Bazara kivuli la Mbowe laanza kuitia kiwewe CCM

Bazara kivuli la Mbowe laanza kuitia kiwewe CCM

Dingswayo

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2009
Posts
4,019
Reaction score
2,931
BARAZA jipya la mawaziri kivuli lililotangazwa juzi na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, limeanza kukitia kiwewe Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Daima Jumapili limebaini.

Mbowe alilisuka upya baraza lake kwa kuwashirikisha wabunge wa vyama vya CHADEMA, CUF na NCCR-Mageuzi ambavyo hivi karibuni vimeunda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kwa lengo la kuishinikiza CCM isihodhi mchakato wa katiba mpya.

Baraza hilo limeunda siku moja baada ya Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila, kuwatuhumu vigogo sita wa serikali wakiwemo mawaziri kuwa walishiriki katika ufisadi wa sh bilioni 200 zilizokuwa kwenye akaunti ya Escrow iliyofunguliwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Tanzania Daima Jumapili limedokezwa kuwa hatua hiyo imeibua hofu bungeni kwa mawaziri na vigogo hao wanaohusishwa na ufisadi wa mabilioni hayo yaliyokuwa yamewekwa kwa pamoja na IPTL na Tanesco.

Wanaotuhumiwa kuhusika na ufisadi huo ambao sasa unachunguzwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ni mawaziri Prof. Sospiter Muhongo wa Nishati na Madini, na Waziri wa Fedha na Uchumi, Saada Mkuya.

Vigogo wengine ni Gavana, Prof. Benno Ndullu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema, Katibu Mkuu Nishati na Madini, Eliachim Maswi na Mkurungenzi wa Tanesco, Felchesmi Mramba.
Vyanzo vya habari kutoka kwa baadhi ya mawaziri mjini hapa, vilidai kuwa kashfa hiyo isiposhughulikiwa vizuri na UKAWA kuamua kuibeba ajenda hiyo kwa wananchi, itawagharimu sio tu vigogo waliotajwa, bali pia itakuwa na madhara makubwa kwa CCM kwenye uchaguzi mkuu mwakani.

Habari hizo zinasema kuwa kuna hofu kubwa ya UKAWA kutumia ufisadi huo kujiimarisha na kama kweli waliotajwa wamehusika kwa namna moja au nyingine, basi kuna hatari ya vigogo hao kung'olewa.

"Jana Mbowe ameunda Baraza Kivuli na kuwaingiza baadhi ya wabunge wa vyama vingine wanaounda UKAWA. Umoja wao ni mbaya na hatari sana kwenye kashfa hii, hivyo ni vizuri serikali ikaona namna bora kulishughulikia," alisema mtoa habari wetu.

Mbunge mwingine wa CCM ambaye hakupenda jina lake litajwe, alitolea mfano wa majibu ya Waziri Mkuu kwamba yalikuwa mepesi sana kiasi kwamba yameacha maswali mengi.

"Kwa mfano mimi najua wakati fedha hizo zinachotwa, bado shauri la Tanesco dhidi ya IPTL katika Baraza la Usuluhishi la Migogoro la Kimataifa lilikuwa halijamalizika. Waliwezaje kuzichukua kabla ya kesi kumalizika?" alihoji.

Akizungumza na Tanzania Jumapili jana, Kafulila alisema hajaridhika na hatua ya serikali kupeleka suala hilo Takukuru kwa ajili ya kufanyia uchunguzi wakati inajua fika kwamba taasisi hiyo iliwahi kuwasafisha watuhumiwa wa kashfa ya Richmond na imeshindwa kuchunguza kashfa ya Katibu Mkuu wa zamani wa Nishati na Madini, David Jairo.

Alisema kuwa anajipanga kuwasilisha hoja binafsi kutaka Bunge liunde kamati teule kuchunguza tuhuma hizo.

Alisisitiza kuwa ana ushahidi wa kutosha kuhusu kashfa hiyo na kwamba yuko tayari kuutoa mahala popote atakapotakiwa.

Kwa upande wake, John Mnyika ambaye ni Waziri Kivuli wa Nishati na Madini, alisema anamsubiri kwa hamu Waziri Muhongo atakapowasilisha bajeti yake bungeni.

Alisema UKAWA lazima waibane serikali bungeni kuhusu kashfa hiyo ili ukweli ujulikane kwani kuna uwezekano mkubwa fedha hizo kutaka zitumike kwenye kampeni za uchaguzi mkuu wa CCM mwakani.

Fedha hizo ziliwekwa kwenye akaunti ya Escrow wakati shauri kati ya Tanesco dhidi ya IPTL lilipokuwa linaendelea.

Tanesco ilifungua kesi kupinga gharama za tarifu walizokuwa wakiilipa IPTL wakati huo ikiwa inamilikiwa na Kampuni ya Malaya Marcma na VIP ya hapa nchini.

IPTL hivi sasa imeuzwa kwa kampuni nyingine ya PAP baada ya wamiliki wa awali kukwaruzana.

