Na Mbusule Shillu,
Kwa muda sasa nimekuwa nikidadisi kuhusu kutofautiana kwa Bei za Mafuta kati ya Kampuni moja ya Mafuta na nyingine au hata Kampuni hiyo hiyo moja kwenye maeneo au barabara tofauti ndani ya mji mmoja.
Leo nitazungumzia Bei ya Petrol katika Jiji la Dar-Es-Salaam ambayo Bei elekezi ya Serikali mpaka sasa ni Tsh. 2510 kwa Lita. Hata hivyo, makampuni yanayoitikia Bei hiyo ni machache sana hapa Dar-Es-Salaam kama Total, Puma na Oryx. Makampuni Mengine makubwa karibu yote Bei zake zimekuwa zikinyumbulika kimaeneo.
Mathalani, Kampuni kubwa la Lake mpaka leo 31.12.2021 huko Bunju linauza mafuta ya Petrol kwa Tsh. 2459/- tu. Sehemu zingine; Sinza Tsh. 2460, Goba 2460, Mbagala 2470, Kamata 2500, Posta 2500, Temeke 2470, Tabata 2470, Kinyerezi 2480 na External 2490 na Victoria 2470.
Makampuni Mengine ni Meru ambalo huko Kinyerezi linauza mafuta kwa Tsh. 2490/- sawa na Kampuni la ATN Mahalia.
Mnyumbuliko huo wa Bei upo hivyo hivyo kwa Makampuni kama Camel, Ester Oil, Oilcom na Olympic.
Nilijaribu kuuliza swali kuhusu mnyumbuliko huo wa Bei lakini niliambulia majibu mepesi sana. Hoja yangu hapa; Je, kama Tshs. 2,459/- inalipa, kwa nini Serikali ilitangaza Bei elekezi ya kuumiza Wananchi? Kwa nini Serikali ifanye makampuni ya mafuta kutengeneze super profit on the expense of the poor majority?
Mwisho nataka kujua kutoka kwako msomaji, hili la mafuta ya Petrol kuwa na utambulisho tofauti tofauti kama Unleaded, Petrol na Super, humaanisha nini haswa?
Nawatakia mwaka mpya wenye KHERI na mafanikio tele..
.....