Bei ya mafuta ya gari yazidi kuporomoka kwenye soko la dunia

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
28,701
71,034
Wakuu habari za leo,

Bei ya mafuta ya gari(Brent crude oil) kwenye soko la dunia leo imezidi kuporomoko na kufikia dola 36.05 per berrel, wataalamu wa mambo ya uchumi wa mafuta duniani wanasema huenda bei hiyo ikazidi kuporomoka, hii inatokana na teknolojia ya kisasa ya gharama nafuu inayotumika kwa sasa kuchimba mafuta, wataalamu hao wameendelea kusema kuwa endapo baadhi ya mataifa yenye mafuta yanayopigana vita kama libya, iraq, syria na yemeni yatapata amani, basi huenda bei ya mafuta ikaporomoka zaidi, na endapo Iran na urusi zitaodolewa vikwazo basi bei ya mafuta inaweza kuwa ya chini kabisa kuwahi kutokea katika miaka ya hivi karibuni.
Source: BBC

Swali la kujiuliza mbona wananchi wa sehemu zingine duniani wanafurahia na wanapata unafuu wa maisha wakati hapa kwetu Tanzania maisha ndiyo yanazidi kuwa magumu?
 
Wao ndo wanamiliki masheli na wana mahisa ktk makampuni ya mafuta hapa Bongo. Mimi naamini kabisa kuna viongozi wana LAANA kutoka kwa Wananchi.
 
Basi waondolewe vikwazo hao urusi na iran habari njema hii Jibu la swali lako ni hili;Kwa utawala wa awamu ya tano wananchi hawatalia ikiwa habari hizi ni za uhakika
 
mimi bado naaamini bei ya mafuta hapa bongo ilipaswa iwe hata 1000 kwa lita moja....kuna hujuma kubwa sana kwenye process ya mafuta pale bandarini....sijaelewa bado kwa nn Magufuli amekaa kimya juu ya hili ilhali linagusa maisha yetu ya kila siku kwa karibu sana...pls Magufuli do the needful
 
Ni ngumu kuona unafuu kwa sababu pesa yetu inazidi kushuka thamani dhidi ya sarafu ya dola. Pengine shilingi ikiweza kuimarika na serikali kupunguza kodi kwenye mafuta basi tutaona unafuu
 
Mafuta ndio kila kitu hakika yakishuka na jamaa akizi kuwabana wezi,akarekebisha ada shule binafsi na kusimamia swala zima la afya at least idadi kubwa ya wanyonge wapate bima ya afya baada ya miaka 5 tutakua tumepumua sana
 
Cha ajabu hapa bongo mafuta hayashuki tu.., alafu EWURA wanakenua mimeno tu as if hawajui kinachoendelea duniani. mi naona ni vema na wao wakatumbuliwa tu.., hawana wanachofanya. mafuta hayakupaswa kuzidi 1,500/- kwa liter.
 
wakuu habari za leo,

bei ya mafuta ya gari(brent crude oil) kwenye soko la dunia leo imezidi kuporomoko na kufikia dola 36.05 per berrel, wataalamu wa mambo ya uchumi wa mafuta duniani wanasema huenda bei hiyo ikazidi kuporomoka, hii inatokana na teknolojia ya kisasa ya gharama nafuu inayotumika kwa sasa kuchimba mafuta, wataalamu hao wameendelea kusema kuwa endapo baadhi ya mataifa yenye mafuta yanayopigana vita kama libya, iraq, syria na yemeni yatapata amani, basi huenda bei ya mafuta ikaporomoka zaidi, na endapo iran na urusi zitaodolewa vikwazo basi bei ya mafuta inaweza kuwa ya chini kabisa kuwahi kutokea katika miaka ya hivi karibuni.
Source: Bbc

swali la kujiuliza mbona wananchi wa sehemu zingine duniani wanafurahia na wanapata unafuu wa maisha wakati hapa kwetu tanzania maisha ndiyo yanazidi kuwa magumu?

mkuu. Hapa ndipo kwenye vidonda ngugu, siyo majipu tena. Magufuli baba njoo huku kwenye nishati kumejaa udalali mkubwa. Kamua wote wananchi tupone.
 
Kushuka bei ya mafuta ni maksudi tu hili kupunguza kasi ya urusi na Iran. Ikumbukwe uchumi waw urusi na irani ulikuwa unakuja juu sana kwasabab ya mafuta na gesi.

Ni mchezo mzuri sana kati ya Marekan na Saudi Arabia wakiamrishwa na Israel kumdhoofisha Mrus na muiran.

Ikumbukwe Saudi Arabia yuko radhi kuwa marafik na muisrael kuliko ndugu yake katika iman mshia Iran hawa ni maadui wakubwa sana.

Ila benki ya dunia imewaonya wasaudia wachukue hatua za haraka sana sasa hiv za kubana matumiz lasivyo baada ya miaka mi5 wataingia keen ye austerity.
 
Mkuu asante sana nimeipenda Comment yako
 
Afadhali ishuke bana nianze kuwasha AC kwenye gari maana hili joto la mji huu ni balaa.
 
mkuu. Hapa ndipo kwenye vidonda ngugu, siyo majipu tena. Magufuli baba njoo huku kwenye nishati kumejaa udalali mkubwa. Kamua wote wananchi tupone.
Mkuu hapa Magufuli anatakiwa kufanya upasuaji wa kuondoa kansa sio kukamua
 
Kushuka bei ya mafuta ni maksudi tu hili kupunguza kasi ya urusi na Iran. Ikumbukwe uchumi waw urusi na irani ulikuwa unakuja juu sana kwasabab ya mafuta na gesi.

Ni mchezo mzuri sana kati ya Marekan na Saudi Arabia wakiamrishwa na Israel kumdhoofisha Mrus na muiran.

Ikumbukwe Saudi Arabia yuko radhi kuwa marafik na muisrael kuliko ndugu yake katika iman mshia Iran hawa ni maadui wakubwa sana.

Ila benki ya dunia imewaonya wasaudia wachukue hatua za haraka sana sasa hiv za kubana matumiz lasivyo baada ya miaka mi5 wataingia keen ye austerity.
Vita ya panzi, furaha kwa kunguru. Acha wao wagombane ili sisi tuneemeke. Hata USA alineemeka wakati wa vita ya pili ya dunia. Cha msingi tukitakacho wananchi ni mafuta kushuka bei tuu.
 
Back
Top Bottom