Bei Elekezi za viwanja/ardhi

Masanja

JF-Expert Member
Aug 1, 2007
4,820
8,886
Jamani hii attachment inaonyesha bei elekezi za viwanja sehemu mbali mbali za Tanzania. Kwa hiyo wale waliozoea kuuza viwanja kwa bei wanazozijua wao, nadhani huu utakuwa muarobaini wao.

Naona ni mwanzo mzuri kama angalau serikali inaweka bei elekezi. Maana bei ya Ardhi ilikuwa imefika pabaya sana especially DSM. Naamini hii itasaidia pia kupanga kodi sahihi za majengo (property tax).

NB: Kama hii habari ilikuwa imeshawekwa humu, naomba Mod muunganishe uzi huu na uzi husika. Nimeweka tuu for information watu wajue.
 
Attachments

  • VIWANGO_ELEKEZI_VYA_BEI_YA_SOKO_LA_ARDHI__2016(2).pdf
    957.9 KB · Views: 1,464
Nashangaa watu hawajaja humu, hii thread muhimu kwa kila mtu..
Hawajaielewa kama mimi. Hyo bei waliyoweka wakaandika kwa mita mraba. Ina maana kwa kila m^2bei ndo hiyo?

Mfano mbagala wameandika 30,000 mpka 50,000 ina maana kwa sqm 1 au?
Nieleweshe tafadhali
 
Jamani hii attachment inaonyesha bei elekezi za viwanja sehemu mbali mbali za Tanzania. Kwa hiyo wale waliozoea kuuza viwanja kwa bei wanazozijua wao, nadhani huu utakuwa muarobaini wao.

Naona ni mwanzo mzuri kama angalau serikali inaweka bei elekezi. Maana bei ya Ardhi ilikuwa imefika pabaya sana especially DSM. Naamini hii itasaidia pia kupanga kodi sahihi za majengo (property tax).

NB: Kama hii habari ilikuwa imeshawekwa humu, naomba Mod muunganishe uzi huu na uzi husika. Nimeweka tuu for information watu wajue.
Umefanya jambo jema sana ku_post hii kitu mkuu
 
Hawajaielewa kama mimi. Hyo bei waliyoweka wakaandika kwa mita mraba. Ina maana kwa kila m^2bei ndo hiyo? Mfano mbagala wameandika 30,000 mpka 50,000 ina maana kwa sqm 1 au?
Nieleweshe tafadhali[/QUOTE
Ndio ndugu, bei zote uzionazo ni kwa square meter moja, kama kiwanja chako ni 900m2 basi wazidisha kwa 900, au kama ni 500m2 wazidisha wa bei iliyowekwa, nafikiri umeipata hiyo..
 
We Masanja umesepa tena
hahaha Mkuu mimi nilipata mahali nikaona niiweke hapa na wenzangu wana-JF waione. Mimi siyo mtaalamu wa haya mambo. Ingawa Kiukweli TZ tulikuwa tumefika pabaya sana. Mtu anakwambia bei ya kiwanja..gharama ambayo hata ungefanya nini huwezi kuimudu.
 
Hii si kweli kuu maana hata waliotuuzia hivi karibuni dodoma wao wenyewe ni zaid ya hii
Screenshot_20180811-113904.jpg
 
Hawajaielewa kama mimi. Hyo bei waliyoweka wakaandika kwa mita mraba. Ina maana kwa kila m^2bei ndo hiyo?

Mfano mbagala wameandika 30,000 mpka 50,000 ina maana kwa sqm 1 au?
Nieleweshe tafadhali

Document inajieleza vya kutosha.
 
Bei elekezi kazi yake ni kwa matumizi ya wathaminishaji kuthaminisha thamani ya ardhi. Thamani ya mthaminishaji ndo inatumika na serikali kutoza kodi kwenye mauzo ya ardhi na kulipa fidia ikitwaa ardhi.

Haimaanishi kwamba ukiwa na ardhi lazima uuze kwa bei hizi elekezi, au kwamba ukienda kununua ardhi ung'ang'anie kuuziwa kwa bei elekezi. Wamiliki na wanunuzi mna uhuru wa kuelewana bei, ila bei ikishuka chini ya bei-elekezi, serikali itapiga hesabu zake na kuwapandishia thamani ya ardhi kwa ajili ya makadirio ya kodi. Ila haitawalazimisha mlipane bei elekezi ya serikali.

Mkiuziana kwa zaidi ya bei-elekezi serikali yenyewe itafurahi zaidi maana itakusanya kodi kubwa. Haitashusha bei kuja kwenye elekezi.

Nadhani naeleweka hapo. Kwa mliowahi kuagiza magari kutoka Japan mtakuwa mshakutana na mambo ya bei-elekezi pale TRA.
 
Je Bei elkezi hizi za tangu mwaka 2016 mpaka leo miaka 6 imepita.. Naomba kujua nyingine zinatoka lini??
 
Back
Top Bottom