Return Of Undertaker
JF-Expert Member
- Jun 12, 2012
- 4,572
- 26,885
Benki nchini zaimarika 2016
Katika robo ya tatu ya mwaka 2016, Benki ya CRDB inayohudumia zaidi ya robo ya wateja wote wa sekta hiyo ilitangaza kupata hasara ya takribani Sh2 bilioni huku Twiga Bancorp ikishindwa kujiendesha hivyo kuwekwa chini ya uangalizi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) wakati akitafutwa mwendeshaji mpya.
Dar es Salaam. Ripoti za mwaka za sekta ya fedha nchini zinaonyesha kuwa baadhi ya benki zimeimarika mwaka jana na kuweza kuongeza matawi na kuajiri wafanyakazi huku nyingine zikifanya vibaya.
Kutolewa kwa ripoti za benki hizo kumepunguza hofu ya wadau wa fedha na uchumi ambao walipatwa na taharuki baada ya kutolewa kwa taarifa za robo ya tatu ya mwaka 2016 iliyobainisha baadhi kupata hasara huku nyingine zikishindwa kujiendesha.

Kwa mujibu wa ripoti za mwaka za benki 10 ambazo Mwananchi imezipitia, tano zimeweza kuongeza idadi ya wafanyakazi wake huku tano zikipunguza. Benki za NMB, CRDB, KCB, Maendeleo na FNB zimeajiri jumla ya wafanyakazi wapya 750 huku Letshego, UBL, TADB, DCB, Access na NBC zimepunguza wafanyakazi jumla ya 210.
Hata hivyo, Mkaguzi wa Hesabu za Fedha na mtaalamu wa masuala ya benki, Reginald Baynit alisema kupungua kwa watumishi katika baadhi ya benki haimaanishi zimewaachisha kazi.
“Inawezekana wamestaafu au wamehamia kwenye benki zilizoongeza watumishi. Kuhama kutoka benki moja kwenda nyingine ni suala la kawaida sana kwenye sekta hii,” alisema.
Benki ya NMB yenye matawi 187, katika robo ya nne ya mwaka jana ilipata faida ya Sh31.81 bilioni zilizochangia faida ya Sh154.22 bilioni za mwaka mzima ikilinganishwa na Sh150.29 bilioni mwaka 2015. Ndani ya mwaka 2016 benki hiyo iliajiri wafanyakazi 269.
Benki nyingine, CRDB yenye matawi ndani na nje ya nchi imepata faida pia licha ya kutangaza hasara ya takriban Sh2 bilioni kwenye robo ya tatu ya mwaka huo.
Mwaka mzima, benki ilitengeneza faida ya Sh73.42 bilioni ikiwa ni pungufu kwa takriban ya Sh50 bilioni ikilinganishwa na Sh122.37 bilioni ya iliyopatikana mwaka uliotangulia. Mbali ya faida hiyo, pia benki iliongeza idadi ya watumishi wake kutoka 3,163 mpaka 3,432 na matawi 13 hadi kufikia 187.
Hesabu za jumla za benki (CRDB Group) hiyo yenye matawi ndani na nje ya nchi, zinaonyesha kupatikana faida ya Sh78.84 bilioni ambayo ni pungufu ikilinganishwa na Sh128.98 zilizopatikana mwaka 2015 ingawa matawi yake yaliongezeka kutoka 199 mpaka 250.
Ufanisi wa Benki ya NBC katika robo ya mwisho iliyoishia Desemba umewezesha kupatikana kwa faida ya Sh7.85 bilioni na mwaka mzima ilipata Sh13.74 bilioni.
Mwaka 2015, ilipata faida ya Sh12.04 bilioni zilizochangiwa na Sh5.58 bilioni zilizopatikana kwenye robo ya mwisho. Faida ya jumla ya benki hii imeongezeka kwa Sh1.7 bilioni ndani ya mwaka uliopita.
Hata hivyo, imepunguza idadi ya wafanyakazi wake kutoka 1,264 mpaka 1,212 kwenye matawi yake 52 ambayo hayajaongezeka ndani ya mwaka huo.
Benki ya TPB (Posta) iliyopata faida ya Sh10.19 bilioni ikiwa ni ongezeko la Sh2 bilioni imepunguza wafanyakazi 53 licha ya kufikisha matawi 30 nchini kote baada ya kuongeza tawi moja.
Benki ya KCB imepunguza wafanyakazi 14 ndani ya muda huo huku ikiongeza tawi moja na kuwa nayo 14 licha ya faida ya Sh6.29 bilioni iliyopata mwaka jana.
Benki ya Access iliyopata hasara ya Sh2.39 bilioni mwaka 2015 ilipata faida ya Sh271 milioni mwaka jana na kufanikiwa kuongeza tawi moja hivyo kuwa nayo 13. Lakini imepunguza wafanyakazi wake kutoka 880 mpaka 828.
Faida ya Benki ya DCB imepungua kutoka Sh3.09 bilioni mwaka 2015 mpaka Sh1.12 bilioni mwaka jana. Upungufu huo umejitokeza kwenye idadi ya watumishi wake pia, kutoka 225 mpaka 210 licha ya kuongeza tawi moja na kuwa nayo tisa.
Benki ya Maendeleo imeongeza wafanyakazi 23 waliochangia kupaisha faida yake kutoka Sh178 milioni mwaka juzi mpaka Sh1.14 bilioni mwaka jana sambamba na kufungua tawi jipya. Sasa ina matawi mawili.
Mabadiliko yameonekana katika Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) ambayo imepunguza wafanyakazi wawili, inao 39, ingawa ilipata faida ya Sh1.59 bilioni baada ya kupata hasara ya Sh1.1 bilioni mwaka uliopita.
Pamoja na kuongeza tawi moja na kupunguza mfanyakazi mmoja, Benki ya UBL imepata hasara ya Sh2.19 bilioni kutoka faida ya Sh223 milioni mwaka juzi. Benki ina matawi mawili na wafanyakazi 32.
Wafanyakazi 20 wamepunguzwa kwenye Benki ya Letshego na imeendelea kubaki na matawi matano iliyokuwa nayo kutokana na kuongezeka kwa hasara inayopata. Hasara imepungua kutoka Sh4.76 bilioni mpaka Sh1.92 bilioni.
Hali inaenda tofauti kidogo kwenye Benki ya FNB ambayo imeongeza wafanyakazi wake kutoka 233 mpaka 284 wa kuhudumia matawi yake 10 baada ya kuongeza mawili mwaka juzi. Mwaka juzi ilipata hasara ya Sh21.64 bilioni na mwaka jana imepata hasara ya Sh20 bilioni.
Licha ya faida zilizoripotiwa, Baynit alieleza uwezekano wa kupungua kwa mikopo kutoka kwenye taasisi hizo. “Benki inaweza kuwa inapata faida inayopungua, hii siyo nzuri kwa mustakabali wake,” alisema.

- Kutolewa kwa ripoti za benki hizo kumepunguza hofu ya wadau wa fedha na uchumi ambao walipatwa na taharuki baada ya kutolewa kwa taarifa za robo ya tatu ya mwaka 2016 iliyobainisha baadhi kupata hasara huku nyingine zikishindwa kujiendesha.