Bei ya zao la fiwi kutopanda nini tatizo

Bei ya zao la fiwi kutopanda nini tatizo

bullion

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2014
Posts
309
Reaction score
112
Wakuu poleni na mihangaiko,

Kuna jamaa zangu kadhaa mwaka huu wamelima zao la fiwi huko maeneo ya upareni, kama kilimo cha biashara. Zao hili ni moja ya mazao ya biashara yanayolimwa maeneo hayo, na soko lake kubwa ni nchini kenya. Kwa bahati mbaya kipindi cha mavuno, kenya walikuwa na sintofahamu ya uchaguzi, kuliko pelekea bei ya zao sokoni kutokuwa nzuri kama kipindi cha mwaka jana. Mwaka jana bei ilikuwa nzuri, na wakulima walinufaika kwa kulima zao hilo, kama mojawapo ya kujikwamua kiuchumi. Bahati mbaya bei bado haijawa nzuri japokuwa uchaguzi nchini Kenya umepita salama. Je hii inasababishwa na walanguzi, au ni kwamba mwaka huu Kenya hawahitaji fiwi.

Mwenye kujua hili anaweza saidia mawazo, maana zao hili ndilo mkombozi wa maeneo hayo, na jamaa zangu wanalitegemea kusomesha, kujenga, na pia mtaji wa kulima hasa kipindi hiki cha kulima mahindi


Nawasilisha
 
Weka picha, fiwi sijui ni nini
upload_2017-12-18_13-10-17.jpeg
 
upload_2017-12-18_13-12-36.png

Ya katika, sema nyeusi ndio ina soko zaidi, ndio ya kibiashara
 
Fiwi au Wifi?? hilo ni jina la kipare au kiswahili?
 
Fiwi???

Ndio nasikia leo aisee, inatumika kufanyia nn mkuu?
 
Yanapatikana wapi haya, yanapikwa kama maharage au yana kaangwa.

Sijawahi kuyaona, je yana ladha nzuri?.
Ladha inategemea na mtu na mtu. Inatumika kama mboga zingine za jamii ya kunde. Sijui kwa nini kwa Kenya inapendwa zaidi katika kila aina ya sherehe hasa za watu wanaojiweza ndio zaidi
 
Ladha inategemea na mtu na mtu. Inatumika kama mboga zingine za jamii ya kunde. Sijui kwa nini kwa Kenya inapendwa zaidi katika kila aina ya sherehe hasa za watu wanaojiweza ndio zaidi
Labda zinaongeza zile nguvu zetu pendwa
 
Lile katazo la kusafirisha mazao nje lilituaffect sana wakulima wa fiwi au ngwara aka lablab beans....mie nimevuna October ebu ngoja kwanza tusubiri demand iongezeke sokoni tuyauze,ila mnadani nasikia yanauzwa kuanzia laki hadi laki na nusu kwa gunia! Nyie upareni mnauza bei gani kwa gunia.
 
Manasa E="charty, post: 24907212, member: 179294"]Lile katazo la kusafirisha mazao nje lilituaffect sana wakulima wa fiwi au ngwara aka lablab beans....mie nimevuna October ebu ngoja kwanza tusubiri demand iongezeke sokoni tuyauze,ila mnadani nasikia yanauzwa kuanzia laki hadi laki na nusu kwa gunia! Nyie upareni mnauza bei gani kwa gunia.[/QUOTE]
Mnada WA wapi huo.
 
Back
Top Bottom