Chanzo:Tanzania Daima
 
Tanzania eee nchi Yangu eee basi bwana rudi Tanganyika usiye na doa
 
Chadema imevaa koti la ukawa
Huu ni ukweli usiopingika na ulio wazi kabisa kwamba, chadema ndio ukawa, hawa wengine ni bendera fuata upepo tu. kama alivyosema jaji warioba kuwa tangantika imevaa koti la muungano, chadema nayo imevaa koti la ukawa...
maamuzi na nafasi muhimu za ukawa zimechukuliwa na viongozi wa chadema, hawa wenzangu na mie, wanazugwa tu ili nao wajione ni sehemu ya ukawa kumbe watu wana mambo yao nyuma ya pazia....hebu fikiria, mwenyekiti wa ukawa bungeni ni freeman mbowe, mwenyekiti wa ukawa nje ni dr W. Slaa..kwanini mwenyekiti mmoja asitoke chama kingine? Na unafahamu fika kuwa hakuna jambo linaweza kuamuliwa au kufanyika bila mwenyekiti kuamua au kukubali...
Hapa ndio ukweli mchungu unapoonekana kwamba chadema imevaa koti la ukawa...hutaki unaacha.
Source: wachambuzi makini wa mambo ya kisiasa nchini.
 
Acha upuuzi wew wakat makamu mwenyekit wa ukawa ni pro. lipumba
 
Kwa hili UKAWA mnastahili pongezi.UMOJA WENU NDIO UTAUONDOA CCM MADARAKANI,NDIO MAANA CCM WANAUBEZA ILI MVUNJIKE MOYO WAENDELEE KUTUFISADI.
 
Sijaelewa vizuri nafikili ni kwa sababu sijaenda shule zaidi nafikili tunaona mwisho cha chadema katika binge hili la bajeti chama chetu chadema litabaki jina tu tutatembelea kilichofanyika mwaka 2010 maana sina hakika kama Cuf watapinga muswaada wowote kwa niaba ya nafasi yao ktk serikali pia mh Mbatia nae anatudanganya serikali ya ccm imeonyesha ni ya muungano na vyama vya siasa vingine kama Nccr mageuzi pia chadema hivyo hawa wanasiasa wanatudanganya tuu hawa hua hawana dhamila ya kweli nao waongo tu hao
 
chadema imevaa koti la ukawa
huu ni ukweli usiopingika na ulio wazi kabisa kwamba, chadema ndio ukawa, hawa wengine ni bendera fuata upepo tu. Kama alivyosema jaji warioba kuwa tangantika imevaa koti la muungano, chadema nayo imevaa koti la ukawa...
Maamuzi na nafasi muhimu za ukawa zimechukuliwa na viongozi wa chadema, hawa wenzangu na mie, wanazugwa tu ili nao wajione ni sehemu ya ukawa kumbe watu wana mambo yao nyuma ya pazia....hebu fikiria, mwenyekiti wa ukawa bungeni ni freeman mbowe, mwenyekiti wa ukawa nje ni dr w. Slaa..kwanini mwenyekiti mmoja asitoke chama kingine? Na unafahamu fika kuwa hakuna jambo linaweza kuamuliwa au kufanyika bila mwenyekiti kuamua au kukubali...
Hapa ndio ukweli mchungu unapoonekana kwamba chadema imevaa koti la ukawa...hutaki unaacha.
Source: Wachambuzi makini wa mambo ya kisiasa nchini.

maneno mengi lakini pumba tupu ! Haya tumekusikia so what ?
 
Hakuna jipya hapa, kazi ya tz daima ni kumsifia mbowe tu
 
Billioni 200!!!!!!!!!! Nawaza mchana ntakula nini mimi,inauma sana.Tumelogwa na nani sisi??????
 
Chadema imevaa koti la ukawa
Huu ni ukweli usiopingika na ulio wazi kabisa kwamba, chadema ndio ukawa, hawa wengine ni bendera fuata upepo tu. kama alivyosema jaji warioba kuwa tangantika imevaa koti la muungano, chadema nayo imevaa koti la ukawa...
maamuzi na nafasi muhimu za ukawa zimechukuliwa na viongozi wa chadema, hawa wenzangu na mie, wanazugwa tu ili nao wajione ni sehemu ya ukawa kumbe watu wana mambo yao nyuma ya pazia....hebu fikiria, mwenyekiti wa ukawa bungeni ni freeman mbowe, mwenyekiti wa ukawa nje ni dr W. Slaa..kwanini mwenyekiti mmoja asitoke chama kingine? Na unafahamu fika kuwa hakuna jambo linaweza kuamuliwa au kufanyika bila mwenyekiti kuamua au kukubali...
Hapa ndio ukweli mchungu unapoonekana kwamba chadema imevaa koti la ukawa...hutaki unaacha.
Source: wachambuzi makini wa mambo ya kisiasa nchini.

We unatetea tu,nchi imeibiwa mamilioni we umeng`ang`ana tu,sijui una akili za kuku wa kisasa ww!yaani hujielewi kabisa.
B.200 zimechotwa BOT ww upo tu na watu wako.Watz wanaangamia na umaskini wa kutupwa pamoja na dhamana ya kuongoza mliopewa na wananchi lakini mmejisahau sana,2015 mtakumbushwa
 
Hebu watanzania tuamke na kuwaunga mkono UKAWA.ingekuwa UKAWA hawana Sera na ushawishi ccm wazingeenda kuwa kujibu mapigo.
 
Back
Top Bottom