Bazazi
JF-Expert Member
- Aug 18, 2008
- 2,806
- 3,526
Nipo na mpenzi kwa muda sasa. Siku moja nikaiona nywila (password) ya simu yake na niliyoyakuta ndio niliyoyakuta. Ugomvi ukawa mwingi, sikumpiga bali niliminya si kidogo. Jamaa aliyekuwa anawasiliana (tumuite JAMES JESSE) na hatua ilikuwa imefikia patamu kwani ilikuwa inatafutwa siku ya utamu. Baada ya ugomvi, waliendelea na mawasiliano ila ni demu ndo apigaye simu ingawa sikuwa najua.
Ila kwa sababu Bazazi ni Bazazi, nilijua kuwa wanawasiliana kwa sana tena mno. Nikapiga biti si kitoto. Namba ikafutwa simuni. He! Kumbe bhana Bazazi anazungukwa, namba haikufutwa bali imebadilishwa jina na kupewa la kike. Ila kwa kuwa Bazazi ni Bazazi nikajua na kuuliza kwanini umebadili jina ilhali ulisema umefuta namba!? Hakuna jibu naye akahamia chumba kingine.
Bazazi akawasiliana na wenye akili kwa kigezo cha umri. Binti anasema anataka kurudi kwao. Bazazi amemruhusu akitaka arudi tu kwao maana maisha yana thamani kuliko papuchi.
Hata hivyo, Maamuzi rasmi yakakuwa tar 15/03/2020 baada ya Ibada ya kwanza. Bazazi atawajuza nini kitajiri maana anaweza kuwa jimbo huru hivyo kuruhusu mabinti wa JF kutuma maombi ya kuliwania.
Kesho sio mbali, tutajuzana yatakayojiri