Bei ya unga wa ugali gharama kuliko hisa za Vodacom

mapessa

JF-Expert Member
Oct 9, 2014
663
1,165
Bei hii ya hisa ilifikiwa baada ya wakurugenzi wa Vodacom kuafikiana pamoja na mshauri mkuu kwa kuangalia baadhi ya mambo kadhaa mfano;

•Muonekano na Mwelekeo wa uchumi wa Tanzania.

•Utendaji wa kifedha wa kampuni pamoja na matarajio ya kampuni.

•Ulinganifu wa thamani za hisa za kampuni zinazofana na kampuni ya Vodacom kwenye masoko ya hisa ya Bara la Afrika kabla ya kuwekwa kwa bei kamili ya kila thamani ya hisa moja.


•Matarajio ya mtiririko wa fedha wa kampuni hiyo kwa lugha ya kiuchumi tunasema (Discounted Cash Flow)
Tathmini ya kampuni imeangalia kwa kiasi hali ya kina ya kibiashara yakampuni ambapo Wakurugenzi wenyewe wanaamini ilihusisha utendaji wa hivi karibuni, na rasilimali ambazo kampuni ya Vodacom imewekeza kuwa itawezekana kabisa kuyafikia malengo.

Vile vile zipo njia kadhaa za kutathmini (Valuation Methodologies) katika kufikia hitimisho hili la bei.

Njia hizo ni pamoja na kufanya ulinganifu (comparative analysis) na kampuni nyingine za mawasiliano katika Bara la Afrika, kwa ukaribu zaidi nchi kama Kenya na Afrika ya Kusini, kutokana hapa nyumbani (Tanzania) hakuna kampuni inayofanana na Vodacom ambayo imeorodhesha hisa zake sokoni.

Katika kufanya ulinganifu huo, kampuni huzingatia kufanya marekebisho ya tathmini kwa kuangalia mambo kama utofauti wa ukubwa wa Soko, Idadi ya watu na tofauti za kiuchumi (Kifedha)

Baada tathimini hatua iliyofuata ili kupata bei kamili unafanyika mchanganuo wa uhusiano (Regression Analysis) siku zote ni kati ya ukuaji wa mapato na viashiria vya biashara ili kuweza kupata thamani za hisa.

Kwa kutumia njia ya Discounted Cash Flow analysis unaweza kupata matokeo ya tathmini yanayoendana na ulinganifu wa makampuni kwa njia ya viashiria vya kibiashara .

Mwisho thamani ya jumla ya wanahisa inayopatikana kwenye tathmini hugawanywa kwa idadi ya hisa zote na kupata thamani ya kila hisa ndiyo sababu kila Hisa moja ya Vodacom inauzwa kwa shilingi 850.

Kama Voda wameweza kufanya tathimini ya kupanga bei ya hisa, kwanini serikali isipange bei ya unga wa. Ugali Watanzania mmepewa nafasi ya kuwekeza haya itumieni sasa.
 
Back
Top Bottom