Bendera ya CCM inapeperushwa mbele ya ofisi ya Serikali, je ina tawi hapa Airport Songea?

Ngalikivembu

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
1,959
872
Wana JF salaam.Ningependa niwaulize wataalamu wetu juu ya suala hili ambalo limekuwa likijitokeza mara kadhaa hapa kiwanja cha ndege Songea.Bendera ya CCM inapeperushwa mbele ya ofisi hii kwenye jengo linaloitwa VIP ikiwa sambamba kabisa na bendera ya Taifa.Hili limekaeje jamani?Kwani ninafahamu siasa zimezuiliwa kwenye ofisi za umma na hata wafanyakazi wake wamezuiwa kufanya siasa eneo la kazi.Je hii bendera sio inaashilia siasa inafanyika hapa?Au kupeperusha bendera si tatizo?Meneja hafanyi siasa hapa kweli? Mwaka juzi tena wakati wa kampeni bendera hii ilikuwa inapeperushwa hapa hapa.Ilikuwa tarehe 10.10.2010 wakati Jakaya alipokuwa anafanya kampeni hapa Songea bendera hii ikawa inapepea.Au ndo tuseme kuna tawi hapa linaendeshwa kwenye majengo haya ya serikali?Kama nikiambiwa ni sahihi basi CDM nasi tutafanya mpango tuwe na tawi hapa.
 
Mwana ndo siasa ya magamba hiyo, huoni viwanja vya mipira walivyojimilikisha
 
Fanya kama Arumeru Mashariki ishushe halafu uipige moto na hawatakufanya lolote maana hutakuwa umevunja sheria bali unasimamia sheria
 
Asante FF kwa usahihishaji wako.Shina na tawi vyote vitakuwepo.Lakini unafurahia ujinga kwa kuitetea serikali yako.Huo si utaratibu wa kuheshimu sheria kama ilishakatazwa.
 
Huko mikoani **** shida kubwa sana na kila mtumishi anajifanya hajielewi wakumbuka walivyokuwa wanamsomea risala ya wilaya na mikoa salma???hawajui wajibu wao na kutochanganya siasa na serikali...??au wanajitoa akili wakidhani wanajilinda???waache kujitoa akili!!!!
 
Ikibidi watu kuingilia kati basi ni lazima ifanyike hivo.Bahati mbaya bendera hiyo sasa imeshushwa kabla ya saa kumi na mbili kufika imebakia ya Taifa tu.
 
Kama viongozi wa serikari wanashindwa kutofautisha siasa na kazi yao kwa nini nchi isifilisike . Badala ya kujenga nchi wao wanajenga CCM!!
 
inaashilia = inaashiria

Kwanini msiweke shina kabisa, tawi halitoshi.
wewe nawe! wewe hujui kama shina liko chini wakati tawi liko juu. Husikii watoto wa mjini wakikwambia "mimi niko matawi ya juu"? shina la nini bwana kama wataka kwenda juu!!?
 
Wana JF salaam.Ningependa niwaulize wataalamu wetu juu ya suala hili ambalo limekuwa likijitokeza mara kadhaa hapa kiwanja cha ndege Songea.Bendera ya CCM inapeperushwa mbele ya ofisi hii kwenye jengo linaloitwa VIP ikiwa sambamba kabisa na bendera ya Taifa.Hili limekaeje jamani?Kwani ninafahamu siasa zimezuiliwa kwenye ofisi za umma na hata wafanyakazi wake wamezuiwa kufanya siasa eneo la kazi.Je hii bendera sio inaashilia siasa inafanyika hapa?Au kupeperusha bendera si tatizo?Meneja hafanyi siasa hapa kweli? Mwaka juzi tena wakati wa kampeni bendera hii ilikuwa inapeperushwa hapa hapa.Ilikuwa tarehe 10.10.2010 wakati Jakaya alipokuwa anafanya kampeni hapa Songea bendera hii ikawa inapepea.Au ndo tuseme kuna tawi hapa linaendeshwa kwenye majengo haya ya serikali?Kama nikiambiwa ni sahihi basi CDM nasi tutafanya mpango tuwe na tawi hapa.
Usijiulize sana ishushe uichome kesi mbele kwa mbele hapo ilipo hairuhusiwi!!
 
uwezo mdogo wa kufikiri ndio huleta mada kama hizi
Ni nani mwenye uwezo mdogo wa kufikiri; wewe au mleta mada? sheria inasemaje kuhusu siasa katika ofisi za serikali? CHADEMA, CUF, TLP n.k. wakiamua pia kusimika za kwao katika kila ofisi watavumiliwa? Ukijibu haya utapambanua nani anayeongea pumba kati yako na mleta mada. Tatizo la viongozi wengi wa CCM bado wako katika giza la ndoto za "chama kushika hatamu" na ndiyo maana hadi leo wanashindwa kabisa kutofautisha shughuli za chama chao na zile za serikali zinazogharimiwa na kodi zetu sote, wana CCM na tusio.
 
uwezo mdogo wa kufikiri ndio huleta mada kama hizi
Tatizo linalokukabili ni kutokubali kukosolewa.... Na hili hili ni tatizo la asilimia kubwa ya wana-CCM, kuanzia mwenyekiti wa taifa hadi mwanachama. Si mnakumbuka yule mtoto aliyeuliza swali kule Mwanza... Kwa mtazamo wako, unataka kila chama cha siasa kilichosajiliwa kiweke bendera yake pale?
 
Ooh Mimi napenda shina! Mimi napenda Tawi.
Yote tisa.
Unapendwa mti na mzizi wake.
Bendera ya CCM katika Ofisi ya serikai ni Utovu wa nidhamu serikalini.
 
Back
Top Bottom