MeinKempf
JF-Expert Member
- Jun 11, 2013
- 11,094
- 7,225
Kufuatia mmiliki wa hotel kubwa iliyojengwa miaka michache iliyopita pande za Mwenge jijini Dar es salaam kushindwa kulipa mkopo wake wa mabilioni ya Pesa aliyokopa, benki hiyo imechukua hatua za kupiga mnada hotel hiyo kwa kutumia idihini halali ya mahakama baada ya mmiliki wake kushindwa kurejesha mkopo aliokuwa kakopa.
Pamoja na kupigwa mnada na hotel kununuliwa na kibopa mwingine, mmiliki wa awali wa hotel hiyo alishindwa kutoa taarifa za kueleweka kwa wanafunzi mbali mbali wa chuo na wapangaji wengine waliokuwa wakiishi katika jengo hilo, hali iliyopelekea kutolewa vitu vyao nje na kampuni ya madalali waliokuwa wamepewa kandarasi na mahakama.
-----------
My take: Hilo ni funzo kwetu kuwa mikopo bila mipango ni majanga matupu. Tujifunze sana kuwa mipango endelevu "sustainable planning" kwa mambo mbalimbali maana hilo hotel ukiliona kwa nje unaweza sema hivi mwenye nalo anajua hata kama kuna jero ya coin?? Maana ni ya kishua kinoma.