Donatila
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 8,273
- 25,297
Akitangaza ongezeko hilo kwa waandishi wa habari, Kaimu Mkurugenzi huduma kwa wateja, wa mamlaka hiyo, Mussa Ramadhan Haji, alisema mafuta ya dizeli yameshuka kwa Sh. 90 kwa lita kutoka Sh. 2,280 mwezi Novemba hadi Sh. 2,190.
Aidha, alisema kwa mafuta ya taa bei imepanda kwa Sh. 80 kwa lita kutoka Sh. 1,539 hadi Sh. 1,619 sawa na ongezeko la asilimia 4.9.
Mafuta ya ndege, yameshuka kwa Shilingi 90 kutoka Sh. 2,122 kwa lita hadi Sh. 2,032 sawa na ongezeko la asilimia 4.4.
Hata hivyo, alisema ZURA inatoa bei za mafuta kila mwezi kwa kuzingatia vigezo maalumu ikiwamo wastani wa mwenendo wa mabadiliko ya bei za mafuta duniani, thamani ya shilingi ya Tanzania, gharama za usafiri, bima na usafirishaji kutoka nje hadi Zanzibar, kodi za serikali na kiwango cha faida kwa wauzaji wa jumla na reja reja.
Alisema bei zilizotangazwa na serikali ndio halali na kuwasisitiza wananchi kununua mafuta katika vituo halali ili kuepuka kuuziwa mafuta yasiyo na viwango.
Chanzo: Nipashe