BBC na DW kinachoendelea Marekani hamkioni?

Usinionee Chief! Yaani Kama umombo haupandi ndo ushamba[emoji41]

Nachojiuliza ni kwamba hizi idhaa zipo kuripoti habari zinazopatikana maziwa makuu tu na hazitakiwa kuripoti kwa undani habari zinazotokea huko kwingine ili wana na binti wa maziwa makuu nao wahabarike kwa undani na habari hizo?
 
Kwa hiyo hizi idhaa malengo yake ni kutafuta habari mbaya mbaya za Afrika na kuzipeleka duniani ila kutuletea kinachoendelea duniani kwa lugha yetu tuelewe sio malengo?
Kuzipeleka dunia ipi? Ushawahi kusikiliza BBC hausa huku Tanzania?BBC Swahili hata Zambia haisikiki sasa dunia ipi unaongelea. Ushawahi ona BbC world wanaizungumzia Tanzania? Halafu kama kuna ubaya je unazushwa au kuna ukweli? Kama kuna ukweli basi tujirekebishe ila kama wanatusingizia sawa.
 
linganisha habari hapa....the other side of the story.hutazipata kwa cnn na bbc au dw
 
Ina maana hujui tofauti ya BBC swahii na. BBC World au DW Swahili na DW News
 
Naona eti umebadilisha maudhui katika mada yako hapo juu na kuondoa BBC. Ndio ushamba wenyewe huo.
 
BBC na DW ni propagandists kama zilivyo CNN na skynews kwa sababu wamelalia magharibi ,mno kuliko hata uhalisia wenyewe
 
Ukitaka kuona Sag la kinachoendea USA, We tune media zao tu kama Fox news, MSNBC, NBC na CNN haswa Ant Trump media ndio unakuwa zinafanya coverage tena live muda wote kama msbnc mpaka zile press za Governor zinarushwa live ila ukienda kwa hizo Bbc world au Aljazera au DW wao wana mambo mengi ya kureport japo pia nimeona wana report na analysis wanafanya pia kama inside story Aljazera
 
Hata ya Kiswahili wanatangaza kila siku
Jiwe kajaribu Watanzania wengi sana na propaganda zake..hivi kuna habari inayotangazwa zaidi ya hayo maandamano ya Marekani Sasa hivi? Hata Corona imesahaulika..
 
Mbona hata ya Kiswahili ndio habari kuu siku hizi,
 
Wewe una shangaa BBC na DW, mimi mpaka sasa wanaharakati wa haki za binaadamu sijawasikia kabisa au labda Ulaya hawapo.

Wala viongozi wa mataifa makubwa wakikemea uvunjivu wa haki za binadamu au labda mkubwa mwenzao.
Sababu hufuatiliagi habari, mbona Amnesty International na Human Rights Watch wameongea against matumizi ya jeshi?
 
Haha tatizo ni ushamba wako, BBC wana BBC inayoshughulikia mambo ya Afrika, wanayo ya marekani na sehemu nyingine. Fungua ya kiinereza utaona wamereport sana kuhusu yanayoendelea marekani, tena updates kibao kila baada ya masaa machache. DW pia same. We kama umesubscribe kwenye BBC Swahili unategemea upate habari zipi?
 
 
BBC Swahili gani hisiyo update Kinachoendelea angalia vichwa vya Habari kubwa nyingi ni za ughaibuni sasa hivi labda hauna bando
 


Siku Gadafi kadhalilishwa na kuuawa kupitia Mjaluo/Obama, je mlithubutu kupiga kelele waafrika na duniani kote waandamane?? Au yule sio ndugu yetu? Ila ya FLOYD ndio yana umuhimu kuliko ya Gadafi? Watu wa waajabu ninyi cjapata kuona!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…