Nyakageni,
Inaelekea hujasoma michango yangu...
Hebu isome kwanza.
Ni vyema kabla ya kuchangia ikawa unajua wengine wamesema nini.
Sibonike,
Hujafikia makamu ya kufanya mnakasha na mimi. Toka mwanzo nilijua hutofika mbali.
Katika yote niliyokuwekea hapo mchango wako ndiyo huo? Basi nimekuwia radhi.
Ilitakiwa ujipime kwanza kabla.
Hiyo paper, "Tanzania a Country Without Heroes," niliitoa Nairobi kwenye kongamano la kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wa nchi za
Afrika ya Mashariki.
Watayarishaji walikuwa IFRA French Institute for Research in Africa /BIEA British Institute in East Africa.
Hawa jamaa ndiyo walionialika na kutoka Tanzania nilikuwa peke yangu.
Hili peke yake ingekujulisha moto wa maji unayotaka kuoga.
Pili paper yangu aliyepiga "critique," ni profesa. Sasa wewe hapa unaingiaje?
Hata ujanja huo huna?
Hata historia aliyokuja nayo profesa si wengi tulipatamo kuisikia.
Tulipaswa kuisikia toka kwako ila wewe hukuambatanisha hicho kipande cha historia. Swali ni kwanini wewe hukuielezea? Were you biased? Sababu profesa haonyeshi kama kukupinga direct, ameongezea vitu ambavyo tulipaswa visoma toka kwako wewe muanzilishi wa hizi mada.
Haina shida nani alianza kuandika;...........
Umepotosha historia kwa kiwango kikubwa, . Unataka watu tuamini masimulizi hayo kwa sababu tu wewe umesema ukitumia kurunzi ya dini kutulazimisha kuona. Bahati mbaya wapo ambao wamekubali haya kwa sababu kutokubali kungewafanya wapoteze umoja ambao wanaamini unausimamia; umoja ambao msingi wake ni dini.
Mtu yeyote ambaye ataamua kukusoma kwa ukosoaji yakinifu kwa hakika atafikia mahitimisho hayo hayo aliyofikia Profesa na labda zaidi.
Prof Karim Hirji kanifurahisha aliposema wakati tunaandaa mitaala yetu UDSM kitengo cha Historia kilikuwa at its best in Africa! Tumepata uhuru wenye degree walikuwa wachache
Akapiga msumari kuwa
"Mohamed Said's claims are . . . . . . . . . EXTREME"
HUYU MZEE NI EXTREMIST
There are many more people who can narrate a similar type of suffering under different circumstances. Your story does not tell us why the students managed to pass with Division One at O level. Was it because they were Christians or were taught in Islamic schools and the the headmaster was a Muslim? This person has decided to analyse everything using the lens of religion. Some students could analyse using the lens of witchcraft, gender, tribalism, political affiliation, etc. I went to school with some people who blamed their failure in school and life on someone else but nothing about themselves.
This person goes on to perform badly in life after school apparently because he was in a Mfumo Kristo. But there are many Christians who have a similar experience, whom should they blame? There are many Muslims who have done very well, what happened?
As for Prof. Njozi, I know what he stands for. He is a person I have interacted with many times but not in religious discussions. The government gave him to head the Morogoro Muslim University but my dear friend turned it into a Madrasa, again reflecting who he is.
Mzee Mohamed Said, naona hata wafuasi wako humu wamekimbia! Nakupa ushauri kuhusu swala la prof Karim Hirji
MTU MZIMA AKIVULIWA NGUO HUCHUTAMA
Hao ndio wengine wenye mtazamo kama wa kwako. Kila kitu kinaangaliwa kwenye kurunzi ya kidini. Hivi Nyerere asingetaifisha shule za mission ili kila mtu bila kujali dini yake asome, hali ingekuwaje leo?
KVM
"Lakini tuende kielimu. Ninayo ripoti ya mwaka huu. Waliofanya mtihani wa darasa la saba kuingia darasa la tisa, asilimia 71 Waislamu. Asilimia 29 ni wengine. Walioshinda katika wale asilimia 71 ni asilimia 21. Katika wale 29 walioshinda tena sema mwenyewe. Katika asilimia 29 waliokwenda shuleni ni asilimia 79.
Katika asilimia 71 waliokwenda darasa la tisa ni asilimia 21. Sasa kuna moja, ama Waislamu wajinga ama akili yao haifanyi kazi, ama mtu ukiwa Muislamu wewe huna kitu, ama kuna kitu. Sasa namwomba Waziri anayehusika, anaposema aseme ya kwamba kwa hali ilivyo Waislamu wameumbwa wajinga. Au kwa hali ilivyo kuna sababu kadha, kadha.
