benja
JF-Expert Member
- May 10, 2011
- 319
- 213
Bei ya mfuko mmoja wa sukari wa kilo 25 kwa sasa ni Tsh 48,000/- mpaka 50,000/- halafu serikali kupitia bodi yake ya sukari wanasema tuuze sukari kwa bei ya Tsh 1,800/- kwa kilo. Hivi wewe Mkurugezi wa Bodi na watu wako kweli mmekaa kabisa mkaamua kumkandamiza muuzaji wa hii bidhaa. Haiitaji Degree ya PhD kujua kwamba Tsh 1,800*25kg =45,000/- na hivyo mfanyabiashara atapata loss/hasara.
Ushauri: Nilidhani mngekaa chini na kufanya utafiti na kujua wapi kuna tatizo, wapi sukari inayotengenezwa/inayozalishwa na viwanda vya ndani inakwenda. baada ya hapo mngejua tatizo mlitatue tatizo na ndipo mtaweza kuregulate bei ya sukari. Nitoe mfano mzuri wa wenzetu wa sekta ya mafuta. Kabla, bei ya mafuta ilikua kila mmoja anajipangia bei yake kama anavyoona. Hii kwa kiasi kikubwa ilichangiwa na kila mwenye kutaka kuagiza mafuta alikuwa na uwezo wa kufanya hivyo. Ila serikali ilikaa na watu wenye akili na kuweza kuweka utaratibu wa bulk procurement system kwamba sio tu kila mwenye pesa aagize kivyake bali sasa kila mwenye kutaka kuagiza mafuta wataagiza kwa pamoja na mafuta yatakuja kwa pamoja (in bulk). Hii inasaidia katika ku - control bei ya mafuta na ndio kitu wanachokifanya ewura na regulatory authority zingine duniani. Nawashangaa nyie Bodi ya Sukari.........mnakurupuka kwenye press conference!!!! shame shame shame on you!!!!