GuDume
JF-Expert Member
- Jan 18, 2015
- 6,651
- 14,314
Ben Saanane.
Habari za siku ndugu yangu?ni muda mrefu sana toka utoweke katika majukwaa yetu ya JF na mitandaoni kwa ujumla. Napenda tu kujua hali yako huko uliko. Bado utabaki kuwa ni Mtanzania mwenzetu. Tukiweka mbal itikadi za vyama,dini n.k
Najiuliza tu unasoma uzi huu ukiwa wapi? Ukiwa mbinguni? Kama upo huko basi naamini upo sehemu njema kabisa kuwepo. Na wala kwa huko sina tatizo nako kama umefanikiwa kufika usirud tena huku duniani. Bado kuna dhiki na mateso kama zaman tu. Watu wanaumwa ,wanafungwa, wanateswa, wanapata njaa, wanajiua,wanauawa na kila aina ya dhiki.
Najiuliza tena unasoma huu uzi ukiwa wapi? Jehanamu? Huko nafaham kwa habari za watumishi wa Mungu kuwa ni kubaya. Kuna mateso zaidi ya haya tunayoyapata hapa ambayo ni kama mazoezi tu mechi kamili tena ya fainali ni huko. Ntakupa pole tu. Hapo sina la kusema.
Najiuliza unasoma huu uzi ukiwa wapi?duniani tanzania sehem flan? Basi hata tuambie kama unapata muda wa kusoma magazeti, tuambie kama unaangalia tv na kusikiliza radio.tuambie kama unaingia JF unatumia ID gan. Nyosha tu mkono ndugu yangu utupungie huko uliko.halaf kaa endelea kufanya uyafanyayo.
Najiuliza unasoma huu uzi au unasomewa ukiwa wapi?kwenye chumba kimoja cha mateso.umefungwa kamba au pingu. Unakula kwa shida na mwli wako una majeraha. Halafu anakuja mtu mmoja ameshika simu anakwambia jamaa zako wanakukumbuka huko JF. Walikuwa wanakuona wewe kidume, wapo wapi sasa?upo peke yako.umechoka.tulikwambia sisi ukadhan utatuweza. Tuna mikono mirefu. Halaf anakusomea uzi huu. Unainamisha kichwa chini ukiwaza wana JF wamekuacha,wamekusahau n.k
Najiuliza unasoma huu uzi ukiwa wapi?nchi flan umetulia hutak tena shida na misukosuko ya tanzania?uliambiwa usijihusishe tena na siasa za tz?unatusoma JF halafu unatabasam au kutikisa kichwa. Unaenda kwenye jokofu unachukua kinywaj unakaa unawasha TV unacheck movie au taarifa ya habari?
Najiuliza unasoma huu uzinukiwa wapi? Ardhini tu. Ardhin hapa hapa tanzania umezikwa ukiwa hujulikani ka ndo wewe maana mwili wako haujatambuliwa. Basi wakati unazikwa ungesema "mimi ndo ben saanane msiendelee kunitafuta" ungesema kw sauti kuepusha maneno mengine yasiendelee.
Kwa sasa ben issue kubwa nadhan umeshaifaham kwa tanzania. Ni series mpya inaitwa drug list. Hii imeishia episode ya tatu na producer ameamua kuifanya iwe reality show. Kwa week kama mbili hivi ilikuwa ndo habari ya mjini. Episode ya tatu sterling anapalalaiz na hatimaye anatokea sterling mwingine ambaye yeye anakuja na mikakati mipya. Producer aligundua kuwa series ile mwisho wake ungekuwa mbaya hivyo anaamua kwa makusudi kumpalalaizi sterling wa kichina aliyekuwa na uwezo mpaka wa kupaa au kukaa hewani. Ameleta sterling mwingine aendeleze story. Hatujajua itaendeleaje.
Tumeumia sana wengine kwa kukosa series hii na wengine tumefarijika kutokana na kuwa tulikuwa tukiishi kwa mashaka sana maana kwa uwezo aliokuwa amepewa sterling kama uliwah gombana naye angepata nafas ya kukulipizia.
Ben Saanane kama binadamu inawezekana kuna uliyotukosea au kosea watu wengine. Tusameheane kama binadamu. Angalau basi tupe tu salama ndugu yetu toka huko uliko. Sema neno moja tu nasi tupate ridhika.