Mwalimu Nyerere alisema zamani ifanywe bidii ya kuwanyanyua waliokuwa chini. Sasa bidii hii siyo ya kuwanyanyua waliokuwa chini. Bidii hii ni ya kuwakandamiza waliokuwa chini."
(Hotuba ya Kitwana Kondo Bungeni, 1999)
Hata historia aliyokuja nayo profesa si wengi tulipatamo kuisikia.
Tulipaswa kuisikia toka kwako ila wewe hukuambatanisha hicho kipande cha historia. Swali ni kwanini wewe hukuielezea? Were you biased? Sababu profesa haonyeshi kama kukupinga direct, ameongezea vitu ambavyo tulipaswa visoma toka kwako wewe muanzilishi wa hizi mada.
KVM
"Lakini tuende kielimu. Ninayo ripoti ya mwaka huu. Waliofanya mtihani wa darasa la saba kuingia darasa la tisa, asilimia 71 Waislamu. Asilimia 29 ni wengine. Walioshinda katika wale asilimia 71 ni asilimia 21. Katika wale 29 walioshinda tena sema mwenyewe. Katika asilimia 29 waliokwenda shuleni ni asilimia 79.
Katika asilimia 71 waliokwenda darasa la tisa ni asilimia 21. Sasa kuna moja, ama Waislamu wajinga ama akili yao haifanyi kazi, ama mtu ukiwa Muislamu wewe huna kitu, ama kuna kitu. Sasa namwomba Waziri anayehusika, anaposema aseme ya kwamba kwa hali ilivyo Waislamu wameumbwa wajinga.
Nadhani hapa unamnukuru Kitwana Kondo mwaka 1999. Kama ilikuwa kweli basi sidhani kuwa mambo yatakuwa yamebadilika hadi leo.
Kwa kweli imani yako imefunika kila kitu unabakia tu kuamini chochote kile mradi tu kielezee mambo ya kuonewa kwa waislamu. Hata kama kimetungwa. Hivi kweli unaamini kuwa wanafunzi waliofanya mtihani darasa la 7 mwaka 1999 walikuwa asilimia 71 ni waislamu na asilimia 29 ni wakristo? Ukifanya hesabu za haraka haraka tu utaona kuwa waislamu Tanzania bara wapo kwa asilimia kubwa mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani na Tanga. Mikoa ya DSM, Tabora, na Kigoma ni mchanganyiko. Mikoa iliyobakia wakristo ni wengi kwa mbali sana.
Na hawa hapa ni wa Dar es Salaam.I doubt the authenticity of your data au guru wako uliyem quote, kwanza umejuaje waislam na wakristo waliomaliza darasa la saba? Hakuna form inayoonesha dini, TSM9 haziandiki dini na pia ni siri
pili, hebu fanya na utafiti kuhusu matatizo ya wanafunzi hapa Dar hasa yanayotokana na kutengana kwa wazazi hivyo kuingia kwenye ngono at teen age
Sibonike,
Usiwe na haraka ya kutoa hukumu.
Mjadala ndiyo kwanza unaanza.
Ila nitakudokeza moja tu.
Prof. Hirji awe kama atakavyokuwa.
Hakubeba mzigo waliobeba Waislam katika ukoloni toka Wajerumani
hadi Waingereza.
Ukitaka kujua mtoto yatima anahisi vipi kufiwa na wazazi wake wawili
muulize mwenyewe.
"mwanangu siku ya Iddi watoto wenzako wamevaa nguo
mpya wamenunuliwa na baba zao wewe huna umejikunyata kibarazani
na matambaa?"
Jibu lake litakusogeza kwenye ukweli na uhakika.
Prof. Shivji hajapita tulipopita sisi.
Atazungumza na shingo kutoa kwa kuwa hana hata uzoefu wa mtoto
wa shangazi yake katika haya Waislam wanayolalamika.
Suali moja nitapenda Prof. Hirji anijibu.
Upungufu katika historia ya Tanganyika aliujua lini?
Aliujua kabla au baada ya Mohamed Said kuusema?
Ikiwa aliujua kabla kipi kilimfanya akae kimya siku zote hizi?
Uoga au kitu gani?
Tatizo la Said ni kuamini kuwa yeye pekee yuko sahihi na alichokiandika kana kwamba anachokihubiria wengine hawawezi kukijua. Afahamu kuwa kulikuwa na watu wengi walioshiriki ukombozi wa nchi hii wakiwa na watoto na wajukuu wanaokumbuka historia