1000 digits
JF-Expert Member
- Oct 16, 2012
- 7,175
- 9,497
Huyu ni kada pekee wa CCM aliyethubutu kusimama na kusema ukweli juu ya kile kilichotokea Zanzibar.
Hakuna ubishi kuwa yaliyotokea Zanzibar ni mambo yanayoliaibisba taifa letu kimataifa.
Namuunga mkono mzee Membe kwa asilimia 100%.
Nchi yetu imekua mfano wa kuigwa barani Afrika kutokana na umoja na mshikamano.
Umoja wetu unatokana na misingi ya kuaminiana na kutobaguana iliyowekwa na waasisi wetu.
Sasa leo hii baadhi ya makada wa CCM wanajenga mfumo wa kibaguzi na kutowaamini watanzania wenzao walioishi nao na kulitumikia taifa hili kwa Muda mrefu. Maalim Seif amelitumikia taifa hili tangu serikali ya awamu ya kwanza na kushika nafasi za juu za uongozi ktk serikali ya mapinduzi Zanzibar, leo hii wananchi wamemchagua awe Rais wao halafu Jecha na waliomtuma wanagoma kumtangaza na kuamua kufuta matokeo yoooote ya uchaguzi. Eti kulikua na dosari tatu tu ,tena ambazo hazikuathiri zoezi la kupiga.
Dosari hizo ni :-
(1) Maalim Seif Kusema kuwa ameongoza kwa idadi ya kura,
(2) Baadhi ya wajumbe wa ZEC kupigana(japo hatukuambiwa kuwa walikua wanapigania kitu gani ;suala la uchaguzi au walikua wanapigania wanawake au wanaume,tumeambiwa tu walipigana!!!!!!) na
(3) Idadi ya wapiga kura kwenye baadhi ya vituo kuruhusu watu wasiojiandikisha kupiga kura.
Naendelea kumuunga mkono na kumpongeza Mh. Membe kwamba dosari zilizojitokeza ni za kawaida kwenye chaguzi zote duniani. Hakuna uchaguzi usio na dosari.
Dunia nzima dosari zinazoweza kurudia uchaguzi baadhi tu ya maeneo ni zile zinazowasababishia wapiga kura kushindwa kufanya zoezi la kupiga kura. Mfano wapiga kura kukosa vifaa vya kupigia kura ,kutokea kwa vurugu kubwa zinazosababisha wasimamizi na wapiga kura kushindwa kusimamia au kutumia haki yao kupiga kura na pengine karatasi za kupigia kura kuchanachanwa na watu kwa lengo la kuvuruga zoezi zima la kupiga kura. Na haya hayawezi kamwe kutokea nchi nzima. Na endapo yatakuwa yametokea nchi nzima basi uchaguzi unaahirishwa bila kuendelea na zoezi zima la kupiga na kuhesabu kura.Jamii nzima za kimataifa wanakua wameliona hili na kutangaza kuwa uchaguzi haukua huru na amani. Haya hayakujitokeza Zanzibar.
Kwa mara ya kwanza kabisa imetokea kwa tume kufanya kazi ya Mahakama.
Mshindi anapotangazwa na kupewa hati ya ushindi kama mbunge au mjumbe wa baraza la wawakilishi, inakua ni jambo la aibu kwa tume kupokea malalamiko na kutengua uteule huo. Jecha angeweza tu kutengua matokeo ambayo yalikua hayajatangazwa ikiwemo ya urais wa Zanzibar.
Lakini matokeo yote ya wawakilishi yaliyokua yametangazwa rasmi na tume alikua hana mamlaka tena ya kuyafuta. Hiyo ilikua ni kazi ya mahakama endapo wangejitokeza watu kupinga ushindi wa mtu mmoja mmoja. Hata Tanzania bara dosara zilikuwepo lakini uchaguzi uluendelea na matokeo yalitangazwa kama kuna malalamiko basi watu wanakwenda mahakamani na mahakama itatoa maamuzi ya haki.
Huu ndio utawala wa sheria.
Kila uchaguzi unakua na malalamiko yake na hasa kwa wale wanaoshindwa.
Kazi ya tume sio kupanga nani ashinde au nani asishinde.Kazi ya tume ni kuratibu na kusimamia zoezi zima la kupiga kura ili lifanyike kwa huru na haki.Baada ya kupiga kura tume inahesabu na kujumlisha kura kisha kumtangaza aliyepata kura nyingi kuwa ndiye mshindi na kisha kumkabidhi hati ya ushindi kama mteule. Baada ya hapo mwenye malalamiko anakwenda mahakamani.
Jecha alichofanya kwa wawakilishi sio sahihi kabisa. Alipaswa kutoa adhabu kwa wajumbe wa ZEC waliopigani bila sababu za msingi au kuwashitaki polisi kwa kupigana adharani lakini sio kufuta uchaguzi.
Kupigana ni kosa la jinai. Pia alitakiawa atoe adhabu kwa maalim Seif na hata kuyafuta matokeo ya urais na kumzuia kugombea ingeleta maana isiyo na shaka kama sheria inasema hivyo na aiainishe bayana.
Pia Jecha angeweza tu kurudia uchaguzi kwenye majimbo yale yaliyokiuka taratibu za uchaguzi kabla ya kuwatangaza washindi.
Kwa hali ilivyo inaonekana dhahiri kuwa alichofanya Jecha ni ubabaishaji na kukurupuka kwa maamuzi binafsi au kusukumwa na maamuzi ya chama kimoja ambacho kinaweza kikawa ni CCM au vyama vingine vilivyoshindwa vibaya.
Kutoka na maamuzi ya Jecha ya kushindwa kusimamia uchaguzi na kusababisha hasara kwa serikali ,sio tu alipaswa ajiuzulu lakini pia atumbuliwe kama majipu mengine yanayoshidwa kutimiza majukumu yao na kufikishwa mahakamani.
Jecha nalo ni jipu linaloisababishia nchi yetu hasara linapaswa litumbuliwe.
Yaliyotokea Zanzibar ni aina mpya ya mapinduzi yanayotaka kuanzishwa na huenda yakaigwa na nchi nyingi za Afrika na watawala wasiopenda demokrasia.
Aina hii ya mapinduzi na ubakaji wa demokrasia kwa Tanzania huenda ukapita salama kabisa na wananchi wakaendelea na maisha yao huku wakiugulia rohoni lakini kwa viongozi wengine wa nchi za kiafrika wanaweza kuiga huu mfumo mpya wa mapinduzi na matokeo yake wakaishia kuingiza nchi zao kwenye machafuko. Tanzania tujiangalie tusije tukawa waasisi wa aina mpya ya mapinduzi na ubakaji wa Demokrasia dunia.
Eti uchaguzi urudiwe bila kupiga kampeni za kuwamasusha watu kujitokeza kupiga kura. Huku ni kuwanyima fursa wagombea wengine wasio na majukwaa ya kujitangaza na kumbeba Dr. Shein na Mawaziri wake ambao watatumia shughuli za kiserikali kujinadi wao na chama chao.
Swali langu ni je, Maalim Seif au mgombea akishindwa na akatokea hadharani kukubali na kujitangaza kuwa AMESHINDWA na kuonyesha kuwa kura zake hazikutosha kabla ya tume kutangaza matokeo ya urais ; uchaguzi utarudiwa tena????
Mwisho nimpongeze tena mzee wetu Membe kwa kusema, "Mzee umeonyesha ukomavu wa kidiplomasia ,nitakuunga mkono daima".
Wako wapi viongozi wa dini,siasa,wanazuoni na wapenda haki wajitokeze kumuunga mkono Membe!!!?