RUCCI
JF-Expert Member
- Oct 6, 2011
- 1,701
- 1,714
Mwenyekiti wa Baraza la Waganga Tanzania Shaka Mohamed Shaka alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu waganga wanaokiuka taratibu na sheria zilizowekwa na Serikali juu ya utoaji huduma ya tiba asili nchini.
‘’Sisi kama Baraza la Waganga Tanzania tukishirikiana na Serikali tunatoa wito kwa vyombo vya habari wasitoe matangazo ya waganga wa tiba asili kwakua jambo hili ni kosa kwa mujibu wa sheria”alisema Shaka.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Baraza hilo David Witekye ameiomba radhi Serikali kutokana na tamko la Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Tiba Asili Tanzania (SHIVYATIATA) Abdulraham Lutenga kwa kuitisha mkutano na waandishi wa habari bila kushirikiana na kamati yake tendaji wala vyama vinavyounda shirikisho hilo na kuwatetea wafanyabiashara wa tiba asili ambao wamejivika kilemba cha utabibu asili.
“Kwa niaba ya BAWATA, tunaiomba radhi Serikali kutokana na tamko la Mwenyekiti wa SHIVYATIATA kupinga tamko la Serikali, tunaamini lile ni tamko lake binafsi na sio la shirikisho”. alisema Wiketye.
Ameongeza kuwa,wameafiki tamko la Serikali kuhusu upimaji na usajili wa dawa asili na kupendekeza zoezi hili kuangaliwa upya ili kuwezesha watabibu asilia kumudu gharama hizo.
Tamko hilo lilitolewa baada ya kujitokeza kwa changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na watoa huduma wa tiba za asili kutozingatia Sheria, Kanuni na miongozo mbalimbali inayohusu afya ya jamii.