Benki ya CRDB yatambulisha mkopo wa kidijitali wa 'jinasue'

Blasio Kachuchu

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2016
Posts
573
Reaction score
359
Katika mpango wake wa kuongeza ujumuishaji wa wananchi kiuchumi, Benki ya CRDB imezindua huduma ya mikopo ya Jinasue inayowalenga wateja wake wote wenye uhitaji wa fedha.

Huduma hiyo iliyozinduliwa na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya CRDB, Stephen Adili itawaruhusu wateja wa benki wenye salio dogo kwenye akaunti zao kuliko muamala wanaotaka kuifanya au wateja wanaohitaji fedha kutokana na dharura walizonazo.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo, Adili amesema ujumuishi wa kifedha ni ajenda ya kimkakati ndani ya Benki ya CRDB inayoamini suala hilo ni msingi wa mapinduzi ya kiuchumi katika jamii yoyote.

“Tunayo mikopo inayowalenga baadhi ya wateja wetu kama vile watumishi, wanafunzi wa vyuo vikuu na wastaafu pamoja na wafanyabiashara. Tumegundua kuna watu ambao hawapo kwenye makundi hayo ambao wanahitaji uwezeshaji hivyo kuja na Jinasue, mikopo inayomlenga kila mteja wa benki yetu,” amesema Adili.
Mikopo hiyo, amesema itakuwa inatolewa kwa kushirikiana na kampuni ya CreditInfo na itatolewa kupitia SimBanking kuwawezesha wateja wetu kumudu gharama za huduma, bidhaa, na ankara mbalimbali wanapokuwa na changamoto za kifedha.

Kupitia SimBanking, wateja watapata mikopo ya Jinasue kwa urahisi kuanzia Shilingi 1,000 hadi Shilingi milioni 1 kwa riba ya asilimia 8 tu. Ili kupata mkopo huu, mteja anatakiwa kuwa anatumia akaunti ya Benki ya CRDB na amejiunga na huduma ya SimBanking.

“Mkopo wa Jinasue ni suluhisho muhimu kwa wateja wanapokabiliwa na changamoto za kifedha wakati wa kulipa ankara na huduma muhimu. Huu ni mkopo wa haraka, wa kidijitali, na wa gharama nafuu ambao utawasaidia wateja wetu kukabiliana na changamoto za uhaba wa fedha,” amesema Adili.

Kwa muda mrefu, Benki ya CRDB imekuwa ikibuni huduma za aina tofauti zinazolenga kukidhi mahitaji ya wateja wake huku ikiwekeza nguvu katika matumizi ya teknolojia.

Katika jitihada hizo, mwaka 2017, ilizindua “salary advance,” mikopo inayowalenga wafanyakazi na watumishi wa umma inayotolewa hadi shilingi milioni 3 kwa riba ya asilimia 5 tu, na mwaka 2019 ikazindua “boom advance,” kwa ajili ya wanafunzi wa vyuo vikuu ikitolewa kuanzia shilingi 1,000 hadi shilingi 150,000 na kurejeshwa hadi kwa siku 60 tangu walipochukua mkopo.

Mwaka 2020 Benki ya CRDB ilitambulisha sokoni “pension advance,” mikopo mahsusi kwa ajili ya wastaafu wanaoruhusiwa kukopa kuanzia shilingi 5,000 hadi shilingi milioni 1.
 
ngoja nivute sasa hivi, maisha ni kiganjani, hakuna kuishi kinyonge tena.
 
Wananikera tu kutokulipa baadhi ya mawaka wao kwa wakati..sio siri hii bank kwa upande wa mawakala wwnawaonea mno..badhii hawawalipi na ushahidi..au sometimes meseji ya kamisheni inakuja haina kiwango..achilia mbali hivyo ukifuatilia tawini inaonekana muamala umewekwa kwenye acc ya wakala lakini kwa wakala haifiki yani ni mauza uza ...unajikuta unawafanyia wao kazi na hawakulipi..
Hata kwa issue ya mtandao ni hovyo...CRDB WANAKERA MNO MNO MNO LIPENI MAWAKALA PESA ZAO ZA KAMISHENI ACHENI WIZI
 
😋😋😋.kama hauna madeni wewe sio mwanaume kamili
 
🤣🤣🤣 na sisi ambao credit bureau wanasema hatukopesheki vipi?, maana tushaacha vilio vikampuni vyoote vya kukopesha
 
Hapo crdb mwaka 2018 nikiwa iringa nilipeleka wazo la kuanzisha boom advance na walilikubali mwaka uliofuata wakaanzisha, niliyempelekea ile proposal akaniminyia chinichini akajifanya wazo ni lake nikakausha.
 
