wewe unaona utofauti.
Iliwahi kunitokea mara ya kwanza kwa mke wangu bila experience yoyote kwa takribani siku mbili ama tatu, ilinikera, ilinikwaza. Sasa siku moja katika maongezi na mama mmoja mtu mzima mwenye age ya around 52, ni staff mwezangu lakini kama yangu na pia ni mama mchungaji, sasa katika maongezi tukafikia kuzungumzia hiyo situation kwa wanawake, alinihoji kwa ufupi sana kuwa "hivi hiyo hali huwa inawakera sana" mwisho wa kunukuu. Kumbe basi nikajua hii kitu huwa ni common kwa wenzetu na kuna kipindi inatokea na ni ya mpito, usihofu mkuu.
Aidha pia niliwahi kuambiwa kuwa Japan hakuna mameneja ama viongozi wa ngazi ja juu wanawake kwa level za maamuzi labda huyu mwanamke huyo awe wa umri mkubwa maana, kwa umri ,mdogo ama wa kati inasemekana (sina hakika hapo, naomba nisihukumiwe na wanawake) ya kwamba kuna kipindi fulani wanapatwa kama na ukichaa fulani hivi na baadaye hurudi kwenye hali ya kawaida, sasa basi kwa kuwa wao wanataka positive output kwenye kazi zao hawataki kusikia hizo excuse na mambo kama hayo hivyo wanawekwa pembeni.
Mwisho kabisa, narudia usigope, kama una wito wa ndoa itika na Mungu atakuwa pamoja nanyi hizo ni changamoto ambazo ukiwa mwenyewe zitakuwa zaidi ya hapo.