BAVICHA wakunwa na Lema nje ya Bunge.

Baba Clara

Member
May 10, 2011
94
0
KUTOKA GAZETI LA MAJIRA LA LEO JUMAPILI UK4.

Umoja wa vijana wa Chadema(BAVICHA) wamesema rufaa iliyompa ushindi mbunge wa arusha mjini Godbless Lema ni fundisho kwa vyama vya siasa hususani chama cha mapinduzi(CCM) kazi ambayo ameifanya akiwa nje ya bunge ya kuimarisha chama chake ni kubwa tofauti na wenye mawazo kwamba mbunge akiwa nje ya bunge kumdhoofisha.

"Hii ni fundisho kwa vyama vya siasa kazi aliyofanya Lema ya kuimarisha chama kipindi ambacho alikuwa nje ya bunge ni mwiba kwa CCM"

Kauli hiyo ilitolewa Dar es salaam jana na katibu mkuu wa Bavicha mkoa wa Mwanza Salvatory Magafu, wakati akizungumza na gazeti hili kuhusiana najinsi walivyopokea uamuzi wa mahakama ya rufaa Tanzania kwa kumrejeshea ubunge wake Lema.

Alisema jambo hilo lilikuwa wazi labda kwa mgeni wa fani ya sheria. Alifafanua kuwa sheria inaweza kuwa katika kesi ya udhalilishaji anayelalamika na mhusika, lakini jambo hilo halikufanyika kwenye kesi hiyo.

Aliongeza kwamba kwa maoni yake mahakama kuu kanda ya Arusha ilihukumu shauri hilo kisiasa. "Uwamuzi uliotolewa ni maamuzi mazuri" alisema. Kuhusu kazi ya Lema ambayo aliifanya akiwa nje ya bunge Magafu alisema: "inauma Lema kurudi bungeni, kwani kazi aliyoifanya akiwa nje ni kubwa amesaidia kukuza chama....tunaweza kusema ni pigo kwa chama".

Alisema Chadema itaathirika kwa kiasi fulani kwa kipindi ambacho atakuwa bungeni kwani atakuwa hana nafasi ya kukiimarisha chama hicho, ikilinganishwa na kipindi ambacho amekuwa nje.

Kwa upande wake katibu wa Bavicha mkoa wa Tanga Deogratius Kisandu, alisema uamuzi wa mahakama kumurejeshea Lema ubunge fundisho kwa serikali kuwa watu wengine wakivuliwa ubunge wanamwaga sumu nchi nzima.

Alisema baada ya kurejeshewa ubunge nguvu sasa atazielekeza bungeni na jimboni kwake. Alisema hukumu iliyompa ushindi Lema inaleta picha kuwa mahakama haiwezi kupingana na nguvu za ukweli.

Alifafanua kuwa tangu awali mbunge huyo alikuwa akipigana kutafuta ukweli ambao sasa amerejeshewa na mahakama.
 

Lokissa

JF-Expert Member
Nov 20, 2010
7,445
2,000
Kamanda Lema kaza buti hadi kieleweke. Ivi watokea makamanda 10 kama Lema ssm itaweka wapi uso. Nadhani hata watoto wa wakubwa walihodhi mali za watz wangeanza kuzirudisha kabla ya 2015. Watz wangepata hata ahuheni kama wakina mama wanaojifungulia njiani kwa sababu wamekosa hata lori la kuwabeba ee Mung njoo haraka. Watoto wanaopata malaria, homa kali, n.k wanafia njiani kwa sababu ya kukosa hata lori au kenta ya kuwabeba. I am saying malori kwa sababu nikisema ambulance najihisi kama nitakuwa mbali mno. Tz ni zaidi uijuavyo!!
 

DALLAI LAMA

JF-Expert Member
Jan 31, 2012
8,640
2,000
Magafu na Kisandu hongera kwa pongezi zenu kwa lema ila nyie ni MASALIA wa Kuwadi ZITTO,tunawasaka mno.
 

Dik

JF-Expert Member
Nov 15, 2011
1,204
1,195
Yule ni jembe syo kama nyie wa kutumiwa na kutupwa kama kondom
 

democratic

JF-Expert Member
Nov 21, 2011
1,642
0
wewe magafu naye unapongeza,au wamekunyima mafao yako huko ugambani? any way asante kwa pongezi,tunazipokea lakini kwa tahadhari kubwa
 
Sep 27, 2012
32
0
Tunasubiri tamko juu yenu wote mlio onyesha usaliti ndani ya chama nazani tamko linatoka mwezi january na tena acheni unafiki wa kupongeza mafanikio ya chama wakati ww mamuluki
 

Ritz

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
42,916
2,000
Bavicha wote njaa tupu hawa ndiyo watakaoizamisha Chadema kwenye uchaguzi mwaka 2015.
 

yegella

JF-Expert Member
Nov 18, 2010
3,113
1,250
lema kasha tengeneza akina lema kama 20 subiri january nani anamjua Bananga, Mawazo...kuna vija wana pasha kuchukua majimbo mbalimbali na wameiva
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom