Naomba nijaribu kuelimisha kidogo, kiwanja kilichopimwa kwa mil 3.5 hii ni ngumu kupata kwa uzoefu wangu. Thamani ya mita moja ya mraba kwasasa inapatikana sio chini ya 15000 itawezekanaje upate kiwanja kwa hela hyo, otherwise kuna mambo mawili yanayofanyika kitaalam, kuna demarcation na survey nafikiria namna ya kuyaweka haya maneno yapate kueleweka, kuna viwanja vilivyofanyiwa demarcation kwa maana mtaalam wa mambo ya survey ametumia machine(total station) kisha akaweka alama kutokana na mchoro wa mpango mji wa eneo husika lakin kitaalam anaishia hapo na anaweza kutengeza pia mchoro kabisa hii watu wanaita upimaji ila kimsingi ni aina ya upimaji ambao haujakamilika yaan hautofautiani sana na wale wanaopima hatua za miguu 20*20 otherwise ukisikia mahali pamepimwa basi ujue kunakuwa approved survey ya maeneo husika kutoka wizara ya ardhi na iwe huru kwa mtanzania yeyote kuifikia akitaka, ninajua hilo eneo linalouzwa hyo mil 3.5limefanyiwa demarcation na sio survey, ninatambua lipo eneo mitaa ya bunju linauzwa viwanja kwa kila sqm 12, 000/=jaribu hapo mkuu unaweza kupata unachohitaj, plan namba ya hilo eneo ni E'301/1048 imepata usajili 10/10/2013 pia nakupa angalizo mchakato wa kupata hati pia unawasumbua hawa wenye kumiliki hii property nakushaur uwaambie wakupe necessary documents ukashughulikie mwenye. Nakutakia mafanikio mema