BBC Swahili katika mobile | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

BBC Swahili katika mobile

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by geek, Nov 4, 2009.

 1. g

  geek Member

  #1
  Nov 4, 2009
  Joined: Feb 12, 2009
  Messages: 85
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tunapenda kuwakumbusha wasomaji na wasikilizaji wetu kuwa habari kutoka Idhaa ya Kiswahili ya BBC zinapatikana kupitia wavuti maalum kwa ajili ya simu za mkononi.

  Huduma hii mpya inawawezesha watumiaji wa simu za mkononi kusoma taarifa za kila siku moja kwa moja katika simu zao badala ya kutumia kompyuta. Hata hivyo ieleweke kuwa baadhi ya simu (handsets) haziwezi kupata huduma hiyo kwa kuwa hazikuundwa maalum kupokea mawasiliano ya tovuti.

  BBC haitozi fedha kwa wanaotumia huduma ya wavuti kupitia simu za mkononi, ni bure kwa kila mtu. Lakini unatakiwa kuzingatia kuwa makampuni ya huduma ya simu za mikononi au PDA kwa kawaida hutoza gharama kutumia huduma ya internet. Lakini hutofautiana kutoka kampuni moja hadi nyingine. Kuna uwezekano ukatozwa na kampuni yako ya simu gharama ambazo hujulikana kama “data charges”.

  Endapo huna uhakika wa uwezekano wa kutozwa fedha kwa kutumia tovuti kwenye simu yako, tafadhali wasiliana na kampuni inayokupa huduma ya simu. Lakini kwa kuwa taarifa ni za maandishi pekee bila picha, sauti au video, gharama yake inaweza kuwa ni ndogo.

  Toleo la wavuti ya BBC Swahili mobile linapatikana kupitia simu za mkononi, PDA na vifaa vingine vya mawasiliano ya mkononi. Kutakuwa na taarifa za matukio na vile vile soka. Wakati wa michuano ya kombe la mataifa ya Afrika nchini Angola, mwanzoni mwa mwaka ujao, utaweza kupata taarifa za moja kwa moja.

  Huduma kama hii pia inapatikana kutoka Idhaa nyingine za BBC zinazorusha matangazo Afrika katika lugha kama Kisomali, Kihausa, Kinyarwanda, Kireno na Kifaransa.

  http://www.bbcswahili.com/mobile
   
Loading...