Benki ya Walimu Tanzania

wa hapahapa

JF-Expert Member
Aug 22, 2012
7,455
4,388
Wadau wa jf.

Hii benki ya walimu imeshaanza kazi za kibenki au bado?, na kama bado nini kikwazo?

Maana mara ya mwisho walitoa orodha ya wanahisa(walimu) walionunua hisa kwenye magazeti.
 
Hiyo benki ni viini macho, kuna ndugu yangu ni mwalimu aliniambia tayari imeanza lakini ni kwa Dar es salaam tu.
 
Natamani kile chama kifutwe kabisa. Danadana za viongozi wake zinachefua
 
Zamani ziliwahi kufanyika jitihada za kuimarisha benki ya wanawake. Naamini kuna mpango wa benki ya vijana na baadaye benki ya wazee kisha tutamalizia benki ya watoto.
Serikali ya Tanzania inaona suluhu ya huduma bora za kibenki ni kuanzisha benki nyingine badala ya kuimarisha huduma kwa benki zilizopo. Walimu wangekopeshwa kwa riba nafuu hata kwa benki zilizopo hivyo hakuna haja ya walimu kuanzisha benki yao. Ndoto yangu ni kushuhudia benki ya madaktari, madereva na makondakta:p
 
Kazi ipo.....!!
 
Hiyo benki ni viini macho, kuna ndugu yangu ni mwalimu aliniambia tayari imeanza lakini ni kwa Dar es salaam tu.

baada ya kuperuzi nikapata taarifa kuwa Mwalimu Commercial Bank itaanza kazi May-2016 kwa mtaji wa bilioni 31 Tsh..
 
Natamani kile chama kifutwe kabisa. Danadana za viongozi wake zinachefua
Haya bhana kwa kuwa TUICO, RAAW, TALGWU nk wanachama wao hawalipi ada ya 2% na wanawasaidia sana wanachama wao kudai haki kwa waajiri bila kuchelewa... Mwambie Makonda awaambie TUICO iwafanye walimu kuwa wanachama wake.
 
baada ya kuperuzi nikapata taarifa kuwa Mwalimu Commercial Bank itaanza kazi May-2016 kwa mtaji wa bilioni 31 Tsh..
Haha mkuu hawa si ndo wale walitangaza ajira za job on training afu mixer wakasema tangazo ni feki! kwel pesa ya walimu imeliwa njenje aisee!
 
icho chama cha walimu naona hakina tofauti na Nssf wanachama wapo hoi chama kina afya njema..
 
Wanachojua ni kukata mishahara ya walimu.Ni wakati sasa wakaacha utaratibu wao wa kijambazi wa kukata 2% ya mishahara ya walimu kila mwezi kwa madai eti ni ada ya uanachama.huu ni unyonyaji .cwt haimsaidii mwalimu bali kumdidimiza.
 
Vzr ifunguliwe haraka nchi nzima isaidie walimu. Kwani walimu wanalalamika makato na riba kubwa ya mikopo kwenye mabenk mengine.
 
inaanza mwezi wa saba

unasema kweli ? au nimatumaini tu.

hivi wanawapigisha watu interview

Haha mkuu hawa si ndo wale walitangaza ajira za job on training afu mixer wakasema tangazo ni feki! kwel pesa ya walimu imeliwa njenje aisee!

kama imeshindaka, wangerudisha pesa za wanahisa

wengne wanajutia!

ni heri pesa ingenunuliwa mifugo pengne wangeshazaliana

au wangewekeza ktk biashara na kilimo

Back
Top Bottom