Bongo hii ya kijinga unafanya ishu kama hizi bila ku mwanasheria
 
Hapo crdb mwaka 2018 nikiwa iringa nilipeleka wazo la kuanzisha boom advance na walilikubali mwaka uliofuata wakaanzisha, niliyempelekea ile proposal akaniminyia chinichini akajifanya wazo ni lake nikakausha.
Kumbe mambo haya yapo

Kuna wadau wawili nilisikia stori yao walikumbana na case kama hii, kwamba wazo la fiesta ni wao walimpelekea the late Ruge Mutahaba pale mawingu akawatoa 50k tu akachukua zake wazo lao akaliboresha mwamba akapiga hela za kushanta. Wadau walilalamika hadi keshokutwa.

Sijui ni kweli au ilikuwa chai.
 
Jina limekaa kimtego sana.
Jinasue kutoka wapi Kama huvutwi ukanase ?
 
Katika mpango wake wa kuongeza ujumuishaji wa wananchi kiuchumi, Benki ya CRDB imezindua huduma ya mikopo ya Jinasue inayowalenga wateja wake wote wenye uhitaji wa fedha.

Huduma hiyo iliyozinduliwa na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya CRDB, Stephen Adili itawaruhusu wateja wa benki wenye salio dogo kwenye akaunti zao kuliko muamala wanaotaka kuifanya au wateja wanaohitaji fedha kutokana na dharura walizonazo.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo, Adili amesema ujumuishi wa kifedha ni ajenda ya kimkakati ndani ya Benki ya CRDB inayoamini suala hilo ni msingi wa mapinduzi ya kiuchumi katika jamii yoyote.

“Tunayo mikopo inayowalenga baadhi ya wateja wetu kama vile watumishi, wanafunzi wa vyuo vikuu na wastaafu pamoja na wafanyabiashara. Tumegundua kuna watu ambao hawapo kwenye makundi hayo ambao wanahitaji uwezeshaji hivyo kuja na Jinasue, mikopo inayomlenga kila mteja wa benki yetu,” amesema Adili.
Mikopo hiyo, amesema itakuwa inatolewa kwa kushirikiana na kampuni ya CreditInfo na itatolewa kupitia SimBanking kuwawezesha wateja wetu kumudu gharama za huduma, bidhaa, na ankara mbalimbali wanapokuwa na changamoto za kifedha.

Kupitia SimBanking, wateja watapata mikopo ya Jinasue kwa urahisi kuanzia Shilingi 1,000 hadi Shilingi milioni 1 kwa riba ya asilimia 8 tu. Ili kupata mkopo huu, mteja anatakiwa kuwa anatumia akaunti ya Benki ya CRDB na amejiunga na huduma ya SimBanking.

“Mkopo wa Jinasue ni suluhisho muhimu kwa wateja wanapokabiliwa na changamoto za kifedha wakati wa kulipa ankara na huduma muhimu. Huu ni mkopo wa haraka, wa kidijitali, na wa gharama nafuu ambao utawasaidia wateja wetu kukabiliana na changamoto za uhaba wa fedha,” amesema Adili.

Kwa muda mrefu, Benki ya CRDB imekuwa ikibuni huduma za aina tofauti zinazolenga kukidhi mahitaji ya wateja wake huku ikiwekeza nguvu katika matumizi ya teknolojia.

Katika jitihada hizo, mwaka 2017, ilizindua “salary advance,” mikopo inayowalenga wafanyakazi na watumishi wa umma inayotolewa hadi shilingi milioni 3 kwa riba ya asilimia 5 tu, na mwaka 2019 ikazindua “boom advance,” kwa ajili ya wanafunzi wa vyuo vikuu ikitolewa kuanzia shilingi 1,000 hadi shilingi 150,000 na kurejeshwa hadi kwa siku 60 tangu walipochukua mkopo.

Mwaka 2020 Benki ya CRDB ilitambulisha sokoni “pension advance,” mikopo mahsusi kwa ajili ya wastaafu wanaoruhusiwa kukopa kuanzia shilingi 5,000 hadi shilingi milioni 1.
Jinasue kwenye shida kwa KUNASA ZAIDI kwenye mkopo wa benki
 
Back
Top Bottom