Habari za Easter Monday wana MMU,natumaini ni bukheri wa afya
Kwa mara ya kwanza naandika uzi katika jukwaa hili ambalo kwangu mimi naliona jukwaa muhimu sana lenye kufunza katika kujenga msingi bora wa familia za baadae.
This thread is inspired by the tv series I have been watching since last week,inaitwa BETRAY,inapatikana hapa kama utapenda kuiangalia
Watch Online Betrayal - Watch Series
Kilichonisukuma zaidi pia ni baada ya kuona usaliti umekuwa tatizo kwa wana ndoa na walio kwenye mahusiano.Usaliti ninaongelea hapa ni ule ambao mtu anasukumwa na sababu mbalimbali za kimazingira ya kawaida ya maisha na za kihisia kufanya usaliti huku nafsi yake ikiwa inamsuta,na si ule usaliti wa mtu kuwa na tabia tu ya ukicheche.
Katika maisha kuna wakati unaweza kukutana na coincidence na kama zitakuwa nyingi huwa kibinadamu inatufanya tuchukulie kama vile ndio destiny,when there are too many coincidences it is human to think that it is destiny.Katika hiyo series muhusika mkuu ni mke,ambaye amejikuta yupo kwenye coincidence nyingi na mwanaume mwingine kiasi cha kumfanya ahisi kuwa huyo mwanaume ni bora kuliko mme wake japo inamuuma.Mbaya zaidi mme wake ni mtu ambaye yupo busy na hampi attention ya kutosha.
To make story short,kimsingi kuna wakati ktk maisha unaweza kupata kila sababu ya kuona kuwa usaliti ni jambo sahihi.Unaweza kukutana na mtu nje ambaye mpo compatible mno kuliko mme/mke wako,na your paths always cross each other to make a series of unplanned coincidences,mbaya zaidi on the other side mme/mke wako anakuwa hana muda na wewe na mmekua hamuelewani kwa kipindi hicho.Hili huweza kukufanya uhisi kwamba kuwa na huyo mtu wa nje ni jambo sahihi.
There is nothing that justifies betrayal hata kama mme/mke wako anakupa kila sababu ya kusaliti and fate has given u all the reasons to be with the other man/woman,japokuwa si kila usaliti mtu anaufanya kwa kupenda ila mazingira tajwa hapo juu yanamsukuma na kibinadamu ni kazi kuyakwepa kama huna misimamo thabiti.As long as uliweka kiapo njia sahihi ni kuongea na mwenzio bila kuchoka,kumueleza unavyojisikia na kumkosoa kuhusu mabadiliko yake.Kama utashindwa kabisa omba divorce ila ukumbuke kuwa hata huko unapoenda kuna siku itafika huyo mtu naye hatokupa attention so utaomba divorce pia?
Mwisho,ndoa ni changamoto na suluhisho sio talaka wala kuchepuka.Tafuta movie ya Nigeria kwenye YouTube inaitwa MR AND MRS uone mfano wa mke mwema mwenye maamuzi sahihi.Pia tafuta movie inayoitwa "Temptation: Confessions of a Marriage Counselor" uone jinsi mume bora ambavyo anamvulia mke ambaye katoka nje ya mstari.Kumbukeni pia kusali,kuomba Mungu awaepushe wenzi wetu na hizo changamoto.
Wasalaam,niawatakie siku njema wana MMU